• Wasiliana nasi |
    • Maswali na majibu |
    • Baruapepe - Watumishi |
    • eVibali |
    • Malalamiko |
Dodoma City Council
Dodoma City Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Jiji la Dodoma

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa taasisi
    • Idara
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Mipango, Takwimu na Ufuatiliaji
      • Afya
      • Fedha na Biashara
      • Elimu ya Msingi
      • Elimu ya Sekondari
      • Maji
      • Kilimo, Umwagiliaji na Ushirika
      • Mifugo na Uvuvi
      • Ardhi na Mipango Miji
      • Maendeleo ya Jamii, Ustawi wa Jamii, Jinsia na Vijana
      • Ujenzi
      • Mazingira na Udhibiti wa Taka ngumu
    • Vitengo
      • Sheria na Usalama
      • Mkaguzi wa Ndani
      • TEHAMA na Uhusiano
      • Manunuzi
      • Uchaguzi
      • Ufugaji Nyuji
    • Ward
  • Fursa za Uwekezaji
    • Maeneo ya Utalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
    • Mji wa Serikali
    • Kwa nini uwekeze Dodoma?
  • Huduma Zetu
    • Maendeleo ya jamii
    • Elimu
    • Miundombinu
    • Mazingira
    • Afya
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Fedha na Utawala
      • Mipango miji na Mazingira
      • Uchumi, Afya na Elimu
      • Kudhitibi UKIMWI
      • Maadili
    • Kamati zingine/Bodi/Uwakilishi
    • Ratiba
      • Vikao vya Madiwani
      • Kuonana na Mstahiki Meya
  • Miradi
    • Miradi itakayotekelezwa
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Ripoti
    • Sheria Ndogo
    • Miongozo
    • Mpango Mkakati
    • Fomu
    • Jifunze Nyumbani
    • Mpango Kabambe
    • Jarida
    • Asemavyo Mahia - Afya na Mazingira
  • Kituo cha habari
    • Taarifa kwa vyombo vya habari
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya picha
    • Habari
    • Matukio
  • City TV

Suala la kuboresha Lishe Bora ni Agizo la Viongozi wote- Dkt. Mollel

Imewekwa tarehe: October 30th, 2022

NAIBU Waziri wa Afya Dkt. Godwin Mollel ameweka wazi kuwa, agizo alilotoa Rais Samia kwa Wakuu wa Mikoa juu ya kusimamia suala la kuboresha lishe bora ni agizo la viongozi wote.

Dkt. Mollel amesema hayo leo kwenye Maadhimisho ya siku ya lishe ambayo kitaifa yamefanyika katika viwanja vya Mikese Mkoani Morogoro na kuwataka Wadau kukutana na viongozi hao kuona namna gani ya kutekeleza agizo hilo.

"Rais wetu Samia Suluhu Hassan ameshaelekeza Wakuu wa Mikoa namna ya kusimamia lishe kwenye Mikoa yao, agizo la Mhe. Rais hawajaagizwa Wakuu wa Mikoa peke yao, ni kwamba sisi Mawaziri, Manaibu Waziri na kila kiongozi asimame kwenye mstari wa mbele kutekeleza maelekezo ya Rais kwenye eneo la lishe." Amesema Dkt. Mollel.

Ameendelea kusema kuwa, Wadau wa maendeleo wamekuwa wakifanya kazi nzuri katika suala la lishe ikiwemo kutengeneza mashine za kuchanganya virutubisho kwenye vyakula ili kutengeneza lishe bora, hivyo kuwaelekeza Wakuu wa Mikoa na viongozi wengine kukaa pamoja kuona namna gani ya kuzitumia mashine hizo.

Ameendelea kusisitiza kuwa, mashine hizo za kuchanganya virutubisho licha ya kuboresha suala la lishe kwa wananchi hususan watoto litasaidia kuongeza ajira kwa vijana na Wanawake kwa kukuza kipato chao.

Sambamba na hilo Dkt. Mollel ametoa wito kwa wazazi kuwapa watoto lishe bora ili kuwajenga kimwili na kutengeneza Taifa lenye watu wenye akili, huku akisisitiza kuwa Dunia ya watu walioendelea ni kwasababu namba kubwa ya wananchi wao wana akili inayotokana na lishe bora.

"Kila Mkuu wa Mkoa anatamani kuona shule zake zinaongoza kwa elimu, kusimamia Walimu kuingia darasani tu haitoshi kuwa sababu ya kuongoza kielimu kama hatutasimamia suala
la lishe bora kwa watoto wetu." Amesema Dkt Mollel 

Pia, ametoa wito kwa Wadau kuendelea kushirikiana na Serikali kwa karibu ili kusaidia kufikisha virutubisho vitavyowekwa kwenye vyakula kama uji wa watoto ili wapate lishe bora
utaowasaidia kukuza kiwango cha uelewa.


Matangazo

  • MKUTANO WA BARAZA LA WAHESHIMIWA MADIWANI January 30, 2025
  • KITUO CHA AFYA ILAZO KIMEANZA KUTOA HUDUMA January 13, 2025
  • HOSPITALI YA JIJI LA DODOMA IMEANZA KUTOA HUDUMA ZA AFYA January 12, 2025
  • TANGAZO LA UUZWAJI WA VIWANJA KIKOMBO December 03, 2024
  • Angalia zote

Habari za hivi punde

  • Barabara ya Lami ya Kilometa 6 yawanufaisha wakazi wa Kata ya Miyuji

    April 23, 2025
  • Huduma ya Chakula na Lishe yapandisha ufaulu Shule ya Sekondari Nala

    April 22, 2025
  • Mradi wa Maji Nala wa Bil. 1.3, mkombozi kwa wananchi

    April 22, 2025
  • Milioni 500 kukamilisha mradi wa Kituo cha Afya Kizota

    April 22, 2025
  • Angalia zote

Video

Watendaji Kata Wilaya ya Dodoma watakiwa kusimamia maswala ya Lishe
Video zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • Historia ya Manispaa
  • Wasifu wa Manispaa
  • Kata na Madiwani
  • Mji wa Serikali
  • Orodha ya Madiwani
  • Mpango Mkakati wa Halmashauri (SP)
  • Kwanini uwekeze Dodoma?
  • Zabuni za Wakala wa Ukusanyaji Mapato
  • Zabuni ya Usafi wa Mazingira

Viunganishi Linganifu

  • Msalato Sekondari
  • Mkoa wa Dodoma
  • OR-TAMISEMI
  • Utumishi
  • Chuo Kikuu Dodoma (UDOM)
  • Bunge

World visitors tracker

world map hits counter

Idadi ya watembeleaji

free HitCounter

Ramani elekezi

Wasiliana nasi

    1 CDA Street, 40477

    Anuani ya posta: 1249, DODOMA, TANZANIA

    Simu: +255 26 232 4817

    Simu ya kiganjani:

    Baruapepe: cd@dodomacc.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya tovuti

Copyright ©2017 The City Council of Dodoma. All rights reserved.