• Wasiliana nasi |
    • Maswali na majibu |
    • Baruapepe - Watumishi |
    • eVibali |
    • Malalamiko |
Dodoma City Council
Dodoma City Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Jiji la Dodoma

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa taasisi
    • Idara
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Mipango, Takwimu na Ufuatiliaji
      • Afya
      • Fedha na Biashara
      • Elimu ya Msingi
      • Elimu ya Sekondari
      • Maji
      • Kilimo, Umwagiliaji na Ushirika
      • Mifugo na Uvuvi
      • Ardhi na Mipango Miji
      • Maendeleo ya Jamii, Ustawi wa Jamii, Jinsia na Vijana
      • Ujenzi
      • Mazingira na Udhibiti wa Taka ngumu
    • Vitengo
      • Sheria na Usalama
      • Mkaguzi wa Ndani
      • TEHAMA na Uhusiano
      • Manunuzi
      • Uchaguzi
      • Ufugaji Nyuji
    • Ward
  • Fursa za Uwekezaji
    • Maeneo ya Utalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
    • Mji wa Serikali
    • Kwa nini uwekeze Dodoma?
  • Huduma Zetu
    • Maendeleo ya jamii
    • Elimu
    • Miundombinu
    • Mazingira
    • Afya
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Fedha na Utawala
      • Mipango miji na Mazingira
      • Uchumi, Afya na Elimu
      • Kudhitibi UKIMWI
      • Maadili
    • Kamati zingine/Bodi/Uwakilishi
    • Ratiba
      • Vikao vya Madiwani
      • Kuonana na Mstahiki Meya
  • Miradi
    • Miradi itakayotekelezwa
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Ripoti
    • Sheria Ndogo
    • Miongozo
    • Mpango Mkakati
    • Fomu
    • Jifunze Nyumbani
    • Mpango Kabambe
    • Jarida
    • Asemavyo Mahia - Afya na Mazingira
  • Kituo cha habari
    • Taarifa kwa vyombo vya habari
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya picha
    • Habari
    • Matukio
  • City TV

TMA yasaini mkataba wa rada ya Dodoma, Kilimanjaro

Imewekwa tarehe: April 6th, 2021

MAMLAKA ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA), imesaini mkataba wa ununuzi  wa Rada mbili za hali ya hewa zitakazofungwa eneo la Nala mkoani Dodoma na Maretoni, Arumeru mpakani mwa mkoa wa Kilimanjaro na Arusha. 

Akizungumza katika hafla fupi ya kusaini mkataba huo, Mwenyekiti wa Bodi ya TMA, Dkt. Buruhani Nyenzi alisema kuwa ununuzi wa Rada hizo mbili za mwisho unakamilisha mtandao wa Rada saba nchini. 

“Ununuzi wa Rada hizi mbili kwa ajili ya Dodoma na Kilimanjaro unagharimu kiasi cha  dola za kimarekani 4,990,447.00, utengenezaji na ufungaji wake utachukua miezi kumi na nne hadi kukamilika kwake”. Alisema Dkt. Nyenzi. Awali Mwenyekiti huyo wa Bodi, aliwataka washiriki wa hafla hiyo fupi kusimama na kuwa na dakika moja ya utulivu ili kumkumbuka Rais wetu Mpendwa Hayati Dkt. John Joseph Pombe Magufuli ambaye katika kipindi cha uongozi wake huduma za hali ya hewa nchini zimeboreshwa kawa kasi kubwa.

“Rada hizi zinauwezo wa kuona zaidi ya kilometa za mkato 450 huku zikizunguka na kuona matone madogo sana ya mvua katika hali ya uhalisia ndani ya kilometa 250. Aidha, mitambo hii pia inasaidia katika kukusanya data za hali ya hewa zinazoonesha uhalisi wa anga letu la Tanzania”. Aliongeza kusema Dkt. Nyenzi. 

Kwa upande wa Mkurugenzi Mkuu wa TMA na Makamu wa Tatu wa Rais wa Shirika la Hali ya Hewa Duniani (WMO), Dkt. Agnes Kijazi aliishukuru Serikali ya Awamu ya Tano chini ya uongozi wa Hayati Dkt. John Joseph Pombe Magufuli kwa kuiwezesha TMA kutengewa fedha za miradi ya maendeleo ambazo zimefanikisha upatikanaji wa Rada 5.

“Katika kipindi kifupi cha miaka mitano ya uongozi wa Jemadari wetu Hayati Dkt. John Joseph Pombe Magufuli, TMA imeweza kutimiza lengo la kuwa na Rada saba (7) za hali ya hewa nchini, haya ni mafanikio makubwa  sana kwa Mamlaka kuweza kupatikana kwa Rada hizo kwa kipindi kifupi”. Alizungumza Dkt. Kijazi.

Aidha, Dkt. Kijazi aliahidi kuendelea kutoa ushirikiano kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango ili kuhakikisha huduma za hali ya hewa zinatolewa kwa viwango vya kimataifa na hivyo kuweza kusaidia kukuza uchumi wa nchi yetu. “Mabadiliko ya hali ya hewa (Climate change) yamekuwa na athari kubwa duniani kote, ambapo hapa nchini tumeshuhudia kubadilika kwa mifumo ya hali ya hewa yenye athari katika utabiri wa msimu na matukio ya majanga yanayosababishwa na hali mabaya ya hewa, ambapo kuwepo kwa vifaa vya kisasa ukiwepo mtandao wa rada kutaiwezesha TMA kutoa huduma bora kwa maendeleo ya Taifa letu”. Alisistiza Dkt. Kijazi.

Naye, mwakilishi kutoka Kampuni ya Enterprise Electronics Corporation (EEC) kutoka Marekani, Bw. Edwin Kisanga alisema mkataba huo unajumuisha pia mafunzo ya wataalamu kutoka TMA yatakayofanyika hapa nchini na kiwandani kule Marekani.

Mkataba huo umesainiwa baina ya TMA na EEC, ukishuhudiwa na Mwenyekiti wa Bodi ya TMA, Dkt Buruhani Nyenzi, Mjumbe wa Bodi  ya TMA kutoka Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi, Mhandisi Aron Kisaka, Mwanasheria kutoka TMA Adv. Emanuel Ntenga, Mwanasheria kutoka EEC Adv. Seni Malimi, menejimenti ya TMA  na baadhi ya wageni waalikwa.

Kwa sasa Mamlaka imeshafunga Rada tatu katika sehemu za Dar es Salaam, Mwanza na Mtwara, na ipo katika hatua za mwisho za matengenezo ya Rada za Mbeya na Kigoma. TMA inaendelea kusisitizaa wananchi wanaoishi karibu na mitambo ya Rada za hali ya hewa,  kuilinda na kuitunza mitambo hiyo kwa manufaa ya Taifa letu.

Matangazo

  • MKUTANO WA BARAZA LA WAHESHIMIWA MADIWANI January 30, 2025
  • KITUO CHA AFYA ILAZO KIMEANZA KUTOA HUDUMA January 13, 2025
  • HOSPITALI YA JIJI LA DODOMA IMEANZA KUTOA HUDUMA ZA AFYA January 12, 2025
  • TANGAZO LA UUZWAJI WA VIWANJA KIKOMBO December 03, 2024
  • Angalia zote

Habari za hivi punde

  • Barabara ya Lami ya Kilometa 6 yawanufaisha wakazi wa Kata ya Miyuji

    April 23, 2025
  • Huduma ya Chakula na Lishe yapandisha ufaulu Shule ya Sekondari Nala

    April 22, 2025
  • Mradi wa Maji Nala wa Bil. 1.3, mkombozi kwa wananchi

    April 22, 2025
  • Milioni 500 kukamilisha mradi wa Kituo cha Afya Kizota

    April 22, 2025
  • Angalia zote

Video

Watendaji Kata Wilaya ya Dodoma watakiwa kusimamia maswala ya Lishe
Video zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • Historia ya Manispaa
  • Wasifu wa Manispaa
  • Kata na Madiwani
  • Mji wa Serikali
  • Orodha ya Madiwani
  • Mpango Mkakati wa Halmashauri (SP)
  • Kwanini uwekeze Dodoma?
  • Zabuni za Wakala wa Ukusanyaji Mapato
  • Zabuni ya Usafi wa Mazingira

Viunganishi Linganifu

  • Msalato Sekondari
  • Mkoa wa Dodoma
  • OR-TAMISEMI
  • Utumishi
  • Chuo Kikuu Dodoma (UDOM)
  • Bunge

World visitors tracker

world map hits counter

Idadi ya watembeleaji

free HitCounter

Ramani elekezi

Wasiliana nasi

    1 CDA Street, 40477

    Anuani ya posta: 1249, DODOMA, TANZANIA

    Simu: +255 26 232 4817

    Simu ya kiganjani:

    Baruapepe: cd@dodomacc.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya tovuti

Copyright ©2017 The City Council of Dodoma. All rights reserved.