Serikali imefuta tozo za kuhamisha fedha kutoka benki kwenda mitandao ya simu.
Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Mwigulu Nchemba akiwasilisha kauli ya Serikali ametangaza kufutwa tozo ya kuhamisha fedha kutoka benki kwenda mitandao ya simu, kufuta tozo ya kuhamisha fedha ndani ya benki moja, kufuta tozo ya kuhamisha fedha toka benki moja kwenda nyingine na kusamehe tozo ya miamala ya utoaji fedha kupitia ATM kwa miamala isiyozidi shilingi 30,000.
Aidha, Waziri Mchemba ametangaza kupunguza gharama za miamala ya siku kwa asilimia 10 hadi 50 kutokana na kundi la miamala.
1 CDA Street, 40477
Anuani ya posta: 1249, DODOMA, TANZANIA
Simu: +255 26 232 4817
Simu ya kiganjani:
Baruapepe: cd@dodomacc.go.tz
Copyright ©2017 The City Council of Dodoma. All rights reserved.