SERIKALI kupitia Wizara ya Afya imeongeza fedha za kusomesha Wataalamu wa fani za kibingwa na bobezi hadi kufikia shilingi Bilioni 8 kutoka Shilingi Bilioni 3 za mwaka wa fedha 2021/22, utakaosaidia kuboresha huduma kwa wananchi na kupunguza Rufaa za nje ya nchi.
Hayo yamesemwa na Waziri wa Afya Mhe. Ummy Mwalimu leo Oktoba 28, 2022 wakati akitoa taarifa kuhusu mpango wa Serikali wa kuendeleza Watumishi wa Sekta ya Afya katika fani za ubingwa na ubingwa bobezi nchini mpango huo umepewa jina la Mpango wa Samia wa kuongeza wataalamu bingwa na bobezi wa afya nchini (Samia Health Super Specialisation Programme in Tanzania)
"Kwa mwaka wa fedha 2022/23 Serikali imeongeza fedha za kusomesha Wataalamu bingwa na bobezi hadi kufikia shilingi Bilioni 8 kutoka Shilingi Bilioni 3 za mwaka wa fedha 2021/22 utakaosaidia kuboresha huduma za afya nchini. " Amesema Mwalimu
Ameendelea kusema kuwa, ili kuimarisha upatikanaji wa huduma za kibingwa na bobezi nchini kuanzia mwaka huu wa fedha, Wizara imeanzisha mkakati mpya wa kutoa ufadhili kwa watumishi wa Sekta ya Afya kwa utaratibu wa seti.
Utaratibu huu umeanzishwa ili kuhakikisha huduma za kibingwa zinazotolewa zinakuwa na wataalamu wote wanaohitajika ili huduma husika iweze kutolewa kwa ukamilifu, amesisitiza.
Aidha, Mwalimu amesema kuwa, Wataalamu watakaosomeshwa kwa ajili ya kutoa huduma ya matibabu ya figo kikamilifu katika set ni kama ifuatavyo; Daktari Bingwa wa Upasuaji Figo, Daktari Bingwa wa matibabu ya Figo, Daktari Bingwa wa utoaji dawa ya Usingizi kwa wagonjwa wa Figo.
Daktari Bingwa wa Mionzi, Muuguzi Bingwa wa Mionzi, Mteknolojia Mionzi, Muuguzi Bingwa wa Figo, Muuguzi Bingwa wa Usimamizi wa huduma za chumba cha upasuaji kwa
wagonjwa wa Figo na Mtaalamu wa Vifaa Tiba vinavyotumika kwa ajili ya matibabu ya figo, aliendelea.
Pia, Mwalimu amesema, jumla ya watumishi 139 wamechaguliwa kupata ufadhili wa masomo ambapo kati ya hao 136 watasomeshwa nje ya nchi na watatu (3) ndani ya nchi, ambapo Wizara itatoa ufadhili wa mafunzo ya seti.
1 CDA Street, 40477
Anuani ya posta: 1249, DODOMA, TANZANIA
Simu: +255 26 232 4817
Simu ya kiganjani:
Baruapepe: cd@dodomacc.go.tz
Copyright ©2017 The City Council of Dodoma. All rights reserved.