• Wasiliana nasi |
    • Maswali na majibu |
    • Baruapepe - Watumishi |
    • eVibali |
    • Malalamiko |
Dodoma City Council
Dodoma City Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Jiji la Dodoma

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa taasisi
    • Idara
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Mipango, Takwimu na Ufuatiliaji
      • Afya
      • Fedha na Biashara
      • Elimu ya Msingi
      • Elimu ya Sekondari
      • Maji
      • Kilimo, Umwagiliaji na Ushirika
      • Mifugo na Uvuvi
      • Ardhi na Mipango Miji
      • Maendeleo ya Jamii, Ustawi wa Jamii, Jinsia na Vijana
      • Ujenzi
      • Mazingira na Udhibiti wa Taka ngumu
    • Vitengo
      • Sheria na Usalama
      • Mkaguzi wa Ndani
      • TEHAMA na Uhusiano
      • Manunuzi
      • Uchaguzi
      • Ufugaji Nyuji
    • Ward
  • Fursa za Uwekezaji
    • Maeneo ya Utalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
    • Mji wa Serikali
    • Kwa nini uwekeze Dodoma?
  • Huduma Zetu
    • Maendeleo ya jamii
    • Elimu
    • Miundombinu
    • Mazingira
    • Afya
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Fedha na Utawala
      • Mipango miji na Mazingira
      • Uchumi, Afya na Elimu
      • Kudhitibi UKIMWI
      • Maadili
    • Kamati zingine/Bodi/Uwakilishi
    • Ratiba
      • Vikao vya Madiwani
      • Kuonana na Mstahiki Meya
  • Miradi
    • Miradi itakayotekelezwa
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Ripoti
    • Sheria Ndogo
    • Miongozo
    • Mpango Mkakati
    • Fomu
    • Jifunze Nyumbani
    • Mpango Kabambe
    • Jarida
    • Asemavyo Mahia - Afya na Mazingira
  • Kituo cha habari
    • Taarifa kwa vyombo vya habari
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya picha
    • Habari
    • Matukio
  • City TV

Senyamule awasisitiza wanufaika wa TASAF kutumia pesa kujiletea maendeleo

Imewekwa tarehe: February 14th, 2025

Na. Aisha Ibrahim, DODOMA

Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Rosemary Senyamule, amewataka wanufaika wa Mfuko wa Maendeleo ya Jamii (TASAF) kutumia vizuri pesa wanayopewa na mfuko huo katika kufanyia shughuli mbalimbali za kuingiza kipato ili kujikwamua kiuchumi na kuondokana na dhana ya kuwa tegemezi katika jamii na taifa kwa ujumla.

Aliyasema hayo wakati akiwa kwenye ziara fupi ya kutembelea wanufaika wa Mfuko wa TASAF katika mtaa wa Mchemwa, Kata ya Makutupora, jijini Dodoma iliyokwenda na Kaulimbiu isemayo ‘TASAF, kwa pamoja tuondoe umaskini’.

Akizungumza wakati wa ziara hiyo, alisema kuwa miongoni mwa malengo ya TASAF ni kuhakikisha wanajamii wenye kipato cha chini wanainuka kiuchumi na kuwa na kipato cha juu ili kusaidia kuinua vipato vyao na familia zao kwa ujumla. “Mfuko wa TASAF umekuja ili kuwafanya wale wenye kipato cha chini kuongezeka na kuanza kupata kipato cha juu” alisema Senyamule.

Katika hatua nyingine, aliwahimiza wanufaika wa mfuko huo kuipa thamani pesa hiyo kwa kufanyia shughuli za maendeleo kwasababu malengo ya TASAF hayawezi kutimia ikiwa walengwa hawatakuwa na utayari wa kufanikisha dhamira hiyo. “Dhamira hii haiwezi kutimia ikiwa mlengwa hajataka kuitimiza kwasababu leo tunaweza kusema tugawe laki moja kwa kila mtu lakini yule mwenye dhamira tutakuta pesa hiyo imeongezeka na imekuwa laki mbili” alisema Senyamule.

Kwa upande wake, Mratibu wa TASAF ngazi ya Halmashauri ya Jiji la Dodoma, Sekunda Kasese alifafanua kuwa katika Mtaa wa Mchemwa kuna kaya 25 zenye wanufaika wa mfuko huo ambao wanapokea pesa hizo kwa njia ya benki na wengine hupokea pesa taslimu.

Nae, mkazi wa Mtaa wa Mchemwa ambae ni mnufaika wa TASAF, Esther Chitojo, mwenye umri wa miaka 68, aliushukuru mfuko huo kwa kuwawezesha na kuwasaidia kuinua vipato vyao kwasababu wameweza kupiga hatua moja kwenda hatua nyingine kimaendeleo. “Nimeshukuru kuletwa kwa TASAF kwasababu imeweza kutuinua sana na maisha yetu yanaenda vizuri” alisema Chitojo.

Sambamba na hayo, alieleza kuwa kupitia pesa anazopata kutoka TASAF aliweza kununua mbuzi wawili walioweza kuzaliana na kufikia mbuzi 12 na baadae alibadirisha mbuzi hao na kupata ng'ombe jike wawili ambao hadi sasa wamezaliana na kufikia ng'ombe 12 wanaotoa maziwa ya kuuza na kumfanya aweze kujipatia Kipato.

Mbali zaidi, alisema kuwa aliweza kuanzisha kilimo cha zao la Choya ambapo baada ya mavuno hupeleka sokoni kuuza na kupitia fedha hizo alifanikiwa kujenga nyumba yenye vyumba vitatu na sebule moja. “Kupitia fedha ninazopata kutoka TASAF nilianzisha kilimo cha Choya na huwa ninauza pamoja na maziwa. Kwahiyo, kwa kuweka pesa kidogo kidogo nilianza kununua simenti, nikafyatua tofali lakini mwaka jana niliuza ng'ombe wawili nikanunua mbao na mabati na nilifanikiwa kujenga nyumba yenye vyumba vitatu na sebule” alisema Chitojo.

Malengo ya mfuko wa TASAF ni kuzinusuru kaya maskini zaidi kwa kuongeza vipato na fursa za kujikimu, kuboresha huduma za kiuchumi na kijamii, kuimarisha lishe bora, kuongeza mahudhurio ya watoto shuleni, na kuhakikisha upatikanaji wa huduma za afya.

Matangazo

  • MKUTANO WA BARAZA LA WAHESHIMIWA MADIWANI January 30, 2025
  • KITUO CHA AFYA ILAZO KIMEANZA KUTOA HUDUMA January 13, 2025
  • HOSPITALI YA JIJI LA DODOMA IMEANZA KUTOA HUDUMA ZA AFYA January 12, 2025
  • TANGAZO LA UUZWAJI WA VIWANJA KIKOMBO December 03, 2024
  • Angalia zote

Habari za hivi punde

  • Barabara ya Lami ya Kilometa 6 yawanufaisha wakazi wa Kata ya Miyuji

    April 23, 2025
  • Huduma ya Chakula na Lishe yapandisha ufaulu Shule ya Sekondari Nala

    April 22, 2025
  • Mradi wa Maji Nala wa Bil. 1.3, mkombozi kwa wananchi

    April 22, 2025
  • Milioni 500 kukamilisha mradi wa Kituo cha Afya Kizota

    April 22, 2025
  • Angalia zote

Video

Watendaji Kata Wilaya ya Dodoma watakiwa kusimamia maswala ya Lishe
Video zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • Historia ya Manispaa
  • Wasifu wa Manispaa
  • Kata na Madiwani
  • Mji wa Serikali
  • Orodha ya Madiwani
  • Mpango Mkakati wa Halmashauri (SP)
  • Kwanini uwekeze Dodoma?
  • Zabuni za Wakala wa Ukusanyaji Mapato
  • Zabuni ya Usafi wa Mazingira

Viunganishi Linganifu

  • Msalato Sekondari
  • Mkoa wa Dodoma
  • OR-TAMISEMI
  • Utumishi
  • Chuo Kikuu Dodoma (UDOM)
  • Bunge

World visitors tracker

world map hits counter

Idadi ya watembeleaji

free HitCounter

Ramani elekezi

Wasiliana nasi

    1 CDA Street, 40477

    Anuani ya posta: 1249, DODOMA, TANZANIA

    Simu: +255 26 232 4817

    Simu ya kiganjani:

    Baruapepe: cd@dodomacc.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya tovuti

Copyright ©2017 The City Council of Dodoma. All rights reserved.