NAIBU WAZIRI Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Deo Ndejembi amesema Serikali imedhamiria kuboresha miundombinu ya michezo katika shule teule 56 nchini ikiwa ni wastani wa shule mbili kwa kila Mkoa.
Alieleza hayo Bungeni Dodoma wakati alijibu Swali la Anastazia Wambura, Mbunge wa Viti Maalum, aliyetaka kujua Je, lini Shule ya Sekondari Mkalapa itatambuliwa kuwa Shule ya vipaji vya michezo ya mpira wa wavu.
Ndejembi alisema Serikali inapokea ombi la Mheshimiwa Mbunge la kuitambua shule ya Sekondari Mkalapa kuwa shule ya vipaji vya mchezo wa wavu.Aidha, aliwaelekeza wataalamu wa Ofisi ya Rais TAMISEMI kutembelea shule hiyo ili kuona miundombinu iliyopo na namna shughuli za michezo zinazofanyika shuleni hapo ili kuona kama inakidhi vigezo vinavyotakiwa.
Ndejembi alisema Serikali kupitia ajira mpya zilitangazwa itahakikisha inatoa fursa kwa Waalimu wa Michezo, Kilimo na walimu wa ufundi ili kuboresha utoaji wa elimu nchini.
1 CDA Street, 40477
Anuani ya posta: 1249, DODOMA, TANZANIA
Simu: +255 26 232 4817
Simu ya kiganjani:
Baruapepe: cd@dodomacc.go.tz
Copyright ©2017 The City Council of Dodoma. All rights reserved.