Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Job Ndugai amekagua ukarabati wa jengo la Bunge leo Oktoba 1, 2020 jijini Dodoma. Katika ukaguzi huo Spika aliambatana na Katibu wa Bunge, Stephen Kagaigai, wakurugenzi na maafisa wa Ofisi ya Bunge pamoja na wahandisi wanaofanya ukarabati huo.
Spika wa Bunge Mhe. Job Ndugai akimsikiliza Katibu wa Bunge, Stephen Kagaigai akielezea kuhusu ukarabati wa jengo la Bunge unaoendelea jijini Dodoma.
Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Job Ndugai (wa pili kushoto mstari wa mbele), Katibu wa Bunge Stephen Kagaigai (mwenye tai) na viongozi wengine wakimsikiliza Mhandisi wa ukarabati akielezea maendeleo ya kazi ya ukarabati wa jengo la Bunge.
1 CDA Street, 40477
Anuani ya posta: 1249, DODOMA, TANZANIA
Simu: +255 26 232 4817
Simu ya kiganjani:
Baruapepe: cd@dodomacc.go.tz
Copyright ©2017 The City Council of Dodoma. All rights reserved.