• Wasiliana nasi |
    • Maswali na majibu |
    • Baruapepe - Watumishi |
    • eVibali |
    • Malalamiko |
Dodoma City Council
Dodoma City Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Jiji la Dodoma

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa taasisi
    • Idara
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Mipango, Takwimu na Ufuatiliaji
      • Afya
      • Fedha na Biashara
      • Elimu ya Msingi
      • Elimu ya Sekondari
      • Maji
      • Kilimo, Umwagiliaji na Ushirika
      • Mifugo na Uvuvi
      • Ardhi na Mipango Miji
      • Maendeleo ya Jamii, Ustawi wa Jamii, Jinsia na Vijana
      • Ujenzi
      • Mazingira na Udhibiti wa Taka ngumu
    • Vitengo
      • Sheria na Usalama
      • Mkaguzi wa Ndani
      • TEHAMA na Uhusiano
      • Manunuzi
      • Uchaguzi
      • Ufugaji Nyuji
    • Ward
  • Fursa za Uwekezaji
    • Maeneo ya Utalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
    • Mji wa Serikali
    • Kwa nini uwekeze Dodoma?
  • Huduma Zetu
    • Maendeleo ya jamii
    • Elimu
    • Miundombinu
    • Mazingira
    • Afya
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Fedha na Utawala
      • Mipango miji na Mazingira
      • Uchumi, Afya na Elimu
      • Kudhitibi UKIMWI
      • Maadili
    • Kamati zingine/Bodi/Uwakilishi
    • Ratiba
      • Vikao vya Madiwani
      • Kuonana na Mstahiki Meya
  • Miradi
    • Miradi itakayotekelezwa
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Ripoti
    • Sheria Ndogo
    • Miongozo
    • Mpango Mkakati
    • Fomu
    • Jifunze Nyumbani
    • Mpango Kabambe
    • Jarida
    • Asemavyo Mahia - Afya na Mazingira
  • Kituo cha habari
    • Taarifa kwa vyombo vya habari
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya picha
    • Habari
    • Matukio
  • City TV

Serikali yaonya ‘wanaochakachua’ maziwa

Imewekwa tarehe: December 7th, 2020

SERIKALI imewataka baadhi ya wafugaji wenye mtindo wa kuongeza unga katika Maziwa kuacha kufanya hivyo kwani sio tu inaharibu biashara ya maziwa katika soko la ndani ya nchi bali hata soko la nje.

Katibu Mkuu, Wizara ya Mifugo na Uvuvi (Mifugo), Prof. Elisante Ole Gabriel alitoa onyo hilo alipotembelea Banda la Maonesho la Bodi ya Maziwa lililopo katika Viwanja vya Maonesho ya bidhaa za Viwanda yanayoendelea kufanyika katika Viwanja vya Maonesho vya Mwl. Nyerere jijini Dar es Salaam jana Disemba 6, 2020.

Prof. Gabriel alisema wanaofanya hivyo wanapaswa kutambua kuwa kitendo hicho ni kibaya, wanajidanganya wao wenyewe na wasipo jirekebisha wataishia pabaya.

“Bodi endeleeni kutafuna wale wote ambao wanachakachua maziwa kadri iwezekanavyo na sheria ichukue mkondo wake na hatutakuwa na huruma na yeyote kwa sababu wanaharibu taswira nzima ya biashara ya maziwa ndani na nje ya nchi,” alisema Prof. Gabriel.

Aliongeza kwa kusema kuwa Wafugaji wajue kwamba Serikali ina vipimo ambavyo vinaweza kutambua maziwa yaliyowekwa unga na hivyo aliwataka wale wote wanaojihusisha na uhalifu huo kuacha kufanya hivyo kwani watakaokutwa sheria itachukua mkondo wake.

Aidha, Prof. Gabriel aliitaka Bodi ya Maziwa kuhakikisha unywaji wa maziwa unaongezeka na wawahamasishe Watanzania kadri iwezekanavyo walau ndani ya miaka mitano ijayo wazidi walau lita zaidi ya 100 kwa mwaka kwani kwa sasa unywaji upo kwenye lita 54 jambo ambalo ni aibu kwa nchi yenye ng’ombe milioni 33. 4 na inazalisha lita za maziwa bilioni 3.01 huku kukiwa na viwanda vya kuchakata maziwa 99.

“Bodi fanyeni kazi ya ziada, msifanye kazi kwa mazoea, wekeni sayansi kwenye kazi yenu na pia pimeni elimu mliyoitoa imeeleweka kiasi gani ili wale wanaofanya vizuri muwapongeze na wale wanaokosea muwaadhibu kwa mujibu wa sheria na taratibu ili kuifanya tasnia iwe bora zaidi,” aliongeza Prof. Gabriel

Aliongeza kuwa anaamini tasnia hiyo ya maziwa itaendelea kusimamiwa vizuri sana na itachangia vizuri katika uchumi wa kati ambao Dkt. John Pombe Magufuli ameshafanya kazi ya ziada kuipeleka nchi katika uchumi wa kati miaka mitano kabla, hivyo anaamini nchi itaendelea kupanda kiuchumi na zao la maziwa ni muhimu likaendelea kuimarishwa ili litoe mchango unaohitajika katika kukuza pato la taifa.

“Bodi ya Maziwa hakikisheni ubora wa maziwa unakuwepo na yapatikane kwa wingi kwa ajili ya kujenga afya bora kwa watumiaji,” alifafanua Prof. Gabriel

Naye, Mkuu wa Wilaya ya Temeke, Godwin Gondwe alisema katika Wilaya ya Temeke na Mkoa wa Dar es Salaam watahakikisha wanaendelea kuhamasisha unywaji wa maziwa kupitia michezo mbalimbali na wamejipanga hivi karibuni wanatarajia kufanya tamasha kubwa ambalo litatumika kuchagiza pia unywaji wa maziwa nchini.

Kaimu Msajili wa Bodi ya Maziwa, Noely Byamungu alisema kuwa wamejipanga kuhakikisha wanajenga utamaduni kwa jamii kupenda kunywa maziwa na wameanza na kundi la wanamichezo lakini kuna mpango mkakati wa kitaifa wa kuwafikia Watoto mashuleni.

“Mpango wa kitaifa unalenga kukuza utamaduni wa unywaji wa maziwa kwa Watoto wadogo na kwa kufanya hivyo kutasaidia kujenga jamii inayopenda kunywa maziwa, hivyo tunawaomba Waandishi wa Habari mtusaidia kuelimisha jamii kuhusu umuhimu wa unywaji wa maziwa ili tuwe na jamii inayopenda kunywa maziwa kwa afya,” alisema Byamungu

Aliongeza kwa kusema kuwa katika kutekeleza mpango huo Bodi itashirikisha wadau tofautitofauti ikiwemo Wizara ya TAMISEMI, Wizara ya Afya na Wizara ya Elimu na Wizara ya Mifugo na Uvuvi ili kuhakikisha unywaji wa maziwa unaongozeka lakini pia wafugaji wazalishe na waweze kupata masoko ya uhakika.

Picha za matukio mbalimbali:



Matangazo

  • MKUTANO WA BARAZA LA WAHESHIMIWA MADIWANI January 30, 2025
  • KITUO CHA AFYA ILAZO KIMEANZA KUTOA HUDUMA January 13, 2025
  • HOSPITALI YA JIJI LA DODOMA IMEANZA KUTOA HUDUMA ZA AFYA January 12, 2025
  • TANGAZO LA UUZWAJI WA VIWANJA KIKOMBO December 03, 2024
  • Angalia zote

Habari za hivi punde

  • Barabara ya Lami ya Kilometa 6 yawanufaisha wakazi wa Kata ya Miyuji

    April 23, 2025
  • Huduma ya Chakula na Lishe yapandisha ufaulu Shule ya Sekondari Nala

    April 22, 2025
  • Mradi wa Maji Nala wa Bil. 1.3, mkombozi kwa wananchi

    April 22, 2025
  • Milioni 500 kukamilisha mradi wa Kituo cha Afya Kizota

    April 22, 2025
  • Angalia zote

Video

Watendaji Kata Wilaya ya Dodoma watakiwa kusimamia maswala ya Lishe
Video zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • Historia ya Manispaa
  • Wasifu wa Manispaa
  • Kata na Madiwani
  • Mji wa Serikali
  • Orodha ya Madiwani
  • Mpango Mkakati wa Halmashauri (SP)
  • Kwanini uwekeze Dodoma?
  • Zabuni za Wakala wa Ukusanyaji Mapato
  • Zabuni ya Usafi wa Mazingira

Viunganishi Linganifu

  • Msalato Sekondari
  • Mkoa wa Dodoma
  • OR-TAMISEMI
  • Utumishi
  • Chuo Kikuu Dodoma (UDOM)
  • Bunge

World visitors tracker

world map hits counter

Idadi ya watembeleaji

free HitCounter

Ramani elekezi

Wasiliana nasi

    1 CDA Street, 40477

    Anuani ya posta: 1249, DODOMA, TANZANIA

    Simu: +255 26 232 4817

    Simu ya kiganjani:

    Baruapepe: cd@dodomacc.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya tovuti

Copyright ©2017 The City Council of Dodoma. All rights reserved.