Mganga Mkuu wa Serikali Prof. Abeid Makubi ameuagiza uongozi wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Dodoma kuboresha huduma za tiba kwa wananchi wanofika kupat ahudma za afya katika Hospitali hiyo.
Prof. Makubi ametoa maagizo hayo kufuatia ziara ya kushtukiza aliyoifanya kwenye Hospitali hiyo na kushuhudia changamoto mbalimbali ikiwemo baadhi wagonjwa kuchelewa kupewa huduma, Madaktari bingwa kutowaona wagonjwa kwa wakati na huduma za vipimo kuchelewa.
"Yapo mazuri tumeona mnayofanya kwa wananchi na tuwapongeza, ila lazima kuangalia upande wa pili ambao wananchi wanayataka, kwa yale mapungufu tuliyoyaona tungependa kuona yanaboreshwa haraka ili hosptiali hii iwe ya mfamo kwa hospitali zote za rufaa za mikoa kwa kutoa huduma zilizo bora".
Prof. Makubi amesema hospitali hiyo inatakiwa kuonesha mfano kuanzia utoaji wa huduma bora kwa mteja pamoja na kupunguza muda wa wagonjwa kusubiri huduma, upatikanajii wa wauguzi na mabingwa wanapohitajika na usafi wa wodi kwani ndiyo chachu ya wananchi wengi kufika hapo na kupata huduma kabla hawajepewa rufaa ya kwenda Hospitali kubwa kama Benjamin Mkapa.
Aidha, Mganga Mkuu huyo ameutaka uongozi na watumishi wa Hospitali hiyo kutambua majukumu yao kwa kuonesha kuwajali wananchi wote na kuwataka kuweka utaratibu usio na usumbufu kwa wangonjwa na kupatiwa huduma kwa wakati.
Prof. Makubi aliyonesha kusikitishwa alipokuta wodini baadhi ya wagonjwa wamelazwa na hawajaonwa na Mabingwa kwa zaidi ya siku tatu, wauguzi wakiwa hawajaambatana na madaktari katika kuzungukia wagonjwa huku madaktari wa vitendo (interns) wakifanya 'procedures' peke yao bila uangalizi na baadhi ya wagonjwa wengine wakiwa wamelazwa chini wakati vitanda viko wazi pamoja na mazingira ya wodi hayakuwa ya kuridhisha na kukosekana kwa mpangilio wa vifaa (5S).
"Lazima watumishi mjitambue mko wapi kwani awamu hii ni ya kuwajali wanyonge na kufanya kazi kwa bidii ndio kanuni ya awamu hii hapa kazi tu". Alisisitiza Prof. Makubi.
Prof. Makubi ameelekeza madaktari wa hospitali hiyo kufanya kazi kwa ushirikiano na wauguzi katika kuwahudumia wagonjwa
Mganga Mkuu wa Serikari Prof. Abeid Makubi akikagua shughuli za uendeshaji wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Dodoma alipofanya ziara ya kushtukiza, ambapo alipongeza pamoja na kuagiza kufanyika kwa maboresho ya utoaji wa viwango vya huduma kwa wananchi.
Chanzo: ukurasa rasmi wa wizara_afyatz (Instagram)
1 CDA Street, 40477
Anuani ya posta: 1249, DODOMA, TANZANIA
Simu: +255 26 232 4817
Simu ya kiganjani:
Baruapepe: cd@dodomacc.go.tz
Copyright ©2017 The City Council of Dodoma. All rights reserved.