SERIKALI imejipanga kuhakikisha tarafa zote za Mkoa wa Dar es Salaam zinakuwa na kituo cha afya ikiwa ni lengo la Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan la kusogeza huduma za afya kwa wananchi.
Hayo yamebainishwa na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, Angellah Kairuki wakati wa kukagua miundombinu ya afya katika Halmashauri ya Jiji la Dar-es-salaam, Mkoani Dar es Salaam.
Alisema Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ameweka mkazo katika Sekta ya afya kuhakikisha tarafa zote zinakuwa na uhakika wa kuwa na kituo cha afya kwa Dar es Salaam.
Kairuki amesema kwa upande wa kata ya Kinyerezi kupitia Halmashauri ya Jiji, Serikali imetoa takribani Sh. milioni 500 kwa ajili ya upanuzi wa zahanati ya Kinyerezi kwa lengo la kupandisha hadhi zahanati hiyo na kuwa Kituo cha afya na tayari majengo manne yamekamilika ili kuanza kutoa huduma kwa wananchi.
Alisema kwa upande wa Kata ya Kimanga, Serikalli imetenga Sh. milioni 140 kwa ajili ya ujenzi wa zahanati hiyo.
"Kwa Kata ya Bunyoka tutaanza na wodi ya wazazi pamoja na kliniki ya mama na mtoto lakini kutokana na miinuko tumewaelekeza wananchi kukaa na kushauri kuona kama majengo haya yajengwe maeneo yaleyale au kupata eneo lingine."
Aidha, Kairuki amesema kuwa Kata ya Kiwalani imepelekewa Sh. milioni 500 na tayari majengo zaidi ya manne yanendelea kujengwa.
Alisema, Kata ya Segerea tayari Serikali imetenga Sh. milioni 500 kwa ajili ya ujenzi wa Kituo cha Afya cha Segerea na ujenzi unaendelea kwa jengo la wazazi, maabara, upasuaji, mionzi na kufulia ambapo Sh. milioni 150 zimeongezwa kwa ajili ya kununulia vifaa tiba.
1 CDA Street, 40477
Anuani ya posta: 1249, DODOMA, TANZANIA
Simu: +255 26 232 4817
Simu ya kiganjani:
Baruapepe: cd@dodomacc.go.tz
Copyright ©2017 The City Council of Dodoma. All rights reserved.