Na. Dotto Mwaibale, DAR ES SALAAM
WAZIRI wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Nape Nnauye amesema Serikali inadhamira ya dhati ya kuboresha sekta ya habari nchini.
Nnauye ameyasema hayo wakati akifungua kongamano la maendeleoya ya sekta ya habari 2022 linaloendelea Ukumbi wa Mikiutano wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaaam.
Alisema serikali ina kila sababu ya kuboresha mazingira bora ya vyombo vya habari kutokana na umuhimu wake hasa katika maendeleo na kuinua uchumi wa nchi.
Nnauye alisema kuwa mwaka ujao wa 2023 Serikali imekusudia kuongeza nguvu zaidi katika kuboresha maslahi ya wanahabari ikiwa ni pamoja na kusimamia mikataba ya ajira zao na kulipwa madeni yao kutoka taasisi mbalimbali zikiwemo halmashauri za wilaya.
Katika hatua nyingine Nnauye amevitaka vyombo vya habari kutimiza wajibu kwa kufanya kazi zao kwa kuzingatia maadili na kulinda lasirimali za nchi na pale zinapotumika vibaya waendelee kuwafichua wabadhirifu.
Aliwaomba waandishi wa habari kuendelea kushirikiana na Serikali katika shughuli mbalimbali ili kuliletea taifa maendeleo na kukuza uchumi wa nchi na kueleza kuwa kongamano hilolitakuwa endelevu ambapo alipendekeza liitwe kongamano la kimataifa la maendeleo ya sekta ya habari badala ya kongomano la maendeleo ya sekta ya habari.
Mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri wa Habari Tanzania (TEF) akizungumzia changangomo kadhaa zinazowakabili waandishi wa habari sambamba na madeni wanayodai alisema bado kunachangamoto kubwa ya ulipwaji wa madeni hayo.
“Mpaka sasa madeni ambayo vyombo vya habari vinadai kwa serikali na taasisi zake zikiwepo halmashauri ni zaidi ya Sh. 7 bilioni na ukijumlisha na deni la Gazeti la Daily News la serikali inakuwa Sh. 11 Bilioni hivyo kulifanya deni lote kufikia Sh. 18 Bilioni,” alisema Balile.
Katika kongamano hilo Wazri Nape alipata fursa ya kutoa tuzo kwa waandishi wa babari 10 na taasisi za serikali 10 waliofanya vizuri katika utoaji wa habari na kuandika habari na makala kwenye taasisi hizo ambapo Wizara ya Madini imetoa tuzo kwa baadhi ya waandishi.
Waandishi waliotunukiwa tuzo hizo ni pamoja na Nelly Mtema (Daily News), George Binagi (BMG Media) na Mohammed Zengwa (Global TV).
Kongamano hilo la siku moja linakutanisha wadau wa habari ikiwa ni pamoja na wahariri na wamiliki wa vyombo vya habari, jukwaa la wahariri wa habari, maafisa habari kutoka Serikalini, Taasisi Binafsi na Mashirika ya Kimataifa.
Aidha, pia katika kongamano hilo zilitolewa mada mbalimbali kutoka kwa Dk. Rose Reuben kutoka TAMWA, Muadhiri wa Dipromasia Deus Kibamba, Kajubi Mkajanga kutoka Baraza la Habari Tanzania (MCT) Heliet Shija kutoka Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA), Mkurugenzi Msaidizi wa Idara Habari (MAELEZO) Rodney Tadeus na Mkurugenzi wa Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC) Dkt. Ayoub Ryioba.
1 CDA Street, 40477
Anuani ya posta: 1249, DODOMA, TANZANIA
Simu: +255 26 232 4817
Simu ya kiganjani:
Baruapepe: cd@dodomacc.go.tz
Copyright ©2017 The City Council of Dodoma. All rights reserved.