MADAKTARI katika Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) wamefanikisha upasuaji wa kuwatenganisha watoto pacha walioungana kifuani Rehema na Neema.
Upasuaji huo uliodumu kwa saa 7, ulioanza saa 3 asubuhi na kumalizika saa 9 alasiri, umefanikiwa licha ya ugumu na changamoto kubwa kwa watoto hao kuungana ini, moyo na baadhi ya tishu za ndani.
Upasuaji huo umefanyika kwa mafanikio leo Ijumaa Julai Mosi 2022 kwa ushirikiano kati ya wataalamu wa afya 31 kutoka Tanzania na Ireland ambao wanatokea Shirika la Operation Child Life.
Akizungumza na vyombo vya habari, Daktari bingwa wa upasuaji watoto hospitalini hapo, Zaitun Bokhari amesema upasuaji huo umefanywa na madaktari bingwa wa upasuaji watoto wadogo 12.
“Madaktari wa usingizi sita, madaktari wa kutengeneza ngozi ‘plastic surgery’ wanne, madaktari ambao kazi yao kuangalia mfumo mzima wa watoto unakwenda vizuri wawili na wauguzi 6,” amesema.
Kufanyika kwa upasuaji huu leo unaandika historia nyingine kwa kuwa Tanzania inakua nchi ya tatu baada ya Misri na Afrika Kusini katika bara la Afrika kufanya upasuaji mgumu zaidi kwa pacha walioungana.
1 CDA Street, 40477
Anuani ya posta: 1249, DODOMA, TANZANIA
Simu: +255 26 232 4817
Simu ya kiganjani:
Baruapepe: cd@dodomacc.go.tz
Copyright ©2017 The City Council of Dodoma. All rights reserved.