• Wasiliana nasi |
    • Maswali na majibu |
    • Baruapepe - Watumishi |
    • eVibali |
    • Malalamiko |
Dodoma City Council
Dodoma City Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Jiji la Dodoma

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa taasisi
    • Idara
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Mipango, Takwimu na Ufuatiliaji
      • Afya
      • Fedha na Biashara
      • Elimu ya Msingi
      • Elimu ya Sekondari
      • Maji
      • Kilimo, Umwagiliaji na Ushirika
      • Mifugo na Uvuvi
      • Ardhi na Mipango Miji
      • Maendeleo ya Jamii, Ustawi wa Jamii, Jinsia na Vijana
      • Ujenzi
      • Mazingira na Udhibiti wa Taka ngumu
    • Vitengo
      • Sheria na Usalama
      • Mkaguzi wa Ndani
      • TEHAMA na Uhusiano
      • Manunuzi
      • Uchaguzi
      • Ufugaji Nyuji
    • Ward
  • Fursa za Uwekezaji
    • Maeneo ya Utalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
    • Mji wa Serikali
    • Kwa nini uwekeze Dodoma?
  • Huduma Zetu
    • Maendeleo ya jamii
    • Elimu
    • Miundombinu
    • Mazingira
    • Afya
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Fedha na Utawala
      • Mipango miji na Mazingira
      • Uchumi, Afya na Elimu
      • Kudhitibi UKIMWI
      • Maadili
    • Kamati zingine/Bodi/Uwakilishi
    • Ratiba
      • Vikao vya Madiwani
      • Kuonana na Mstahiki Meya
  • Miradi
    • Miradi itakayotekelezwa
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Ripoti
    • Sheria Ndogo
    • Miongozo
    • Mpango Mkakati
    • Fomu
    • Jifunze Nyumbani
    • Mpango Kabambe
    • Jarida
    • Asemavyo Mahia - Afya na Mazingira
  • Kituo cha habari
    • Taarifa kwa vyombo vya habari
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya picha
    • Habari
    • Matukio
  • City TV

Serikali yaagiza Halmashauri kutenga bajeti kuua Mbu

Imewekwa tarehe: April 27th, 2021

WAZIRI wa Afya, Maendeleo ya jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mhe. Dorothy Gwajima amewaagiza wakurugenzi wa Halmashauri zote nchini kuhakikisha inatenga bajeti kwa ajili ya ununuzi wa dawa ya kuua mazalia ya viluilui wa mbu waenezao Malaria ili kupunguza na kujikinga na maambukizi ya ugonjwa wa malaria nchini.

Ametoa agizo hilo wakati akihutubia wananchi ikiwa ni siku ya kilele cha maadhimisho ya siku ya Malaria Duniani yaliyofanyika kitaifa Jijini Arusha, yenye kauli mbiu ya "Ziro Malaria inaanza na mimi, Nachukua hatua kuitokomeza".

Katika maadhimisho hayo, Dkt. Gwajima amesema kuwa   dawa hizi zinatakiwa kufika kwa viongozi wa vijiji na kata ili kuhamasisha jamii umuhimu wa utuzaji wa mazingira kwa kuuwa mazalia ya mbu nchini.

Amefafanua kuwa wananchi wakihamasishwa juu ya matumizi sahihi ya dawa ya kuulia vimelea vya mbu nchini kutasaidia kupunguza ugonjwa wa malaria kuanzia ngazi ya familia na Taifa kwa ujumla.

Kwa upande wa mafanikio yaliyofikiwa yaliyofikiwa na Wizara yake Dkt. Gwajima amesema wamegawa vyandarua Katika halmashauri 50 na kuweza kuwafikia wananchi milioni 15.3 na hivyo kuwakinga watu takribani milioni 15.6 kupitia kampeni maalumu,pia wamegawa vyandarua  milioni 3.7 kupitia vituo vya kutolea huduma za afya vya Umma kwa wajawazito na Watoto chini ya mwaka mmoja wanaohudhuria kliniki. 

Kwa upande wa upuliziaji wa dawa za ukoko Kwenye ukuta ndani ya nyumba amesema jumla ya nyumba 552,643 zimepuliziwa na hivyo kutoa Kinga kwa watu milioni 2.5.

Naye Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa anayeshugulikia afya, Dkt. Grace Magembe ameziagiza Halmashauri zote nchini kuhakikisha wanatenga bajeti kwa ajili ya afua za kujikinga na maambukizi ya malaria nchini.

Amesema kuwa Halmashauri ambazo hazitatenga fedha kwa ajili ya afua mbalambali za afua hizo Serikali haitasita kuzirejesha bajeti hizo mpaka pale watakapotenga fedha hizo.

Dkt. Magembe amesema kuwa nguvu kubwa inahitajika kuwekwa katika kata ambazo bado tatizo kubwa la maumbukizi ya ugonjwa huo, hivyo ni nyema halmashauri zikahakikisha zinatenga fedha za kutosha kwa lengo la kupunguza maambukizi ya malaria nchini.

Aidha. Dkt. Magembe amesema kuwa Halmashauri zimeendelea kutekeleza Sheria ya afya ya Jamii ya mwaka 2009 hususani kipengele kinachohusu usimamizi , udhibiti na usafi wa mazingira  ili kuzuia mbu na wadudu wanobeba  vimelea vya magonjwa kuzaliana.

Dkt Magembe amesema kuwa bado kuna halmashauri chache ambazo bado ugonjwa wa malaria ni tatizo, hivyo Serikali itahakikisha inaweka nguvu katika kuhakikisha wanasimamia ili kupunguza maambukizi ya malaria.

Ameendelea kusema kuwa Halmashauri zetu zimekuwamstari wa mbele katika kutunga sheria na kuzisimamia usafi wa mazingira, kaya, kata, masoko, ofisi za umma katika maeneo ya bishara haya yote yamelenga katika kuhakikisha wanatokomeza maambukizi ya Malaria. 

Kwa upande mwingine, amewataka wananchi kuhakikisha wanatumia vituo vya afya kwa ajili ya kupima afya zao, kwa kuwa serikali imewekeza fedha nyingi katika kuhakikisha wanajenga miundombinu.

Matangazo

  • MKUTANO WA BARAZA LA WAHESHIMIWA MADIWANI January 30, 2025
  • KITUO CHA AFYA ILAZO KIMEANZA KUTOA HUDUMA January 13, 2025
  • HOSPITALI YA JIJI LA DODOMA IMEANZA KUTOA HUDUMA ZA AFYA January 12, 2025
  • TANGAZO LA UUZWAJI WA VIWANJA KIKOMBO December 03, 2024
  • Angalia zote

Habari za hivi punde

  • Barabara ya Lami ya Kilometa 6 yawanufaisha wakazi wa Kata ya Miyuji

    April 23, 2025
  • Huduma ya Chakula na Lishe yapandisha ufaulu Shule ya Sekondari Nala

    April 22, 2025
  • Mradi wa Maji Nala wa Bil. 1.3, mkombozi kwa wananchi

    April 22, 2025
  • Milioni 500 kukamilisha mradi wa Kituo cha Afya Kizota

    April 22, 2025
  • Angalia zote

Video

Watendaji Kata Wilaya ya Dodoma watakiwa kusimamia maswala ya Lishe
Video zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • Historia ya Manispaa
  • Wasifu wa Manispaa
  • Kata na Madiwani
  • Mji wa Serikali
  • Orodha ya Madiwani
  • Mpango Mkakati wa Halmashauri (SP)
  • Kwanini uwekeze Dodoma?
  • Zabuni za Wakala wa Ukusanyaji Mapato
  • Zabuni ya Usafi wa Mazingira

Viunganishi Linganifu

  • Msalato Sekondari
  • Mkoa wa Dodoma
  • OR-TAMISEMI
  • Utumishi
  • Chuo Kikuu Dodoma (UDOM)
  • Bunge

World visitors tracker

world map hits counter

Idadi ya watembeleaji

free HitCounter

Ramani elekezi

Wasiliana nasi

    1 CDA Street, 40477

    Anuani ya posta: 1249, DODOMA, TANZANIA

    Simu: +255 26 232 4817

    Simu ya kiganjani:

    Baruapepe: cd@dodomacc.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya tovuti

Copyright ©2017 The City Council of Dodoma. All rights reserved.