• Wasiliana nasi |
    • Maswali na majibu |
    • Baruapepe - Watumishi |
    • eVibali |
    • Malalamiko |
Dodoma City Council
Dodoma City Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Jiji la Dodoma

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa taasisi
    • Idara
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Mipango, Takwimu na Ufuatiliaji
      • Afya
      • Fedha na Biashara
      • Elimu ya Msingi
      • Elimu ya Sekondari
      • Maji
      • Kilimo, Umwagiliaji na Ushirika
      • Mifugo na Uvuvi
      • Ardhi na Mipango Miji
      • Maendeleo ya Jamii, Ustawi wa Jamii, Jinsia na Vijana
      • Ujenzi
      • Mazingira na Udhibiti wa Taka ngumu
    • Vitengo
      • Sheria na Usalama
      • Mkaguzi wa Ndani
      • TEHAMA na Uhusiano
      • Manunuzi
      • Uchaguzi
      • Ufugaji Nyuji
    • Ward
  • Fursa za Uwekezaji
    • Maeneo ya Utalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
    • Mji wa Serikali
    • Kwa nini uwekeze Dodoma?
  • Huduma Zetu
    • Maendeleo ya jamii
    • Elimu
    • Miundombinu
    • Mazingira
    • Afya
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Fedha na Utawala
      • Mipango miji na Mazingira
      • Uchumi, Afya na Elimu
      • Kudhitibi UKIMWI
      • Maadili
    • Kamati zingine/Bodi/Uwakilishi
    • Ratiba
      • Vikao vya Madiwani
      • Kuonana na Mstahiki Meya
  • Miradi
    • Miradi itakayotekelezwa
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Ripoti
    • Sheria Ndogo
    • Miongozo
    • Mpango Mkakati
    • Fomu
    • Jifunze Nyumbani
    • Mpango Kabambe
    • Jarida
    • Asemavyo Mahia - Afya na Mazingira
  • Kituo cha habari
    • Taarifa kwa vyombo vya habari
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya picha
    • Habari
    • Matukio
  • City TV

Tanzania yapunguza maambukizi ya Malaria kwa asilimia 50

Imewekwa tarehe: November 10th, 2019

Serikali kupitia Wizara ya Afya imefanikiwa kupunguza maambukizi ya malaria kwa takribani asilimia 50% kutoka 14.8% mwaka 2015 mpaka kufikia 7.3% mwaka 2017.

Hayo yamesemwa jana na Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu wakati wakiongozana na Mawaziri kutoka nchi za SADC ziarani Mkoa wa Pwani, Kibaha kutembelea Kiwanda cha Viuadudu wa kibaiolojia cha TBPL.

Waziri Ummy Mwalimu amesema, mafanikio haya ni kutokana na kuwekeza rasilimali fedha, utashi wa viongozi, wadau mbalimbali na jamii kwa ujumla katika kutekeleza mikakati ya udhibiti wa malaria.

Mojawapo ya afua zilizochukuliwa na Serikali ya Tanzania katika kudhibiti ugonjwa wa malaria ni kujenga kiwanda cha viuadudu vya kibailojia kwa ajili ya kuua mazalia, alibainisha Waziri Ummy.

Aliendelea kusisitiza kuwa matumizi ya viuadudu hivyo vya kibailojia ni kwa ajili ya kuangamiza viluilui vya mbu wanavyoeneza magonjwa mbalimbali yakiwemo; malaria, homa ya dengue, zika, homa ya manjano, matende, giri-majihoma ya bonde la ufa na chikungunya.

Aidha, Waziri Ummy amesema  kuwa ili kuendeleza mafanikio na hatimae kutokomeza kabisa malaria katika nchi zote za SADC tunahitaji kuongeza wigo na kuhakikisha nchi wanachama wanaongeza rasilimali fedha ili kutekeleza afua  mbalimbali za udhibti wa malaria, alisema.

Aidha, Waziri Ummy akiongozana na Mawaziri wa nchi za Jumuiya ya Maendeleo ya nchi Kusini mwa Afrika (SADC) alifanya ziara katika Bohari ya Dawa MSD, huku kwa kiasi kikubwa kuonekana kuridhishwa na hali ya utendaji kazi wa Bohari ya Dawa nchini (MSD), kutokana na mfumo mzuri wa manunuzi na usambazaji wa dawa, vifaa, vifaatiba na vitendanishi.

Waziri Ummy ambae pia ni, Mwenyekiti wa baraza hilo la Mawaziri amesema wameridhishwa na utendaji kazi wa bohari hiyo na kwamba sasa wanasubiri hatua za mwisho zikamilike manunuzi yaanze.

“Wameshuhudia MSD wana uwezo, utaalamu, vifaa kwa hiyo mawaziri wameridhika na hali waliyoikuta hapa  na tunaamini kwa kununua dawa kwa pamoja kama nchi za Sadc bei pia itashuka,” amesema Ummy Mwalimu.

Mbali na hayo, Waziri Ummy amesema kuwa, MSD ina uwezo na utaalamu unaokidhi viwango katika manunuzi na usambazaji wa dawa, hali iliyopelekea kushinda zabuni ya usambazaji wa dawa kwa nchi wanachama wa SADC.

Picha mbalimbali za matukio kwenye ziara ya mawaziri wa SADC.




Chanzo: afyablog.moh.go.tz


Matangazo

  • MKUTANO WA BARAZA LA WAHESHIMIWA MADIWANI January 30, 2025
  • KITUO CHA AFYA ILAZO KIMEANZA KUTOA HUDUMA January 13, 2025
  • HOSPITALI YA JIJI LA DODOMA IMEANZA KUTOA HUDUMA ZA AFYA January 12, 2025
  • TANGAZO LA UUZWAJI WA VIWANJA KIKOMBO December 03, 2024
  • Angalia zote

Habari za hivi punde

  • Barabara ya Lami ya Kilometa 6 yawanufaisha wakazi wa Kata ya Miyuji

    April 23, 2025
  • Huduma ya Chakula na Lishe yapandisha ufaulu Shule ya Sekondari Nala

    April 22, 2025
  • Mradi wa Maji Nala wa Bil. 1.3, mkombozi kwa wananchi

    April 22, 2025
  • Milioni 500 kukamilisha mradi wa Kituo cha Afya Kizota

    April 22, 2025
  • Angalia zote

Video

Watendaji Kata Wilaya ya Dodoma watakiwa kusimamia maswala ya Lishe
Video zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • Historia ya Manispaa
  • Wasifu wa Manispaa
  • Kata na Madiwani
  • Mji wa Serikali
  • Orodha ya Madiwani
  • Mpango Mkakati wa Halmashauri (SP)
  • Kwanini uwekeze Dodoma?
  • Zabuni za Wakala wa Ukusanyaji Mapato
  • Zabuni ya Usafi wa Mazingira

Viunganishi Linganifu

  • Msalato Sekondari
  • Mkoa wa Dodoma
  • OR-TAMISEMI
  • Utumishi
  • Chuo Kikuu Dodoma (UDOM)
  • Bunge

World visitors tracker

world map hits counter

Idadi ya watembeleaji

free HitCounter

Ramani elekezi

Wasiliana nasi

    1 CDA Street, 40477

    Anuani ya posta: 1249, DODOMA, TANZANIA

    Simu: +255 26 232 4817

    Simu ya kiganjani:

    Baruapepe: cd@dodomacc.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya tovuti

Copyright ©2017 The City Council of Dodoma. All rights reserved.