NAIBU Waziri, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe. Festo Dugange (Mb) amesema Serikali itaendelea kufanya ukarabati wa vituo vya afya Nchini kwa kuhakikisha huduma bora za afya kwa Wananchi zinapatikana.
Mhe. Dkt Dugange amesema hayo katika kipindi cha maswali na majibu Bungeni Jijini Dodoma, wakati akijibu swali la Mbunge wa Viti Maalumu Mhe. Mariam Madulu Nyoka, aliyeuliza Je, Serikali ina mpango gani wa kukarabati kituo cha afya Mji Mwema hasa Wodi za akina Mama, Wanaume na OPD?
“kituo cha afya Mji Mwema kilichopo katika Manispaa ya Songea kilijengwa mwaka 1982 kituo hiki ni miongoni mwa vituo vya afya 202 vilivyofanyiwa tathmini kwa ajili ya ukarabati mkubwa na kuongeza miundombinu ili kuendana na mahitaji ya sasa ya utoaji wa huduma za afya”
Amesema katika mwaka wa fedha 2022/2023 na 2023/2024 kituo cha afya Mji Mwema kilipelekewa shilingi Milioni 35 kutoka mapato ya ndani ya Halmashauri pamoja na wadau wa huduma rafiki kwa Vijana kwa ajili ya ukarabati ambapo Majengo yaliyo karabatiwa ni Wodi ya Wanawake na Watoto, Jengo la huduma ya uzazi na mtoto (RCH), Wodi ya Wanaume na jengo la huduma za Wagonjwa wa nje (OPD).
Aidha amesema pia katika mwaka wa fedha 2024/2025 kituo kimetenga shilingi Milioni 28 kwa ajili ya kukamilisha ukarabati wa jengo la huduma za Wagonjwa wa nje na wodi ya wanaume.
1 CDA Street, 40477
Anuani ya posta: 1249, DODOMA, TANZANIA
Simu: +255 26 232 4817
Simu ya kiganjani:
Baruapepe: cd@dodomacc.go.tz
Copyright ©2017 The City Council of Dodoma. All rights reserved.