WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amesema kuwa Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Rais Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan imedhamiria kujenga vyuo vya Ufundi Stadi (VETA) katika kila halmashauri nchini.
Amesema kuwa lengo la ujenzi wa vyuo hivyo ni kuhakikisha vinatoa elimu ya ujuzi maalum kwa vijana wa Kitanzania katika maeneo mbalimbali ikiwemo utaalam wa TEHAMA, Ufundi Umeme, makenika na maeneo mengine.
Amesema hayo leo Ijumaa (Septemba 17, 2021) wakati akiweka jiwe la msingi la ujenzi wa Chuo cha Ufundi Stadi cha Wilaya Buhingwe ambacho kitagharimu shilingi bilioni 2.4 mpaka kukamilika kwake, ambapo mpaka sasa kiasi cha shilingi bilioni 1.6 zimeshatumika.
“Tulianza na ujezi wa vyuo vya VETA kimoja kimoja kila mkoa, sasa tunashuka chini kwenye kila halmashauri, chuo hiki nimeweka jiwe la msingi leo, maana yake hakitasimama, kitajengwa mpaka kikamilike kwa ajili ya vijana wetu kupata eneo la kujiongezea ujuzi”
1 CDA Street, 40477
Anuani ya posta: 1249, DODOMA, TANZANIA
Simu: +255 26 232 4817
Simu ya kiganjani:
Baruapepe: cd@dodomacc.go.tz
Copyright ©2017 The City Council of Dodoma. All rights reserved.