• Wasiliana nasi |
    • Maswali na majibu |
    • Baruapepe - Watumishi |
    • eVibali |
    • Malalamiko |
Dodoma City Council
Dodoma City Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Jiji la Dodoma

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa taasisi
    • Idara
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Mipango, Takwimu na Ufuatiliaji
      • Afya
      • Fedha na Biashara
      • Elimu ya Msingi
      • Elimu ya Sekondari
      • Maji
      • Kilimo, Umwagiliaji na Ushirika
      • Mifugo na Uvuvi
      • Ardhi na Mipango Miji
      • Maendeleo ya Jamii, Ustawi wa Jamii, Jinsia na Vijana
      • Ujenzi
      • Mazingira na Udhibiti wa Taka ngumu
    • Vitengo
      • Sheria na Usalama
      • Mkaguzi wa Ndani
      • TEHAMA na Uhusiano
      • Manunuzi
      • Uchaguzi
      • Ufugaji Nyuji
    • Ward
  • Fursa za Uwekezaji
    • Maeneo ya Utalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
    • Mji wa Serikali
    • Kwa nini uwekeze Dodoma?
  • Huduma Zetu
    • Maendeleo ya jamii
    • Elimu
    • Miundombinu
    • Mazingira
    • Afya
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Fedha na Utawala
      • Mipango miji na Mazingira
      • Uchumi, Afya na Elimu
      • Kudhitibi UKIMWI
      • Maadili
    • Kamati zingine/Bodi/Uwakilishi
    • Ratiba
      • Vikao vya Madiwani
      • Kuonana na Mstahiki Meya
  • Miradi
    • Miradi itakayotekelezwa
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Ripoti
    • Sheria Ndogo
    • Miongozo
    • Mpango Mkakati
    • Fomu
    • Jifunze Nyumbani
    • Mpango Kabambe
    • Jarida
    • Asemavyo Mahia - Afya na Mazingira
  • Kituo cha habari
    • Taarifa kwa vyombo vya habari
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya picha
    • Habari
    • Matukio
  • City TV

Serikali yaagiza watumishi waliotia nia warudi kazini

Imewekwa tarehe: September 1st, 2020

SERIKALI imeagiza watumishi wote wa umma waliotia nia kwenye vyama vya siasa na hawakuteuliwa kugombea, warudishwe kazini katika nafasi na vyeo vyao kuanzia leo na walipwe mshahara wa kuanzia mwezi huu.

Aidha, watumishi wa umma wameonywa kutokuwa sehemu au chanzo cha vurugu wakati huu wa kampeni na uchaguzi.

Naibu Katibu Mkuu katika Ofisi ya Rais Menejimineti ya Utumishi wa Umma, Dkt. Francis Michael aliyasema hayo wakati wa kufungua kikao kazi cha siku mbili cha Wizara ya Maji na watendaji wakuu wa taasisi zilizo chini ya wizara hiyo.

Alisema Agosti 26 mwaka huu, ofisi yake ilitoa waraka unaotengua uamuzi wa awali wa kuwataka watumishi wa umma waliokwenda kutia nia ya kugombea nafasi mbalimbali wakiwa wameomba ruhusa au wamekwenda kimyakimya, kuchukua likizo bila malipo.

"Watumishi wa umma wote sasa wanatakiwa kuripoti kazini na kurejea katika nafasi zao na vyeo vyao haraka sana kuanzia Septemba 1 mwaka huu," alisema Dkt. Michael na kuongeza:

"Kuna taarifa zilizokuwa zimezagaa kwenye mitandao ya kijamii kuwa watumishi wa umma waliokwenda kutia nia hawatarudishwa kazini. Taarifa hizi sio sahihi, wale wote ambao hawakuteuliwa wanapaswa kurejea kazini kwani mtumishi wa umma kuwa mfuasi wa chama cha siasa au kushiriki siasa na kupiga kura ni haki yake" alisema.

Vyama vya siasa vimekamilisha taratibu za kuwachagua watakaopeperusha bendera zao (za vyama) katika nafasi ya urais, wabunge na udiwani kwa ajili ya Uchaguzi Mkuu uliopangwa kufanyika Oktoba 28 mwaka huu.

Dkt. Michael alisema kwa mujibu wa Kanuni za Utumishi wa Umma na Kanuni za Uchaguzi, watumishi wa umma ambao hawataendelea na nafasi zao kwenye utumishi ni wale ambao wameteuliwa na vyama vyao kugombea.

Pia Dkt. Michael alimuagiza Katibu Mkuu Wizara ya Maji na wakurugeni watendaji katika wizara hiyo, kuwaandikia barua haraka za kuwarejesha watumishi wa umma ambao walikuwa likizo bila malipo kwa sababu ya kushiriki shughuli za siasa.

Alisema ingawa mtumishi wa umma ana haki ya kuwa mwanachama wa chama chochote cha siasa na kushiriki shughuli za siasa kwenye vyama vyao, lakini ushiriki kwao usioneshe upendeleo katika utumishi wao.

Hata hivyo alisema watumishi wa umma wanapaswa kuzingatia masharti ya ushiriki wao katika masuala ya siasa, ambayo ni kutotoa siri za serikali na kutotumia rasilimali za umma.

Alisema wasaidizi wa viongozi wakiwemo mawaziri, hawaruhusiwi kushiriki na kufanya kazi zao endapo mkuu wake wa kazi atakuwa amegombea, na endapo atataka kushiriki, itabidi achukue likizo ya bila malipo na akitaka kurejea ataandika barua ya kurejea.

"Kushiriki kwa wasaidizi hao, au magari ya serikali kunaweza kumsababishia mgombea kuvuliwa ubunge endapo itabainika ushindi wake umechangiwa au kutokana na jitihada hizo na gari la serikali kutumika kwenye kampeni" alisema.

Dkt. Michael alisisitiza umuhimu wa watumishi wa umma kuwa waadilifu kwa mujibu wa Kanuni za Utendaji Kazi kwa Watumishi wa Umma kwa mwaka 2005, ikiwemo ya kuwa na matumizi sahihi ya madaraka, matumizi mazuri ya fedha na rasilimali za umma, matumizi ya dawa za kulevya na ulevi wa kupindukia, kutopokea rushwa na kutotumia kwa mambo binafsi wakati wa muda wa mwajiri.

Naibu Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Evaristo Longopa alisema watumishi wa umma wana haki ya kuwa wanachama wa kikundi au chama cha siasa, isipokuwa kwa watumishi wa vyombo vya ulinzi na usalama, Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru), watumishi wa Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa na wale wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC).

Alisema watumishi wa umma wanakatazwa kutamka au kutoa matamko yanayoidhalilisha serikali kwenye kampeni na kutumia rasilimali za umma yakiwemo magari. Alisema mtumishi atakayebainika kufanya hivyo, atachukuliwa hatua za kinidhamu ikiwa ni pamoja na kufukuzwa kazi.

"Ukumbuke kwa kufanya hivyo, mtumishi utaingia matatani ikiwamo kufukuzwa kazi na pia hata huyo uliyemsaidia akishinda ushindi wake unaweza kutenguliwa" alisema.


Chanzo: HabariLeo

Matangazo

  • MKUTANO WA BARAZA LA WAHESHIMIWA MADIWANI January 30, 2025
  • KITUO CHA AFYA ILAZO KIMEANZA KUTOA HUDUMA January 13, 2025
  • HOSPITALI YA JIJI LA DODOMA IMEANZA KUTOA HUDUMA ZA AFYA January 12, 2025
  • TANGAZO LA UUZWAJI WA VIWANJA KIKOMBO December 03, 2024
  • Angalia zote

Habari za hivi punde

  • Barabara ya Lami ya Kilometa 6 yawanufaisha wakazi wa Kata ya Miyuji

    April 23, 2025
  • Huduma ya Chakula na Lishe yapandisha ufaulu Shule ya Sekondari Nala

    April 22, 2025
  • Mradi wa Maji Nala wa Bil. 1.3, mkombozi kwa wananchi

    April 22, 2025
  • Milioni 500 kukamilisha mradi wa Kituo cha Afya Kizota

    April 22, 2025
  • Angalia zote

Video

Watendaji Kata Wilaya ya Dodoma watakiwa kusimamia maswala ya Lishe
Video zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • Historia ya Manispaa
  • Wasifu wa Manispaa
  • Kata na Madiwani
  • Mji wa Serikali
  • Orodha ya Madiwani
  • Mpango Mkakati wa Halmashauri (SP)
  • Kwanini uwekeze Dodoma?
  • Zabuni za Wakala wa Ukusanyaji Mapato
  • Zabuni ya Usafi wa Mazingira

Viunganishi Linganifu

  • Msalato Sekondari
  • Mkoa wa Dodoma
  • OR-TAMISEMI
  • Utumishi
  • Chuo Kikuu Dodoma (UDOM)
  • Bunge

World visitors tracker

world map hits counter

Idadi ya watembeleaji

free HitCounter

Ramani elekezi

Wasiliana nasi

    1 CDA Street, 40477

    Anuani ya posta: 1249, DODOMA, TANZANIA

    Simu: +255 26 232 4817

    Simu ya kiganjani:

    Baruapepe: cd@dodomacc.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya tovuti

Copyright ©2017 The City Council of Dodoma. All rights reserved.