NAIBU Waziri wa Afya Dkt. Godwin Mollel amesema, Serikali imetenga shilingi Bilioni 10.7 kwa ajili ya kutekeleza Mpango Mkakati wa Tatu wa Kitaifa wa Kuzuia na Kudhibiti Magonjwa Yasiyoambukiza.
Dkt. Mollel amesema hayo, wakati akijibu swali la Mbunge wa Jimbo la Mtoni Mhe. Idrissa Juma Abdul - Hafar katika kikao cha pili cha Bunge la 9, Jijini Dodoma.
Amesema, Mpango mkakati huo, umeainisha mikakati mahsusi ya udhibiti wa visababishi vya magonjwa yasiyoambukiza ikiwemo, Kuimarisha uratibu na ushirikishwaji wa sekta mtambuka, kuimarisha miundombinu ya utoaji wa huduma.
Aliendelea kusema kuwa, mipango mingine ni pamoja na kuimarisha uwezo watumishi katika kukabiliana na magonjwa yasiyoambukiza, kuimarisha na kusimamia shughuli za utafiti pamoja na kuhamasisha wananchi kuhusu njia za kujikinga na magonjwa yasiyoambukiza, pamoja na kujenga tabia ya kufanya mazoezi.
Aidha, Dkt. Mollel amesema kuwa, Serikali inaendelea kuhamasisha wananchi kujiunga na Bima ya afya kwa wote pindi Sheria hiyo itakapopitishwa na Bunge ili kupunguza gharama za matibabu kwa wananchi, hasa matibabu ya magonjwa yasiyoambukiza.
Sambamba na hilo, Dkt. Mollel amesema Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan asmetenga kiasi cha Shilingi Bilioni 149.77 kwaajili ya kuwapatia Bima wananchi wasio na uwezo.
|||
O
1 CDA Street, 40477
Anuani ya posta: 1249, DODOMA, TANZANIA
Simu: +255 26 232 4817
Simu ya kiganjani:
Baruapepe: cd@dodomacc.go.tz
Copyright ©2017 The City Council of Dodoma. All rights reserved.