WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amesema Serikali imeshatoa shilingi Bilioni 15 kwa Wakala wa Taifa wa Hifadhi ya Chakula (NFRA) ili kununua mahindi kutoka kwa wakulima.
“Uzalishaji wa mahindi ni mkubwa lakini na sisi pia tumeimarisha hifadhi yetu ya Taifa ya chakula. NFRA tumeipa fedha za kwenda kununua mahindi kwa bei ya kumwezesha mkulima ili ajikimu hadi msimu ujao. Uwezo si mkubwa sana, lakini tumeipa shilingi Bilioni 15,” amesema.
Ametoa kauli hiyo leo (Alhamisi, Septemba 2, 2021) Bungeni jijini Dodoma wakati akijibu swali la Mbunge wa Kwela, Mheshimiwa Deus Clement Sangu kwenye kipindi cha maswali ya papo kwa papo kwa Waziri Mkuu.
Mbunge wa Kwela, Mheshimiwa Deus Clement Sangu alipokuwa akiuliza swali kwenye kipindi cha maswali ya papo kwa papo kwa Waziri Mkuu.
Chanzo: msemajimkuuwaserikali (instagram)
1 CDA Street, 40477
Anuani ya posta: 1249, DODOMA, TANZANIA
Simu: +255 26 232 4817
Simu ya kiganjani:
Baruapepe: cd@dodomacc.go.tz
Copyright ©2017 The City Council of Dodoma. All rights reserved.