• Wasiliana nasi |
    • Maswali na majibu |
    • Baruapepe - Watumishi |
    • eVibali |
    • Malalamiko |
Dodoma City Council
Dodoma City Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Jiji la Dodoma

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa taasisi
    • Idara
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Mipango, Takwimu na Ufuatiliaji
      • Afya
      • Fedha na Biashara
      • Elimu ya Msingi
      • Elimu ya Sekondari
      • Maji
      • Kilimo, Umwagiliaji na Ushirika
      • Mifugo na Uvuvi
      • Ardhi na Mipango Miji
      • Maendeleo ya Jamii, Ustawi wa Jamii, Jinsia na Vijana
      • Ujenzi
      • Mazingira na Udhibiti wa Taka ngumu
    • Vitengo
      • Sheria na Usalama
      • Mkaguzi wa Ndani
      • TEHAMA na Uhusiano
      • Manunuzi
      • Uchaguzi
      • Ufugaji Nyuji
    • Ward
  • Fursa za Uwekezaji
    • Maeneo ya Utalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
    • Mji wa Serikali
    • Kwa nini uwekeze Dodoma?
  • Huduma Zetu
    • Maendeleo ya jamii
    • Elimu
    • Miundombinu
    • Mazingira
    • Afya
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Fedha na Utawala
      • Mipango miji na Mazingira
      • Uchumi, Afya na Elimu
      • Kudhitibi UKIMWI
      • Maadili
    • Kamati zingine/Bodi/Uwakilishi
    • Ratiba
      • Vikao vya Madiwani
      • Kuonana na Mstahiki Meya
  • Miradi
    • Miradi itakayotekelezwa
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Ripoti
    • Sheria Ndogo
    • Miongozo
    • Mpango Mkakati
    • Fomu
    • Jifunze Nyumbani
    • Mpango Kabambe
    • Jarida
    • Asemavyo Mahia - Afya na Mazingira
  • Kituo cha habari
    • Taarifa kwa vyombo vya habari
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya picha
    • Habari
    • Matukio
  • City TV

Spika Ndugai amuonesha Jafo ujenzi wa shule ya Wasichana Bunge

Imewekwa tarehe: February 28th, 2020

Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Job Ndugai tarehe 25/02/2020 alimpeleka Waziri wa Nchi, OR-TAMISEMI Mhe. Selemani Jafo eneo inapojengwa shule maalumu ya wasichana itakayojulikana kama Shule ya Sekondari ya Wasichana Bunge inayojengwa katika eneo la Kikombo katika Halmashauri ya Jiji la Dodoma.

Akiwa katika eneo hilo la ujenzi Spika wa Bunge Mhe. Job Ndugai alisema ni vyema Waziri anayehusika na uendeshaji na usimamizi wa shule akajua mapema sehemu inapojengwa na maendeleo ya ujenzi wake ili kama kuna maboresho aweze kuyatoa mapema na kufanyiwa kazi.

“Hapa tunajenga kwa kutumia ‘Force Account’ mfumo ule ule ulioasisiwa na TAMISEMI na ramani za majengo ni zile zile za TAMISEMI ila kuna baadhi ya maeneo tumeboresha kidogo lakini hatujaenda nje ya maelekezo ya Wizara hii kuhusu ujenzi wa miundombinu ya shule” Alisema Spika Mhe. Ndugai.

Akizungumzia wazo wa kujenga shule hiyo Spika Ndugai alisema Waheshimiwa Wabunge Walifanya changizo kupitia matukio ya kijamii na wadau mbalimbali wakachangia jumla ya kiasi cha shilingi bilioni 1.2 fedha hiyo ilipatikana kutoka katika sehemu ya posho za Wabunge na michango ya wadau hao.

“Lengo la awali ilikua kujenga vyoo vya mfano vya wasichana katika kila Jimbo Nchini lakini baadae tukaona tuunganishe nguvu tujenge kitu kimoja kikubwa kitakachoacha alama ya Bunge la 11 mara litakapomaliza muda wake”.

Hakika katika hili, Bunge la 11 limefanya kazi ya zaida, zaidi ya ile ambayo tumeizoea na ipo Kisheria ambayo ni kutunga Sheria. Wakati huu tumeamua kufanya kazi ya Jamii itakayoboresha Elimu ya mtoto wa Kike wa Tanzania na tukaelekeza nguvu katika ujenzi wa shule hii ya mfano ya Wasichana alisema Spika Ndugai.

“Shule hii inayojengwa itakua na  miundombinu yote inayohitajika kwa ajili ya Shule ya Sekondari kuanzia madarasa ya kutosha, maabara, mabweni, bwalo la kisasa, vyoo, ofisi za walimu, jengo la utawala pamoja na library yenye miundombinu ya TEHAMA” aliongeza Spika Ndugai.

Aidha Spika Ndugai ameweka wazi kuwa ujenzi wa shule hiyo utakamilika mwezi Juni, 2020 na kwa umoja wa Bunge la 11 wataikabidhi kwa Waziri wa TAMISEMI Mhe. Jafo mbele ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. John Pombe Joseph Magufuli.

Akizungumza akiwa katika eneo la ujenzi wa shule hiyo Waziri wa Nchi OR-TAMISEMI Mhe. Selemani Jafo amemshukuru Spika wa Bunge Mhe. Job Ndugai pamoja na Wabunge wote wa Bunge la 11 kwa michango yao na wazo lenye tija la kujenga shule maalumu ya Wasichana ya Bunge.

“Nimefarijika sana kuona wazo hili limeanza kutekelezwa na ndoto ya Bunge la 11 sasa inaanza kutimia na kwa sababu Spika amekuja kunionesha, kuanzia leo na mimi nitakuwa napita mara kwa mara kuangalia maendeleo ya ujenzi huu ili kwa pamoja tuweze kuikamilisha ndoto hii ya Bunge letu” alisema Jafo kwa msisitizo.

Nitahakikisha kuwa Shule hii mara inapokamilika na kukabidhiwa TAMISEMI tunapanga walimu wenye ubora na wanafunzi wenye ufaulu mzuri ili kwa pamoja waweze kuleta matokeo mazuri ya shule hii, tunakata shule hii iwe ya mfano na maalumu kwa heshima ya Bunge la 11 alisema Jafo.

“Tunataka tuienzi shule hii kwa heshima ya Bunge la 11, tutafanya kila linalowezekana kuhakikisha wanafunzi watakaosoma hapa wanafaulu kwa viwango vya juu ili shule hii iweze kuingia katika shule kumi bora za Tanzania katika matokeo ya kidato cha sita alisisitiza Jafo.

Chanzo: Tovuti ya tamisemi.go.tz


Matangazo

  • MKUTANO WA BARAZA LA WAHESHIMIWA MADIWANI January 30, 2025
  • KITUO CHA AFYA ILAZO KIMEANZA KUTOA HUDUMA January 13, 2025
  • HOSPITALI YA JIJI LA DODOMA IMEANZA KUTOA HUDUMA ZA AFYA January 12, 2025
  • TANGAZO LA UUZWAJI WA VIWANJA KIKOMBO December 03, 2024
  • Angalia zote

Habari za hivi punde

  • Barabara ya Lami ya Kilometa 6 yawanufaisha wakazi wa Kata ya Miyuji

    April 23, 2025
  • Huduma ya Chakula na Lishe yapandisha ufaulu Shule ya Sekondari Nala

    April 22, 2025
  • Mradi wa Maji Nala wa Bil. 1.3, mkombozi kwa wananchi

    April 22, 2025
  • Milioni 500 kukamilisha mradi wa Kituo cha Afya Kizota

    April 22, 2025
  • Angalia zote

Video

Watendaji Kata Wilaya ya Dodoma watakiwa kusimamia maswala ya Lishe
Video zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • Historia ya Manispaa
  • Wasifu wa Manispaa
  • Kata na Madiwani
  • Mji wa Serikali
  • Orodha ya Madiwani
  • Mpango Mkakati wa Halmashauri (SP)
  • Kwanini uwekeze Dodoma?
  • Zabuni za Wakala wa Ukusanyaji Mapato
  • Zabuni ya Usafi wa Mazingira

Viunganishi Linganifu

  • Msalato Sekondari
  • Mkoa wa Dodoma
  • OR-TAMISEMI
  • Utumishi
  • Chuo Kikuu Dodoma (UDOM)
  • Bunge

World visitors tracker

world map hits counter

Idadi ya watembeleaji

free HitCounter

Ramani elekezi

Wasiliana nasi

    1 CDA Street, 40477

    Anuani ya posta: 1249, DODOMA, TANZANIA

    Simu: +255 26 232 4817

    Simu ya kiganjani:

    Baruapepe: cd@dodomacc.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya tovuti

Copyright ©2017 The City Council of Dodoma. All rights reserved.