Katika utekelezaji wa Agizo la Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli, Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto (Afya) kupitia kibali cha Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Manajimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora chenye Kumb. Na. FA.97/128/01/"A"/51 cha tarehe 16 Machi, 2020; imetangaza nafasi elfu moja (1,000) za Ajira Mpya za Kada ya Madaktari Daraja la II kwa mchanganuo ufuatao:
1. Ofisi ya Rais TAMISEMI (Hospitali za Wilaya) nafasi 610
2. Wizara ya Afya (Hospitali za Rufaa na Mikoa) nafasi 306
3. Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) nafasi 40
4. Hospitali ya Benjamin Mkapa (BMH) nafasi 20
5. Taasisi ya Mifumo Muhimbili (MOI) nafasi 10
6. Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI) nafasi 7 na
7. Taasisi ya Saratani ya Ocean Road (ORCI) nafasi 7
Kusoma tangazo bofya hapa: TANGAZO LA NAFASI ZA AJIRA MPYA ZA MADAKTARI 1,000
1 CDA Street, 40477
Anuani ya posta: 1249, DODOMA, TANZANIA
Simu: +255 26 232 4817
Simu ya kiganjani:
Baruapepe: cd@dodomacc.go.tz
Copyright ©2017 The City Council of Dodoma. All rights reserved.