WAZIRI Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Kassim Majaliwa amepongeza jitihada zinazofanywa na Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo katika kukuza Sanaa na muziki na kuitangaza Tanzania kupitia Tamasha la Muziki la Serengeti linalofanyika katika viwanja vya Bustani ya kupumzikia ya Chinangali Jijini Dodoma.
Mhe. Majaliwa ametoa kauli hiyo leo kupitia simu ya Katibu Mkuu wa Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dkt. Hassan Abbasi ambapo amefafanua kuwa Serikali inaunga mkono jitihada hizo na kwamba tamasha hili litaendelea kuboreshwa zaidi mwakani ili lnengo lake liweze kufikiwa.
Pia amesema kupitia Tamasha hili Rais wa Jamhuri ya Muungano anawasalimu na kuwapongeza wasanii kwa kazi nzuri wanazofanya katika kuitangaza Tanzania.
Aidha, amemwelekeza Katibu Mkuu Dkt. Hassan Abbasi kusimamia Waziri wa Utamaduni kusimamia kufanya tathmini ya Tamasha hili kubaini changamoto ili zisaidie kuboresha tamasha la mwakani.
Naye Naibu Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Pauline Gekul amemshukuru Mhe. Waziri Mkuu na amemhakikishia kuendelea kutekeleza maelekezo yote kwa faida ya wasanii wa Tanzania.
Tamasha hili limehudhuriwa pia na viongozi mbalimbali wa Serikali, Wabunge na Naibu Waziri wa Kilimo na Mbunge wa Jimbo la Dodoma mjini, Mhe. Anthony Mavunde.
Tamasha hili la siku mbilli Machi 12 na 13, 2022 linatarajiwa kuwapandisha wasanii takribani 200.
1 CDA Street, 40477
Anuani ya posta: 1249, DODOMA, TANZANIA
Simu: +255 26 232 4817
Simu ya kiganjani:
Baruapepe: cd@dodomacc.go.tz
Copyright ©2017 The City Council of Dodoma. All rights reserved.