SERIKALI ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imepokea msaada wa Dola zaMarekani milioni 90 sawa na shilingi bilioni 240.95 kutoka Mfuko wa Ushirikianowa Elimu Duniani (GPE), kwa ajili ya kugharamia miradi miwili ya Sekta yaElimu.
Mikataba ya msaada huo imesainiwa katika ukumbi wa Wizara ya Fedha naMipango jijini Dar es Salaam, na Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Bw. Doto James kwaupande wa Serikali na Balozi wa Sweden nchini, Bw. Anders Sjoberg, ambaye nchiyake ni Wakala wa Msaada huo kupitia Shirika la Maendeleo la Kimataifa la nchihiyo (SIDA).
Akizungumza katika hafla ya utiaji saini mikataba ya msaada huo, Katibu Mkuuwa Wizara ya Fedha na Mipango, Bw. Doto James alisema msaada huo ni kwa ajiliya kugharamia miradi ya Mpango wa Maendeleo ya Sekta ya Elimu (ESDP) 2016/17 –2021/22 na nyongeza ya Mpango wa Elimu kwa Matokeo (EP4R).
“Kati ya fedha hizo za msaada, dola za Marekani milioni 38.89 (Sh. bil.88.55) zitatumika kughagharamia Mpango wa Maendeleo ya Sekta ya Elimu (ESDP)2016/17 – 2021/22 na dola za Marekani milioni 51.11 (Sh. bil. 116.40) ni kwaajili ya nyongeza katika mchango wa Sweden katika Mpango wa Elimu kwa Matokeo(EP4R) ulioanza tangu mwaka 2015”, alifafanua.
Alisema fedha za kugharamia Mpango wa Maendeleo ya Sekta ya Elimu zitatumikakutimiza malengo mahsusi ya programu za Sekta ndogo za elimu ya msingi, elimujumuishi na watu wazima pamoja na elimu nje ya mfumo rasmi.
Alibainisha kuwa utekelezaji wa miradi hiyo utachangia kwa kiasi kikubwakufikia malengo ya Mapango wa Pili wa Taifa wa Maendeleo wa miaka mitano ambaopamoja na mambo mengine unalenga kuboresha Sekta ya Elimu kupitia Mafunzo yaKusoma, Kuandika na Kuhesabu (LANES), kuongeza udahili wa wanafunzi pamoja nakuboresha mazingira ya kusomea kwa kujenga madarasa.
Aliishukuru Serikali ya Sweden kwa kuratibu upatikanaji wa fedha hizi ambazozinafanya uwekezaji wa nchi hiyo hapa nchini kufikia zaidi ya shilingi trilioni1.25 zilizowekezwa kwenye miradi mbalimbali ikiwemo mapitio ya matumizi yafedha za Umma, maliasili na hifadhi ya jamii, elimu, nishati, utafiti, nakusisitiza kuwa uhusiano wan chi hizo mbili utaendelea kuimarika.
Aidha, Bw. James amempongeza Mhe. Rais wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania,Dkt. John Pombe Joseph Magufuli, kwa jitihada zake kubwa za kusimamia miradimbalimbali ya maendeleo ikiwemo maboresho makubwa katika Sekta ya Elimu,ikiwemo utoaji elimu bila malipo kuanzia shule za msingi hadi sekondari.
Naye Balozi wa Sweden Tanzania, Bw. Anders Sjoberg, aliipongezaSerikali ya Tanzania kwa jitihada mbalimbali iliyochukua katika kuboresha elimuhususani katika awamu ya kwanza ya programu ya Mafunzo ya Kusoma, Kuandika naKuhesabu (LANES) pamoja na Mpango wa Maendeleo ya Sekta ya Elimu (ESDP) 2017 –2021.
Aliishauri Serikali ya Tanzania kuangalia kwa karibu suala la maendeleo yaelimu ya mtoto wa kike hasa kipindi cha kutoka elimu ya msingi kwenda Sekondaripamoja na kuboresha matokeo yao.
Alibainisha kuwa Sweden na washirika wengine wa maendeleo wapo tayarikushirikiana na Tanzania katika kuendeleza miradi mbalimbali ya maendeleoikiwemo elimu.
Kwa upande wake Mkuu wa Shirika la Misaada ya Maendeleo la Uingereza (DFID),Bi. Beth Arthy akizungumza kwa niaba ya washirika wengine wa maendeleo,ameipongeza Serikali ya Tanzania kwa kupiga hatua katika Sekta ya elimu ambayomatokeo yake yanaongezeka kila mwaka.
Alisema matokeo hayo yanatokana na mikakati mbalimbali iliyowekwa katikaSekta hiyo ikiwemo mpango wa elimu bila malipo ambao umeongeza idadi yawanafunzi na kuiwezesha Tanzania kujizolea umaarufu duniani.
Pamoja na maendelo hayo, Bi. Arthy aliishauri Serikali kuongeza idadi yawalimu mashuleni ili waweze kuhudumia wanafunzi kwa ufanisi na kuongeza ufauluzaidi.
“Tangu kuanzishwa kwa programu ya elimu bila malipo idadi ya wanafunzimashuleni imeongezeka kwa kasi tofauti na idadi ya walimu waliopo haliinayowafanya walimu kufanyakazi kubwa zaidi ya uwezo wao” aliongeza Bi. Arthy.
Akipokea msaada huo kwa shukrani, Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu, Sayansi naTeknolojia, Dkt. Leonard Akwilapo, alisema kuwa Wizara hiyo itahakikisha fedhahizo zinatumika kwa malengo yaliyokusudiwa ili kuhakikisha Elimu bora kwawote inapatikana Tanzania.
Msaada huoumechangiwa na washirika mbalimbali wa maendeleo wakiwemo UNICEF,UNESCO, Benki ya Dunia, Umoja wa Ulaya, Australia, Canada, Denmark, Ufaransa,Korea, Uholanzi, Norway, Hispania, Uswiss, Marekani na Uingereza kupitia Mfukowa Ushirikiano wa Elimu Duniani (GPE)
1 CDA Street, 40477
Anuani ya posta: 1249, DODOMA, TANZANIA
Simu: +255 26 232 4817
Simu ya kiganjani:
Baruapepe: cd@dodomacc.go.tz
Copyright ©2017 The City Council of Dodoma. All rights reserved.