• Wasiliana nasi |
    • Maswali na majibu |
    • Baruapepe - Watumishi |
    • eVibali |
    • Malalamiko |
Dodoma City Council
Dodoma City Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Jiji la Dodoma

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa taasisi
    • Idara
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Mipango, Takwimu na Ufuatiliaji
      • Afya
      • Fedha na Biashara
      • Elimu ya Msingi
      • Elimu ya Sekondari
      • Maji
      • Kilimo, Umwagiliaji na Ushirika
      • Mifugo na Uvuvi
      • Ardhi na Mipango Miji
      • Maendeleo ya Jamii, Ustawi wa Jamii, Jinsia na Vijana
      • Ujenzi
      • Mazingira na Udhibiti wa Taka ngumu
    • Vitengo
      • Sheria na Usalama
      • Mkaguzi wa Ndani
      • TEHAMA na Uhusiano
      • Manunuzi
      • Uchaguzi
      • Ufugaji Nyuji
    • Ward
  • Fursa za Uwekezaji
    • Maeneo ya Utalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
    • Mji wa Serikali
    • Kwa nini uwekeze Dodoma?
  • Huduma Zetu
    • Maendeleo ya jamii
    • Elimu
    • Miundombinu
    • Mazingira
    • Afya
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Fedha na Utawala
      • Mipango miji na Mazingira
      • Uchumi, Afya na Elimu
      • Kudhitibi UKIMWI
      • Maadili
    • Kamati zingine/Bodi/Uwakilishi
    • Ratiba
      • Vikao vya Madiwani
      • Kuonana na Mstahiki Meya
  • Miradi
    • Miradi itakayotekelezwa
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Ripoti
    • Sheria Ndogo
    • Miongozo
    • Mpango Mkakati
    • Fomu
    • Jifunze Nyumbani
    • Mpango Kabambe
    • Jarida
    • Asemavyo Mahia - Afya na Mazingira
  • Kituo cha habari
    • Taarifa kwa vyombo vya habari
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya picha
    • Habari
    • Matukio
  • City TV

Serikali yaipa JKT Mitambo na Zana za Kilimo za Bilioni 4

Imewekwa tarehe: October 7th, 2022

Na Rhoda Simba, Dodoma.

SERIKALI imetoa mitambo na zana za kilimo zenye thamani ya takribani bilioni 4 kwa Jeshi la Kujenga Taifa ( JKT) ili kuongeza uzalishaji wa chakula hapa nchini  huku  ikilipongeza Jeshi hilo  kwa kuendelea kusimamia malengo ya kuanzishwa kwake nakutimiza  majukumu ya malezi ya vijana na uzalishaji mali ili kujenga uchumi na Taifa kwa ujumla.

Zana hizo ambazo zimetoka nchini Italia zenye uwezo wa kulima Hekari  500 kwa siku, zitaliwezesha jeshi hilo kujilisha kwa asilimia 100 ifikapo 2025 na ziada ya chakula kutumika kama biashara ndani na nje ya nchi.

 Akikabidhi zana na vifaa hivyo, Waziri wa Ulinzi  na Jeshi la Kujenga Taifa Innocent Bashungwa amesema fedha hizo ni sehemu ya bajeti ya mwaka wa fedha  katika mwaka wa fedha 2021/22 zilizotolewa na Serikali, na kuongeza tija ya uzalishaji mali hususani katika eneo la kilimo chini ya jeshi la kujenga Taifa ili kuondokana na kilimo cha mkono na kutumia Teknolojia ya kisasa.

 

“Nishukuru uongozi wa Jeshi la kujenga Taifa kwa maandalizi ya hafla hii fupi ya uzinduzi wa mitambo na zana hizi za kilimo ambazo zitatumika katika uzalishaji mali na kuongeza tija na ufanisi katika kilimo ndani ya jeshi la kujenga Taifa” amesema Bashungwa

Aidha Waziri Bashungwa amesema kuwa jitihada hizo za kutumia zana za kisasa na Teknolojia  ya kisasa chini ya jeshi la kujenga taifa ni sehemu ya mkakati wa kusaidia taifa na mpango mzima  wa kuhakikisha zinafanya jitihada za uzalishaji ili kuweza kujitosheleza kwa chakula  hapa nchini.

Kwa upande wake Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Dk Stergomena Tax amesema kuna upungufu wa utekelezaji wa miundombinu mbalimbali hususani miundombinu ya mradi wa Umwagiliaji wa Chita na Mgeta,kutokana na hilo alisema zinahitajika sh Bilioni 10 kwa ajili ya kukamilisha utekelezaji wa mradi huo.

"Kuna hitajika fedha kwa ajili ya kutekeleza miundombinu ya miradi mbalimbali ikiwemo kilimo cha umwagiliaji katika maeneo ya Mgeta na Chita,"amesema Tax.

Awali akimkaribisha Mkuu wa Majeshi Mwenyekiti wa Kilimo Mkakati Mifugo na Uvuvi Brigedia Jenerali, Hassan Mabena alisema wamejipanga kuhakikisha wanafanya kilimo chenye tija ili kuhakikisha Jeshi hilo linajitosheleza kwa chakula.

Kutokana na hilo amesema wanaishukuru serikali kutokana na zana hizo ambazo wanaamini watatekeleza miradi ya kilimo kwa weledi.

Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Jenerali Jacob Mkunda amesema JKT inapaswa kubuni na kuanzisha viwanda ili kuongeza kipato ndani ya Jeshi hilo.

Naye Mkuu wa JKT, Meja Jenerali Rajabu Mabele, ameishukuru serikali kutokana na kutoa fedha hizo za kununua zana za kilimo.

Hata hivyo kwa upande wake Katibu Mkuu Wizara ya Ulinzi Dk Faraji Mnyepe amesema Wizara itaendelea kutoa ushirikiano kwa Jeshi hilo ili kuhakikisha Kilimo kinasonga mbele.

 


Matangazo

  • MKUTANO WA BARAZA LA WAHESHIMIWA MADIWANI January 30, 2025
  • KITUO CHA AFYA ILAZO KIMEANZA KUTOA HUDUMA January 13, 2025
  • HOSPITALI YA JIJI LA DODOMA IMEANZA KUTOA HUDUMA ZA AFYA January 12, 2025
  • TANGAZO LA UUZWAJI WA VIWANJA KIKOMBO December 03, 2024
  • Angalia zote

Habari za hivi punde

  • Barabara ya Lami ya Kilometa 6 yawanufaisha wakazi wa Kata ya Miyuji

    April 23, 2025
  • Huduma ya Chakula na Lishe yapandisha ufaulu Shule ya Sekondari Nala

    April 22, 2025
  • Mradi wa Maji Nala wa Bil. 1.3, mkombozi kwa wananchi

    April 22, 2025
  • Milioni 500 kukamilisha mradi wa Kituo cha Afya Kizota

    April 22, 2025
  • Angalia zote

Video

Watendaji Kata Wilaya ya Dodoma watakiwa kusimamia maswala ya Lishe
Video zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • Historia ya Manispaa
  • Wasifu wa Manispaa
  • Kata na Madiwani
  • Mji wa Serikali
  • Orodha ya Madiwani
  • Mpango Mkakati wa Halmashauri (SP)
  • Kwanini uwekeze Dodoma?
  • Zabuni za Wakala wa Ukusanyaji Mapato
  • Zabuni ya Usafi wa Mazingira

Viunganishi Linganifu

  • Msalato Sekondari
  • Mkoa wa Dodoma
  • OR-TAMISEMI
  • Utumishi
  • Chuo Kikuu Dodoma (UDOM)
  • Bunge

World visitors tracker

world map hits counter

Idadi ya watembeleaji

free HitCounter

Ramani elekezi

Wasiliana nasi

    1 CDA Street, 40477

    Anuani ya posta: 1249, DODOMA, TANZANIA

    Simu: +255 26 232 4817

    Simu ya kiganjani:

    Baruapepe: cd@dodomacc.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya tovuti

Copyright ©2017 The City Council of Dodoma. All rights reserved.