• Wasiliana nasi |
    • Maswali na majibu |
    • Baruapepe - Watumishi |
    • eVibali |
    • Malalamiko |
Dodoma City Council
Dodoma City Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Jiji la Dodoma

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa taasisi
    • Idara
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Mipango, Takwimu na Ufuatiliaji
      • Afya
      • Fedha na Biashara
      • Elimu ya Msingi
      • Elimu ya Sekondari
      • Maji
      • Kilimo, Umwagiliaji na Ushirika
      • Mifugo na Uvuvi
      • Ardhi na Mipango Miji
      • Maendeleo ya Jamii, Ustawi wa Jamii, Jinsia na Vijana
      • Ujenzi
      • Mazingira na Udhibiti wa Taka ngumu
    • Vitengo
      • Sheria na Usalama
      • Mkaguzi wa Ndani
      • TEHAMA na Uhusiano
      • Manunuzi
      • Uchaguzi
      • Ufugaji Nyuji
    • Ward
  • Fursa za Uwekezaji
    • Maeneo ya Utalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
    • Mji wa Serikali
    • Kwa nini uwekeze Dodoma?
  • Huduma Zetu
    • Maendeleo ya jamii
    • Elimu
    • Miundombinu
    • Mazingira
    • Afya
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Fedha na Utawala
      • Mipango miji na Mazingira
      • Uchumi, Afya na Elimu
      • Kudhitibi UKIMWI
      • Maadili
    • Kamati zingine/Bodi/Uwakilishi
    • Ratiba
      • Vikao vya Madiwani
      • Kuonana na Mstahiki Meya
  • Miradi
    • Miradi itakayotekelezwa
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Ripoti
    • Sheria Ndogo
    • Miongozo
    • Mpango Mkakati
    • Fomu
    • Jifunze Nyumbani
    • Mpango Kabambe
    • Jarida
    • Asemavyo Mahia - Afya na Mazingira
  • Kituo cha habari
    • Taarifa kwa vyombo vya habari
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya picha
    • Habari
    • Matukio
  • City TV

Tanzania ni salama kwa utalii

Imewekwa tarehe: August 18th, 2020

BODI ya Utalii Tanzania imesema dunia imefahamu ukweli kuhusu usalama wa Tanzania dhidi ya virusi vya Corona, ndio maana watalii wanamiminika kwa wingi kila siku kuja kutalii na kuingiza fedha nyingi za kigeni.

Hayo yamesemwa jana na Ofisa Masoko wa Bodi ya Utalii Tanzania, Francis Malugu, bodi hiyo hivi karibuni ilipokea mamia ya watalii kutoka sehemu mbalimbali za dunia kupitia viwanja vya ndege vya Mwalimu Julius Nyerere jijini Dar es Salaam na Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro (KIA) mkoani Kilimanjaro.

Alisema mashirika mbalimbali ya ndege ya kimataifa yakiwamo KLM, Ethiopian Airways, Qatar Airways na la Falme za Kiarabu la Emirates, ni miongoni mwa mashirika yanayoleta watalii wengi nchini kutoka sehemu mbalimbali duniani.

Kutokana taifa kuwa salama dhidi ya Virusi vya Corona, Baraza la Wasafiri na Utalii Duniani (WTTC) hivi karibuni iliitambua Tanzania kama nchi salama zaidi duniani na kuipa stempu maalum inayoitambulisha kuwa na kiwango cha juu cha usalama.

Kwa mujibu wa Waziri wa Maliasili na Utalii, Dkt. Hamis Kigwangala, watalii wengi kabla ya kufanya uamuzi wa kutembelea nchi yoyote, huwa kwanza wanataka kujihakikishia usalama wa nchi husika kuanzia ulinzi, huduma za vyakula, malazi na usafiri, hivyo stempu hiyo inawapa uhakika wa kupata huduma hizo.

Wakati hali ya utalii ikiwa shwari Tanzania, baadhi ya nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC), zimekiri kuathiriwa kwa sekta zao za utalii ambazo ndio nguzo ya mapato katika uchumi wao kutokana na virusi vya Corona.

Wiki iliyopita, nchi za Kenya, Uganda na Rwanda zilithibitisha kupata athari kubwa kutokana na virusi vya Corona ambavyo vimesababisha anga  la mataifa hayo kufungwa, hivyo watalii kushindwa kuingia tofauti na ilivyokuwa kabla ya virusi hivyo kuingia.

Hali ilivyo Kenya

Bodi ya Utalii ya nchi hiyo imesema baada ya kufungua anga na uchumi wa nchi Agosti Mosi, hakuna mtalii hata mmoja ambaye ameonesha nia ya kutembelea vivutio vya nchi hiyo ikiwamo mbuga ya wanyama maarufu ya Maasai Mara iliyoanzishwa mwaka 1961.

Kauli hiyo iliungwa mkono na mmiliki wa kampuni ya kusafirisha watalii nchini humo, Milton Ole Siloma, wakati akizungumza na Shirika la Habari la Aljazeera, ambapo alisema mpaka sasa ni nusu mwezi tangu anga kufunguliwa, lakini hakuna mtalii hata mmoja aliyefika nchini humo.

Kwa mujibu wa Wizara ya Maliasili na Utalii nchini Kenya, mpaka kufikia Agosti, mwaka jana, taifa hilo lilikuwa limepata zaidi ya watalii milioni mbili, wengi wao kutoka katika nchi za Marekani, Ulaya na China na kuingiza zaidi ya dola za Marekani bilioni 1.4.

Lakini mpaka kufikia Agosti, mwaka huu, Kenya imepata hasara ya dola za Marekani milioni 752 kutokana na athari za virusi vya corona.

Nchini Uganda

Serikali ya nchi hiyo imegeukia wananchi wake kuwahamasisha washiriki katika utalii wa ndani kutokana na athari mbaya ya virusi vya corona zilioosababisha ukosefu wa watalii kutoka nje ya nchi.

Hivi karibuni, Bodi ya Utalii ya nchi hiyo, ilisema janga la corona limesababisha kuwa na uhaba mkubwa wa watalii kutoka nje ya nchi, hali iliyoilazimisha kuangalia utalii wa ndani kama njia mbadala ya kuihuisha sekta hiyo.

Kwa mujibu wa bodi hiyo, kabla ya virusi vya corona kuingia nchini humo, Uganda ilikuwa ikipata watalii zaidi ya milioni moja, lakini baada ya kutangazwa sheria ya ‘lockdown’, watalii wamepungua kwa asilimia 22.

Hali mbaya Rwanda

Bodi ya Maendeleo ya Utalii  Rwanda imesema virusi vya Corona vimesababisha hasara kubwa kwa uchumi wa nchi hiyo mwaka huu.

Taarifa iliyotolewa na bodi hiyo baada ya kufungua shughuli za kitalii mapema mwezi huu, ilisema nchi hiyo inakadiria kuwa mapato ya utalii yatapungua kwa kati ya asilimia 50 hadi 70.

Taifa hilo ambalo utalii wake mkubwa ni sokwe wa milimani, lilipata watalii milioni 1.6 mwaka jana na kuingiza dola za Marekani milioni 498, lakini mwaka huu kutakuwa na punguzo la karibu asilimia 70 ya ingizo hilo.

Taarifa hiyo iliongeza kuwa, kutengemaa kwa sekta hiyo kunaweza kusubiri hadi kadiri ya miezi 12 hadi 18 ijayo.




Chanzo: HabariLeo


Matangazo

  • MKUTANO WA BARAZA LA WAHESHIMIWA MADIWANI January 30, 2025
  • KITUO CHA AFYA ILAZO KIMEANZA KUTOA HUDUMA January 13, 2025
  • HOSPITALI YA JIJI LA DODOMA IMEANZA KUTOA HUDUMA ZA AFYA January 12, 2025
  • TANGAZO LA UUZWAJI WA VIWANJA KIKOMBO December 03, 2024
  • Angalia zote

Habari za hivi punde

  • Barabara ya Lami ya Kilometa 6 yawanufaisha wakazi wa Kata ya Miyuji

    April 23, 2025
  • Huduma ya Chakula na Lishe yapandisha ufaulu Shule ya Sekondari Nala

    April 22, 2025
  • Mradi wa Maji Nala wa Bil. 1.3, mkombozi kwa wananchi

    April 22, 2025
  • Milioni 500 kukamilisha mradi wa Kituo cha Afya Kizota

    April 22, 2025
  • Angalia zote

Video

Watendaji Kata Wilaya ya Dodoma watakiwa kusimamia maswala ya Lishe
Video zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • Historia ya Manispaa
  • Wasifu wa Manispaa
  • Kata na Madiwani
  • Mji wa Serikali
  • Orodha ya Madiwani
  • Mpango Mkakati wa Halmashauri (SP)
  • Kwanini uwekeze Dodoma?
  • Zabuni za Wakala wa Ukusanyaji Mapato
  • Zabuni ya Usafi wa Mazingira

Viunganishi Linganifu

  • Msalato Sekondari
  • Mkoa wa Dodoma
  • OR-TAMISEMI
  • Utumishi
  • Chuo Kikuu Dodoma (UDOM)
  • Bunge

World visitors tracker

world map hits counter

Idadi ya watembeleaji

free HitCounter

Ramani elekezi

Wasiliana nasi

    1 CDA Street, 40477

    Anuani ya posta: 1249, DODOMA, TANZANIA

    Simu: +255 26 232 4817

    Simu ya kiganjani:

    Baruapepe: cd@dodomacc.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya tovuti

Copyright ©2017 The City Council of Dodoma. All rights reserved.