MKURUGENZI wa Jiji la Dodoma Dkt. Fredrick Sagamiko amesema matumizi ya SPV (Special Purpose Vehicle) ni njia bora ya usimamizi na uendeshaji wa miradi ya vitega uchumi vya Halmashauri ili kuweza kufikia lengo maalumu lililokusudiwa kwa kuanziashwa kwa vitega uchumi hivyo ikiwemo kutoa huduma kwa Wananchi na kukusanya mapato kwa Halmashauri.
Dkt. Sagamiko ameyasema hayo katika kikao kazi cha maandalizi ya mpango na bajeti kwa mwaka 2025/26 kwa wataalamu wa mipango kutoka ofisi ya Rais TAMISEMI, Ofisi za Wakuu wa Mikoa na Mamlaka za Serikali za Mitaa kinachoendelea katika Ukumbi wa VETA Jijini Dodoma.
Amesema SPV ni chombo cha kisheria (kampuni) inayoanzishwa kwaajili ya kusimamia shughuli mbalimbali zikiwemo za kibiashara na uzalishaji katika taasisi husika ikiwemo Mamlaka ya Serikali za Mitaa.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa Sera na Mipango Ofisi ya Rais TAMISEMI Bw. John Mihayo Cheyo amesema Serikali imekwisha kuandaa miongozo maalumu kwaajili ya usimamizi na uendesheja wa vituo vyote SPV katika Halmashauri zote nchini.
1 CDA Street, 40477
Anuani ya posta: 1249, DODOMA, TANZANIA
Simu: +255 26 232 4817
Simu ya kiganjani:
Baruapepe: cd@dodomacc.go.tz
Copyright ©2017 The City Council of Dodoma. All rights reserved.