• Wasiliana nasi |
    • Maswali na majibu |
    • Baruapepe - Watumishi |
    • eVibali |
    • Malalamiko |
Dodoma City Council
Dodoma City Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Jiji la Dodoma

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa taasisi
    • Idara
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Mipango, Takwimu na Ufuatiliaji
      • Afya
      • Fedha na Biashara
      • Elimu ya Msingi
      • Elimu ya Sekondari
      • Maji
      • Kilimo, Umwagiliaji na Ushirika
      • Mifugo na Uvuvi
      • Ardhi na Mipango Miji
      • Maendeleo ya Jamii, Ustawi wa Jamii, Jinsia na Vijana
      • Ujenzi
      • Mazingira na Udhibiti wa Taka ngumu
    • Vitengo
      • Sheria na Usalama
      • Mkaguzi wa Ndani
      • TEHAMA na Uhusiano
      • Manunuzi
      • Uchaguzi
      • Ufugaji Nyuji
    • Ward
  • Fursa za Uwekezaji
    • Maeneo ya Utalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
    • Mji wa Serikali
    • Kwa nini uwekeze Dodoma?
  • Huduma Zetu
    • Maendeleo ya jamii
    • Elimu
    • Miundombinu
    • Mazingira
    • Afya
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Fedha na Utawala
      • Mipango miji na Mazingira
      • Uchumi, Afya na Elimu
      • Kudhitibi UKIMWI
      • Maadili
    • Kamati zingine/Bodi/Uwakilishi
    • Ratiba
      • Vikao vya Madiwani
      • Kuonana na Mstahiki Meya
  • Miradi
    • Miradi itakayotekelezwa
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Ripoti
    • Sheria Ndogo
    • Miongozo
    • Mpango Mkakati
    • Fomu
    • Jifunze Nyumbani
    • Mpango Kabambe
    • Jarida
    • Asemavyo Mahia - Afya na Mazingira
  • Kituo cha habari
    • Taarifa kwa vyombo vya habari
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya picha
    • Habari
    • Matukio
  • City TV

Serikali yabakisha vijiji 40 vilivyokuwa maeneo ya hifadhi Dodoma

Imewekwa tarehe: October 6th, 2021

Na Munir Shemweta, WANMM CHEMBA

SERIKALI imevibakisha vijiji 40 kati ya 42 ambavyo wananchi wake walikuwa wakiishi na kuendesha shughuli zao kwenye maeneo ya hifadhi na mapori ya akiba katika mkoa wa Dodoma.

Hatua hiyo inalenga kuwawezesha wananchi wa vijiji hivyo kuendelea na shughuli zao baaada ya kuwepo mgogoro wa matumizi ya ardhi uliosababisha kuundwa kwa Timu ya wataalamu iliyoongozwa na Mawaziri nane kutafuta ufumbuzi wa mgogoro huo.

Akizungumza na wananchi wa vijiji vya Bubutole na Mwombose vilivyo katika wilaya ya Chemba mkoani Dodoma tarehe 5 Oktoba 2021 katika ziara ya Mawaziri nane kutoa mrejesho wa ufumbuzi wa migogoro ya ardhi katika maeneo ya hifadhi na mapori ya akiba, Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi, William Lukuvi alisema uamuzi huo unafuatia Serikali kuamua kufuta mapori 12 yenye ukubwa wa ekari 707,659 na ekari 46,755 za misitu 12 kwa ajili ya kuwamegea wananchi sehemu ya maeneo hayo ili kuendesha shughuli za uzalishaji mali ikiwemo kilimo na ufugaji.

“Maelekezo ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan ni kuondoa shaka na taharuki kwa wananchi wanaoishi kwenye vijiji husika” alisema Lukuvi. 

Waziri Lukuvi alisema, tayari GN za Misitu na Mapori ya akiba vilivyokuwemo vijiji hivyo imefutwa na  sasa taasisi zenye dhamana na maeneo ya hifadhi zinatakiwa kulinda na kuweka alama za mipaka kwenye maeneo yaliyobaki kwa lengo la kuepusha kuvamiwa na wananchi.

Lukuvi ambaye ni kiongozi wa kamati ya Mawaziri nane alisema, vijiji viwili kati ya 42 katika mkoa huo wa Dodoma itabidi viondolewe kupisha ujenzi wa bwawa la maji la Farkwa katika wilaya ya Chemba na vijiji hivyo ni Bubutole na Mwombose vilivyopo katika wilaya ya Chemba.

"Serikali tayari imelipa fidia kwa wananchi katika vijiji hivi na wale ambao fidia haikwenda vizuri Serikali ipo na kila mtu lazima alipwe kulingana na mali zake na Rais wetu Mhe. Samia Suluhu Hassan ameshatoa fedha kwa ajili ya huduma za shule, zahanati pamoja na maji pale mtakapokwenda’’. Alisema Lukuvi.

Tayari wakazi 2,829 sawa na asilimia 99 kati ya 2,868 katika vijiji hivyo viwili wameshalipwa fidia.

Bwawa litakalojengwa litakuwa na ukubwa wa kilomita za mraba 68 na mm za ujazo milioni 470 na litanufaisha wakazi wa jiji la Dodoma, Chemba, Bahi na Chamwino pamoja na vijiji vyote vitakavyopitiwa na bomba hilo.

Hata hivyo, Lukuvi alisema, pamoja na Serikali kubakisha vijiji 40 katika mkoa wa Dodoma baadhi ya vitongoji navyo vitafanyiwa tathimini upya ili kuondoa kasoro zilizojitokeza awali na kusisitiza kuwa tathmini hiyo itakuwa shirikishi kwa viongozi, wataalamu na wananchi wa vitongoji husika.

“Vijiji vyote 40 katika mkoa huu wa Dodoma vitabaki ila ndani ya vijiji 20 kuna vitongoji  tutavifanyia tathmini upya na suala hili litakuwa shirikishi” alisema Lukuvi.

Mawaziri nane kutoka wizara za kisekta wameanza ziara katika katika vitongoji vilivyopo vijiji vya Handa na kuzungumza na wananchi wa kitongoji cha Mbugani katika hifadhi ya pori la Swagaswaga na kuendelea na vijiji vya Bubutole na Mwombose kwa lengo la kutoa mrejesho ikiwa ni utekelezaji agizo la Rais Samia Suluhu Hassan alilolitoa tarehe 7 Agosti 2021 kutaka kutekelezwa kwa ufumbuzi wa migogoro ya matumizi ya ardhi katika vijiji 975 bila kuleta taharuki kwa kuzingatia maslahi mapana ya taifa ambapo mrejesho huo umeanza katika vijiji 920.





Matangazo

  • MKUTANO WA BARAZA LA WAHESHIMIWA MADIWANI January 30, 2025
  • KITUO CHA AFYA ILAZO KIMEANZA KUTOA HUDUMA January 13, 2025
  • HOSPITALI YA JIJI LA DODOMA IMEANZA KUTOA HUDUMA ZA AFYA January 12, 2025
  • TANGAZO LA UUZWAJI WA VIWANJA KIKOMBO December 03, 2024
  • Angalia zote

Habari za hivi punde

  • Barabara ya Lami ya Kilometa 6 yawanufaisha wakazi wa Kata ya Miyuji

    April 23, 2025
  • Huduma ya Chakula na Lishe yapandisha ufaulu Shule ya Sekondari Nala

    April 22, 2025
  • Mradi wa Maji Nala wa Bil. 1.3, mkombozi kwa wananchi

    April 22, 2025
  • Milioni 500 kukamilisha mradi wa Kituo cha Afya Kizota

    April 22, 2025
  • Angalia zote

Video

Watendaji Kata Wilaya ya Dodoma watakiwa kusimamia maswala ya Lishe
Video zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • Historia ya Manispaa
  • Wasifu wa Manispaa
  • Kata na Madiwani
  • Mji wa Serikali
  • Orodha ya Madiwani
  • Mpango Mkakati wa Halmashauri (SP)
  • Kwanini uwekeze Dodoma?
  • Zabuni za Wakala wa Ukusanyaji Mapato
  • Zabuni ya Usafi wa Mazingira

Viunganishi Linganifu

  • Msalato Sekondari
  • Mkoa wa Dodoma
  • OR-TAMISEMI
  • Utumishi
  • Chuo Kikuu Dodoma (UDOM)
  • Bunge

World visitors tracker

world map hits counter

Idadi ya watembeleaji

free HitCounter

Ramani elekezi

Wasiliana nasi

    1 CDA Street, 40477

    Anuani ya posta: 1249, DODOMA, TANZANIA

    Simu: +255 26 232 4817

    Simu ya kiganjani:

    Baruapepe: cd@dodomacc.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya tovuti

Copyright ©2017 The City Council of Dodoma. All rights reserved.