NAIBU WAZIRI Ofisi ya Rais Tamisemi anayeshughulikia Elimu, Zainabu Katimba (Mb) amsema Serikali inatambua umuhimu wa uzio kwenye shule za bweni za wasichana nchini kwaajili ya usalama wa mali na wanafunzi zikiwemo shule za Halmashauri ya Wilaya ya Urambo.
Aidha, kwa sasa kipaumbele cha serikali ni ujenzi wa miundombinu ya msingi inayowezesha wanafunzi wote kupata fursa ya elimu.
Katimba amesema hayo Bungeni Jijini Dodoma katika kipindi cha maswali na majibu, wakati akijibu swali Mheshimiwa Jacqueline Kainja Andrew, Mbunge wa Viti Maalumu Mbunge wa Viti Maalumu alieuliza Je, kuna mpango gani wa kujenga uzio kwenye Shule zote za Bweni za Wasichana Wilayani Urambo.
“Serikali itapeleka shilingi bilioni 2.4 katika Jimbo la Urambo kwa ajili ya ujenzi wa miundombinu mbalimbali yakiwemo madarasa 16, mabweni 8 na matundu ya vyoo 20 katika shule mbili za sekondari mpya za kata katika Kata ya Nsenda kijiji cha Mtakuja na Kata ya Ukandamoyo kijiji cha Tumaini. Aidha, kwa mwaka 2024/25 zimetengwa jumla ya shilingi milioni 110 kwa ajili ya ujenzi wa nyumba ya walimu ya“two in one” ambayo itajengwa katika Kata ya Uyogo”Katimba.
Aidha Katimba amemelekeza Mkurugenzi wa Halmashauri ya Urambo kufanya Tathimini na kuweka katika mipango ya kibajeti inayotokana na Mapato ya Ndani ya Halmashauri kutenga fedha kwaajili ya Ujenzi wa Uzio katika shule ya Sekondari Iyumbu.
Amesema pia Serikali kwa kushirikiana na wadau mbalimbali itaendelea kutenga na kupeleka fedha kwa ajili ya ujenzi wa miundombinu ya shule za msingi na sekondari kulingana na vipaumbele vyake.
1 CDA Street, 40477
Anuani ya posta: 1249, DODOMA, TANZANIA
Simu: +255 26 232 4817
Simu ya kiganjani:
Baruapepe: cd@dodomacc.go.tz
Copyright ©2017 The City Council of Dodoma. All rights reserved.