RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan ambaye pia ni Mwenyekiti wa Baraza la Taifa la Biashara (TNBC), leo tarehe 26 Juni, 2021 ameongoza Mkutano wa 12 wa Baraza hilo lililojadili mambo mbalimbali ikiwa ni pamoja na masuala ya kodi, Mamlaka ya kodi, Mamlaka za udhibiti pamoja na mazao yatokanayo na misitu.
Mhe. Samia amesema Serikali itaendelea kuboresha mazingira ya Uwekezaji na Biashara nchini ili kuchangia pato la Taifa.
Amesema sekta binafsi ni mhimili muhimu wa maendeleo ya nchi kwa sababu huchangia kwa kiasi kikubwa kukuza uchumi. Pia Mhe. Rais Samia amesisitiza kuwa hakuna Taifa lolote duniani ambalo linaweza kupiga hatua ya maendeleo bila kushirikiana na sekta binafsi.
Mhe. Rais Samia amewaagiza Mawaziri wa sekta mbalimbali kukaa na kujadiliana na Wafanyabiashara wa sekta binafsi kuendelea kutatua changamoto zinazowakabili.
Aidha, Mhe. Rais amewaagiza Wakuu wa Mikoa na Wilaya ambao ni Wenyeviti wa Mabaraza hayo katika ngazi za Mikoa na Wilaya kushirikiana na Sekretarieti ya Baraza Taifa na kuhakikisha Mabaraza hayo yanafanyika kwani ndio chimbuko la mabadiliko katika ngazi ya Taifa.
1 CDA Street, 40477
Anuani ya posta: 1249, DODOMA, TANZANIA
Simu: +255 26 232 4817
Simu ya kiganjani:
Baruapepe: cd@dodomacc.go.tz
Copyright ©2017 The City Council of Dodoma. All rights reserved.