• Wasiliana nasi |
    • Maswali na majibu |
    • Baruapepe - Watumishi |
    • eVibali |
    • Malalamiko |
Dodoma City Council
Dodoma City Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Jiji la Dodoma

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa taasisi
    • Idara
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Mipango, Takwimu na Ufuatiliaji
      • Afya
      • Fedha na Biashara
      • Elimu ya Msingi
      • Elimu ya Sekondari
      • Maji
      • Kilimo, Umwagiliaji na Ushirika
      • Mifugo na Uvuvi
      • Ardhi na Mipango Miji
      • Maendeleo ya Jamii, Ustawi wa Jamii, Jinsia na Vijana
      • Ujenzi
      • Mazingira na Udhibiti wa Taka ngumu
    • Vitengo
      • Sheria na Usalama
      • Mkaguzi wa Ndani
      • TEHAMA na Uhusiano
      • Manunuzi
      • Uchaguzi
      • Ufugaji Nyuji
    • Ward
  • Fursa za Uwekezaji
    • Maeneo ya Utalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
    • Mji wa Serikali
    • Kwa nini uwekeze Dodoma?
  • Huduma Zetu
    • Maendeleo ya jamii
    • Elimu
    • Miundombinu
    • Mazingira
    • Afya
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Fedha na Utawala
      • Mipango miji na Mazingira
      • Uchumi, Afya na Elimu
      • Kudhitibi UKIMWI
      • Maadili
    • Kamati zingine/Bodi/Uwakilishi
    • Ratiba
      • Vikao vya Madiwani
      • Kuonana na Mstahiki Meya
  • Miradi
    • Miradi itakayotekelezwa
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Ripoti
    • Sheria Ndogo
    • Miongozo
    • Mpango Mkakati
    • Fomu
    • Jifunze Nyumbani
    • Mpango Kabambe
    • Jarida
    • Asemavyo Mahia - Afya na Mazingira
  • Kituo cha habari
    • Taarifa kwa vyombo vya habari
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya picha
    • Habari
    • Matukio
  • City TV

Serikali ya awamu ya sita imetengeneza mazingira mazuri ya uwekezaji

Imewekwa tarehe: April 1st, 2024

Na. Dennis Gondwe, DODOMA

SERIKALI ya awamu ya sita inayoongozwa na Rais, Dkt. Samia Suluhu Hassan imetengeneza mazingira mazuri ya uwekezaji na kuwavutia wenye viwanda kuwekeza Halmashauri ya Jiji la Dodoma na kukuza uchumi.

Kauli hiyo ilitolewa na Kaimu Mkuu wa Divisheni ya Uwekezaji, Viwanda na Biashara Halmashauri ya Jiji la Dodoma, Abeid Msangi alipokuwa akiongelea mafanikio ya serikali ya awamu ya sita kwa kipindi cha miaka mitatu ya Rais, Dkt. Samia Suluhu Hassan katika ukumbi wa Halmashauri ya Jiji la Dodoma.

Msangi alisema kuwa kwa mazingira mazuri ya uwekezaji yanayofanywa na serikali ya awamu ya sita, Halmashauri ya Jiji la Dodoma itaendelea kunufaika na uchumi wake kuanza kutegemea viwanda. “Katika kwenda sambamba na ongezeko la uwekezaji katika Halmashauri ya Jiji la Dodoma, tumejitika kufuata maelekezo ya Mpango Kabamba wa Jiji la Dodoma. Mpango huo umepanga maeneo kadhaa ya uwekezaji yakiwepo ya viwanda vikubwa kule Nala. Eneo la uwekezaji wa viwanda lina zaidi ya ekari 1,500 na viwanja zaidi ya 241. Sehemu ya viwanja hivyo, imetolewa kwa ajili ya ‘Export Processing Zines Authority’ (EPZA). Pia wapo wawekezaji wengine wa kati na wakubwa” alisema Msangi.

Alisema kuwa katika eneo la viwanda Nala kimejengwa kiwanda kikubwa cha mbolea Itracom chenye uwezo wa kuzalisha tani 1,000,000 za mbolea kwa mwaka. “Kiwanda hicho ni ‘icon’ kwa sasa kinazalisha tani 400,000. Kiwanda hiki kinaifanya Tanzania kuwa mzalishaji mkubwa wa mbolea na muuzaji katika soko la Afrika Mashariki na Kati. Kiwanda hiki kimeweza kubadilisha kabisa uchumi wa Dodoma. Kitakapokamilika kabisa kinatarajiwa kutoa ajira rasmi zaidi ya 400 na wale wanaopata fursa kupitia kiwanda hicho kufikia 15,000” alisema Msangi.

Mafanikio mengine alisema kuwa halmashauri inajivunia kuanza kujengwa kiwanda kingine kikubwa kitakachokuwa kinazalisha na kuchuja mbegu za mafuta ya alizeti, ufuta na karanga. ”Kiwanda kinajengwa eneo la Veyula na kitakuwa na uwezo wa mchujo mara mbili. Kiwanda kitaweza kukamua alizeti tani 200 kwa siku na kuzalisha mafuta yenye mchujo mara mbili tani 100 kila siku. Kiwanda kikikamilika kitaweza kuajiri wafanyakazi kati ya 500-600” alisema Msangi.

Msangi alisema “ndani ya miaka mitatu tumeshuhudia mabadiliko makubwa, mfano leseni za viwanda vidogo zimebadilika zaidi ya mara mbili katika kipindi cha miaka mitatu. Tulitoa leseni 242 mwaka 2020 hadi kufikia mwisho wa mwaka 2023 tumetoa leseni za viwanda vidogo 582. Yote hii inaonesha mazingira bora yaliyojengwa na serikali ya awamu ya sita yameweza kuvutia uwekezaji katika hii sekta lakini pia kuongeza nafasi za ajira na kuongeza pato la taifa”.

Halmashauri ya Jiji la Dodoma imefanya jambo kubwa katika kutambua mchango wa machinga. Halmashauri imetambua machinga zaidi ya 3,000 na kuwajengea soko kubwa la kisasa kwa shilingi bilioni 9.5 na mazingira yao ya kufanya biashara ni mazuri na salama, aliongeza.

Matangazo

  • Tangazo na Orodha ya Walioitwa kwenye mafunzo ya Wasimamizi, Wasimamizi wasaidizi na Makarani Jimbo la Dodoma Mjini na Mtumba October 23, 2025
  • TANGAZO LA MABADILIKO YA TAREHE YA USAHILI October 03, 2025
  • TANGAZO LA MAJINA YA WASIMAMIZI JIMBO LA MTUMBA October 03, 2025
  • MAJINA YA WASIMAMIZI WA VITUO VYA KUPIGIA KURA- DODOMA MJINI October 03, 2025
  • Angalia zote

Habari za hivi punde

  • Rc Senyamule awasihi wawekezaji sekta binafsi kuwekeza Dodoma

    October 03, 2025
  • CCTV kamera mwarobaini wa wavunjifu wa sheria jiji la Dodoma

    October 02, 2025
  • Wadau wa afya wapongezwa kwa juhudi zakudhibiti vifo vya wajawazito

    October 01, 2025
  • UONGOZI WA KLABU YA MICHEZO OFISI YA MKUU WA MKOA WA DODOMA WAKUTANA NA RAS KAZUNGU

    September 29, 2025
  • Angalia zote

Video

Watendaji Kata Wilaya ya Dodoma watakiwa kusimamia maswala ya Lishe
Video zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • Historia ya Manispaa
  • Wasifu wa Manispaa
  • Kata na Madiwani
  • Mji wa Serikali
  • Orodha ya Madiwani
  • Mpango Mkakati wa Halmashauri (SP)
  • Kwanini uwekeze Dodoma?
  • Zabuni za Wakala wa Ukusanyaji Mapato
  • Zabuni ya Usafi wa Mazingira

Viunganishi Linganifu

  • Msalato Sekondari
  • Mkoa wa Dodoma
  • OR-TAMISEMI
  • Utumishi
  • Chuo Kikuu Dodoma (UDOM)
  • Bunge

World visitors tracker

world map hits counter

Idadi ya watembeleaji

free HitCounter

Ramani elekezi

Wasiliana nasi

    1 CDA Street, 40477

    Anuani ya posta: 1249, DODOMA, TANZANIA

    Simu: +255 26 232 4817

    Simu ya kiganjani:

    Baruapepe: cd@dodomacc.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya tovuti

Copyright ©2017 The City Council of Dodoma. All rights reserved.