• Wasiliana nasi |
    • Maswali na majibu |
    • Baruapepe - Watumishi |
    • eVibali |
    • Malalamiko |
Dodoma City Council
Dodoma City Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Jiji la Dodoma

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa taasisi
    • Idara
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Mipango, Takwimu na Ufuatiliaji
      • Afya
      • Fedha na Biashara
      • Elimu ya Msingi
      • Elimu ya Sekondari
      • Maji
      • Kilimo, Umwagiliaji na Ushirika
      • Mifugo na Uvuvi
      • Ardhi na Mipango Miji
      • Maendeleo ya Jamii, Ustawi wa Jamii, Jinsia na Vijana
      • Ujenzi
      • Mazingira na Udhibiti wa Taka ngumu
    • Vitengo
      • Sheria na Usalama
      • Mkaguzi wa Ndani
      • TEHAMA na Uhusiano
      • Manunuzi
      • Uchaguzi
      • Ufugaji Nyuji
    • Ward
  • Fursa za Uwekezaji
    • Maeneo ya Utalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
    • Mji wa Serikali
    • Kwa nini uwekeze Dodoma?
  • Huduma Zetu
    • Maendeleo ya jamii
    • Elimu
    • Miundombinu
    • Mazingira
    • Afya
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Fedha na Utawala
      • Mipango miji na Mazingira
      • Uchumi, Afya na Elimu
      • Kudhitibi UKIMWI
      • Maadili
    • Kamati zingine/Bodi/Uwakilishi
    • Ratiba
      • Vikao vya Madiwani
      • Kuonana na Mstahiki Meya
  • Miradi
    • Miradi itakayotekelezwa
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Ripoti
    • Sheria Ndogo
    • Miongozo
    • Mpango Mkakati
    • Fomu
    • Jifunze Nyumbani
    • Mpango Kabambe
    • Jarida
    • Asemavyo Mahia - Afya na Mazingira
  • Kituo cha habari
    • Taarifa kwa vyombo vya habari
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya picha
    • Habari
    • Matukio
  • City TV

Serikali kushughulikia maslahi ya watumishi, kumwaga ajira 40,731

Imewekwa tarehe: April 15th, 2021

SERIKALI imesema kuwa itahakikisha inazingatia  maslahi ya watumishi wa Umma ikiwemo nyongeza ya mishahara, malipo ya wastaafu na kupandiswa kwa madaraja kwa mujibu wa sheria huku inakusudia kutangaza ajira mpya zipatazo 40,731.

Hayo yamebainishwa na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais-Utumishi na Utawala Bora, Mohammed Mchengerwa wakati akifungua Mkutano wa Pili wa Baraza Kuu la Nne la Wafanyakazi Katika Utumishi wa Umma uliofanyika leo April 14,2021 jijini Dodoma. 

Mhe.Mchengerwa amesema kuwa masuala kama nyongeza ya mishara, kupandishwa kwa madaraja ya watumishi, malipo ya wastafu ni mambo ambayo yapo kwa mujibu wa sheria hivyo utekelezaji wake ni wa lazima na siyo hiyari.

“Mtumishi kuongezwa mshahara, kupandishwa madara au kupandishwa vyeo haya yapo kwa mujibu wa sheria na siyo ombi wala huruma ya mwajiri wake hivyo tutahakikisha kuwa tunatekeleza kwa mujibu wa sheria inavyo elekeza”amesema Mchengerwa

Aidha Waziri Mchengerwa amesema kuwa Serikali inakusudia kutangaza ajira mpya zipatazo 40,731 katika sekta za kipaumbele na zenye changamoto za uhaba wa watumishi hizo ni  tofauti na zile 6,000 za kada ya ualimu na 2,000 za afya ambazo zenyewe zilishatangazwa.

Mchengerwa amesema kipaumbele katika ajira hizo mpya ambazo zitatangazwa kitakua katika sekta ya elimu kwa maana ya walimu wa masomo ya sayansi, hisabati na kiingereza, sekta ya afya kwa maana ya madaktari na wauguzi pamoja na sekta ya kilimo.

” Huu ni mpango wa Serikali inayoongozwa na Rais wetu Samia Suluhu Hassan, lengo letu tunafahamu kuwepo kwa changamoto ya ajira nchini lakini kwa kuanza tutatangaza hizo chache, niwaahidi watanzania kwamba serikali itaendelea kuweka bajeti ya kuhakikisha kila mwaka kunakua na ajira mpya.

Kama serikali tumepanga kuwashika mkono watanzania lakini pia tumepanga kuwashika mkono watumishi wake wote, niwaombe tu wazidi kuchapa kazi kwa uzalendo, uadilifu na nidhamu huku wakisimamia maadili na taratibu zote za utumishi wa umma,” Amesema Waziri Mchengerwa.

Amewataka waajiri na watumishi wote wa umma nchini kuacha matumizi ya mabavu, uonevu na ubabe na badala yake wajikite kuwahudumia watanzania kwani serikali ya Rais Samia inaamini inaweza kufanikiwa bila kutumia nguvu.

Katika mkutano huo wa Baraza la wafanyakazi, Waziri Mchengerwa amesisitiza ushirikishwaji wa watumishi katika maamuzi kwani jukumu la wafanyakazi kushirikishwa ni suala la kikatiba na liliwahi kusisitizwa na hayati Baba wa Taifa Mwalimu Julius Nyerere.

” Nitoe rai kwa Viongozi mliohudhuria baraza hili kuacha kufanya maamuzi bila kuwashirikisha watumishi wetu, niagize kwenu waajiri wote kuhakikisha mabaraza yote ya Wafanyakazi yanakua hai na katika mkutano ujao nipewe taarifa ya mabaraza yote, lengo ni kuangalia namna gani Wafanyakazi wetu wanashirikishwa katika maamuzi,” Amesema Mchengerwa.

Matangazo

  • MKUTANO WA BARAZA LA WAHESHIMIWA MADIWANI January 30, 2025
  • KITUO CHA AFYA ILAZO KIMEANZA KUTOA HUDUMA January 13, 2025
  • HOSPITALI YA JIJI LA DODOMA IMEANZA KUTOA HUDUMA ZA AFYA January 12, 2025
  • TANGAZO LA UUZWAJI WA VIWANJA KIKOMBO December 03, 2024
  • Angalia zote

Habari za hivi punde

  • Barabara ya Lami ya Kilometa 6 yawanufaisha wakazi wa Kata ya Miyuji

    April 23, 2025
  • Huduma ya Chakula na Lishe yapandisha ufaulu Shule ya Sekondari Nala

    April 22, 2025
  • Mradi wa Maji Nala wa Bil. 1.3, mkombozi kwa wananchi

    April 22, 2025
  • Milioni 500 kukamilisha mradi wa Kituo cha Afya Kizota

    April 22, 2025
  • Angalia zote

Video

Watendaji Kata Wilaya ya Dodoma watakiwa kusimamia maswala ya Lishe
Video zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • Historia ya Manispaa
  • Wasifu wa Manispaa
  • Kata na Madiwani
  • Mji wa Serikali
  • Orodha ya Madiwani
  • Mpango Mkakati wa Halmashauri (SP)
  • Kwanini uwekeze Dodoma?
  • Zabuni za Wakala wa Ukusanyaji Mapato
  • Zabuni ya Usafi wa Mazingira

Viunganishi Linganifu

  • Msalato Sekondari
  • Mkoa wa Dodoma
  • OR-TAMISEMI
  • Utumishi
  • Chuo Kikuu Dodoma (UDOM)
  • Bunge

World visitors tracker

world map hits counter

Idadi ya watembeleaji

free HitCounter

Ramani elekezi

Wasiliana nasi

    1 CDA Street, 40477

    Anuani ya posta: 1249, DODOMA, TANZANIA

    Simu: +255 26 232 4817

    Simu ya kiganjani:

    Baruapepe: cd@dodomacc.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya tovuti

Copyright ©2017 The City Council of Dodoma. All rights reserved.