Serikali imetangaza kifo cha kwanza cha mgonjwa wa Covid-19 ugonjwa unaosababishwa na virusi vya Corona. Kifo hicho kimetokea leo alfajiri ya tarehe 31 Machi 2020 katika kituo cha wagonjwa wa Covid-19 kilichopo Mloganzila, Dar es Salaam.
Kwa masikitiko makubwa, Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu ameliambia Taifa kuwa mgonjwa huyo ni mwanaume mwenye umri wa miaka 49 ambaye pia alikuwa akisumbuliwa na maradhi mengine.
Aidha, amesema kuwa hadi kufikia leo asubuhi jumla ya watu waliopata maambukizi ya Covid-19 hapa nchini ni 19, aliyepona mmoja (1) na kifo kimoja (1).
Kutoma taarifa kwa umma bofya hapa: Taarifa ya Kifo cha kwanza cha mgonjwa wa Corona Machi 31, 2020
1 CDA Street, 40477
Anuani ya posta: 1249, DODOMA, TANZANIA
Simu: +255 26 232 4817
Simu ya kiganjani:
Baruapepe: cd@dodomacc.go.tz
Copyright ©2017 The City Council of Dodoma. All rights reserved.