WIZARA ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi maalum imepokea gari aina ya Toyota Land cruiser 'hard top' kutoka shirika la PACT Tanzania.
Kamishna wa Ustawi wa Jamii Dkt. Nandera Mhando akikabidhi gari hilo kwa Kaimu Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Patrick Golwike jijini Dodoma, amesema litahudumia makazi ya wazee Mwanzage na Msufini mkoani Tanga.
Dkt. Nandera amesema kwa sasa uhitaji wa magari bado ni mkubwa katika makazi ya wazee ambapo magari 20 yanahitajika, hivyo ujio wa gari hilo ni moja ya jitihada za kupunguza uhaba huo na kwamba jitihada zinaendelea kwa kushirikiana na wadau.
Akizungumza baada ya kupokea gari hilo, Kaimu Katibu Mkuu Bw. Patrick Golwike amelishukuru shirika la PACT kwa kuona hali ya uhitaji na kujitoa.
"Kama mnavyofahamu tunafanya kazi na Wadau, kwetu sisi kupokea Gari hili ni fahari kuona wadau wapo karibu na Serikali, PACT wameonesha mfano hivyo ni rai yetu kwa wadau wengine kujitokeza kuunga mkono jitihada za kuwahudumia Watanzania kwa hali mali".
1 CDA Street, 40477
Anuani ya posta: 1249, DODOMA, TANZANIA
Simu: +255 26 232 4817
Simu ya kiganjani:
Baruapepe: cd@dodomacc.go.tz
Copyright ©2017 The City Council of Dodoma. All rights reserved.