• Wasiliana nasi |
    • Maswali na majibu |
    • Baruapepe - Watumishi |
    • eVibali |
    • Malalamiko |
Dodoma City Council
Dodoma City Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Jiji la Dodoma

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa taasisi
    • Idara
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Mipango, Takwimu na Ufuatiliaji
      • Afya
      • Fedha na Biashara
      • Elimu ya Msingi
      • Elimu ya Sekondari
      • Maji
      • Kilimo, Umwagiliaji na Ushirika
      • Mifugo na Uvuvi
      • Ardhi na Mipango Miji
      • Maendeleo ya Jamii, Ustawi wa Jamii, Jinsia na Vijana
      • Ujenzi
      • Mazingira na Udhibiti wa Taka ngumu
    • Vitengo
      • Sheria na Usalama
      • Mkaguzi wa Ndani
      • TEHAMA na Uhusiano
      • Manunuzi
      • Uchaguzi
      • Ufugaji Nyuji
    • Ward
  • Fursa za Uwekezaji
    • Maeneo ya Utalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
    • Mji wa Serikali
    • Kwa nini uwekeze Dodoma?
  • Huduma Zetu
    • Maendeleo ya jamii
    • Elimu
    • Miundombinu
    • Mazingira
    • Afya
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Fedha na Utawala
      • Mipango miji na Mazingira
      • Uchumi, Afya na Elimu
      • Kudhitibi UKIMWI
      • Maadili
    • Kamati zingine/Bodi/Uwakilishi
    • Ratiba
      • Vikao vya Madiwani
      • Kuonana na Mstahiki Meya
  • Miradi
    • Miradi itakayotekelezwa
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Ripoti
    • Sheria Ndogo
    • Miongozo
    • Mpango Mkakati
    • Fomu
    • Jifunze Nyumbani
    • Mpango Kabambe
    • Jarida
    • Asemavyo Mahia - Afya na Mazingira
  • Kituo cha habari
    • Taarifa kwa vyombo vya habari
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya picha
    • Habari
    • Matukio
  • City TV

Tahadhari yatolewa matumizi ya vijiti, pamba za kusafisha masikio

Imewekwa tarehe: June 21st, 2019

Imeelezwa kuwa vijiti na pamba za kusafisha masikio zinasababisha kwa kiasi kikubwa magonjwa ya usikivu yanayopelekea kuwa kiziwi.

Hayo yamebainishwa wakati wataalamu wa afya ya masikio na usikivu kutoka taasisi ya "Starkey Foundation for Ear and Healing Care" walipomweleza Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu wakati alipotembelea mabanda ya utoaji wa huduma za masikio na usikivu kwa wananchi mbalimbali jijini Dodoma.

Kufuatia hatua hiyo, Waziri Ummy amewataka wananchi kulinda masikio yao kwa kufuata ushauri wa madaktari na kuacha tabia ya kutumia vifaa vinavyosababisha matatizo ya usikivu kama spika za masikioni na matumizi ya pamba za kutolea uchafu.

“Tatizo la usikivu ni kubwa katika nchi yetu, katika tafiti ndogo ndogo ambazo zimefanyika zinaonesha asilimia 3 ya wanafunzi ambao wako shuleni wana matatizo ya usikivu kwa kiwango fulani lakini pia takwimu zinaonesha kuwa kila watu 100 wenye magonjwa yasiyo ya kuambukiza, 24 kati yao wanakua na matatizo ya usikivu”. Amesema Waziri Ummy.

Aidha, Waziri Ummy amesema tafiti zinaonesha pia waathirika wengine wenye matatizo ya usikivu ni wale wanaofanya kazi katika migodi na viwandani hasa viwanda vya nguo ambapo takwimu zinaonyesha asilimia 50 wanakua na matatizo hayo.

Waziri Ummy ameishukuru taasisi ya "Starkey Foundation for Ear and Healing Care" kwa kutoa huduma za masikio na usikivu nchini huku akisema Serikali imeweka mikakati ya kuimarisha miundombinu, kununua vifaa na kuongeza wataalamu wa huduma za masikio na usikivu, kutoka wataalamu bingwa 11 mwaka 2009 mpaka kufikia wataalamu 46 mwaka 2018.

Hata hivyo Waziri Ummy amesema toka kuanzishwa kwa huduma hizi nchini kumesaidia kupunguza idadi ya watoto kupelekwa India, ambapo kila mwaka takribani watoto 13 walikua wanapelekwa India kupata matibabu na mtoto mmoja alikua anagharimu Tsh. Milioni 80 mpaka Milioni 100. Lakini kuanzishwa kwa huduma hizi katika Hospitali ya Muhimbili mwaka 2017, watoto takribani 26 wamepata huduma kwa gharama ya Tsh. Milioni 35 na kuokoa fedha za Serikali kwa zaidi ya asilimia 60.

Kwa upande wake muanzilishi wa taasisi ya Starkey Foundation for Ear and Healing Care Dkt. Bill Austin ameishukuru Serikali ya Tanzania kwa kutoa ushirikiano kwa taasisi hiyo kuendelea kutoa huduma na vifaa vya masikio na usikivu kwa wananchi ambapo ilianza kutoa huduma hizo Jijini Mwanza na kuendelea kutoa huduma Jijini Dodoma.

Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu akifafanua jambo kutoka kwenye kitabu cha Mpango Mkakati wa Masuala ya Masikio na Usikivu leo Jijini kabla ya kuzindua mpango huo.

Dkt. Bill Austin (kulia) kutoka Taasisi ya Starkey Hearing Foundation akifafanua jambo wakati wa uzinduzi wa Mpango Mkakati wa Masuala ya Masikio na Usikivu Jijini Dodoma aliye kushoto ni  mke wake Dkt. Tani Austin.

Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu (wa pili kutoka kushoto) akizindua rasmi Mpango Mkakati wa Masuala ya Masikio na Usikivu akiwa pamoja na Bwana na Bibi Bill Austin (waliovaa makoti meupe) kutoka Taasisi ya Starkey Hearing Foundation, kutoka kushoto ni Dkt. Grace Maghembe Mkurugenzi wa Tiba kutoka Wizara ya Afya na Daktari Bingwa wa Masikio na Usikivu Dkt Edwin Liyombo (wa pili kutoka kulia)

Wananchi waliojitokeza kupata matibabu ya masikio katika kliniki inayoendeshwa na Taasisi ya Starkey Hearing Foundation leo Jijini Dodoma.

Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu (kushoto) akifuatilia mtaalam wakati akifunga vifaa vya usikivu kwa mtoto Monica Denis kabla ya kuzindua Mpango Mkakati wa Taifa wa Masuala ya Masikio na Usikivu Jijini Dodoma. 


Chanzo: Blogu ya Wizara ya Afya (www.afyablog.moh.go.tz)

Matangazo

  • MKUTANO WA BARAZA LA WAHESHIMIWA MADIWANI January 30, 2025
  • KITUO CHA AFYA ILAZO KIMEANZA KUTOA HUDUMA January 13, 2025
  • HOSPITALI YA JIJI LA DODOMA IMEANZA KUTOA HUDUMA ZA AFYA January 12, 2025
  • TANGAZO LA UUZWAJI WA VIWANJA KIKOMBO December 03, 2024
  • Angalia zote

Habari za hivi punde

  • Barabara ya Lami ya Kilometa 6 yawanufaisha wakazi wa Kata ya Miyuji

    April 23, 2025
  • Huduma ya Chakula na Lishe yapandisha ufaulu Shule ya Sekondari Nala

    April 22, 2025
  • Mradi wa Maji Nala wa Bil. 1.3, mkombozi kwa wananchi

    April 22, 2025
  • Milioni 500 kukamilisha mradi wa Kituo cha Afya Kizota

    April 22, 2025
  • Angalia zote

Video

Watendaji Kata Wilaya ya Dodoma watakiwa kusimamia maswala ya Lishe
Video zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • Historia ya Manispaa
  • Wasifu wa Manispaa
  • Kata na Madiwani
  • Mji wa Serikali
  • Orodha ya Madiwani
  • Mpango Mkakati wa Halmashauri (SP)
  • Kwanini uwekeze Dodoma?
  • Zabuni za Wakala wa Ukusanyaji Mapato
  • Zabuni ya Usafi wa Mazingira

Viunganishi Linganifu

  • Msalato Sekondari
  • Mkoa wa Dodoma
  • OR-TAMISEMI
  • Utumishi
  • Chuo Kikuu Dodoma (UDOM)
  • Bunge

World visitors tracker

world map hits counter

Idadi ya watembeleaji

free HitCounter

Ramani elekezi

Wasiliana nasi

    1 CDA Street, 40477

    Anuani ya posta: 1249, DODOMA, TANZANIA

    Simu: +255 26 232 4817

    Simu ya kiganjani:

    Baruapepe: cd@dodomacc.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya tovuti

Copyright ©2017 The City Council of Dodoma. All rights reserved.