Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), anayeshughulikia Afya, Dkt. Jafar Seif, amewaagiza Waganga Wakuu wa Mikoa, Halmashauri na Wafawidhi wote kutangaza huduma mpya za Afya zinazoongezwa kwenye vituo vyao vya kutolea huduma ili kutoa fursa kwa jamii kutumia huduma husika.
Naibu Waziri Dkt. Seif ametoa agizo hilo alipofanya ziara ya ukaguzi wa ujenzi wa miundombinu katika hospitali ya Frelimo na kituo cha afya Itimba, manispaa ya Iringa mkoani humo.
Amesema Serikali imefanya maboresho makubwa hasa ya kununua vifaa tiba vya kutolea huduma mbalimbali za kibingwa, lakini sehemu kubwa ya wananchi wanaozunguka vituo husika wamesalia bila taarifa ya uwepo wa huduma hizo katika maeneo yao, na hivyo kuagiza kuwekwa kwa utaratibu rahisi na rafiki wa kuwahabarisha wananchi juu ya ongezeko la huduma mpya katika maeneo yao.
1 CDA Street, 40477
Anuani ya posta: 1249, DODOMA, TANZANIA
Simu: +255 26 232 4817
Simu ya kiganjani:
Baruapepe: cd@dodomacc.go.tz
Copyright ©2017 The City Council of Dodoma. All rights reserved.