• Wasiliana nasi |
    • Maswali na majibu |
    • Baruapepe - Watumishi |
    • eVibali |
    • Malalamiko |
Dodoma City Council
Dodoma City Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Jiji la Dodoma

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa taasisi
    • Idara
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Mipango, Takwimu na Ufuatiliaji
      • Afya
      • Fedha na Biashara
      • Elimu ya Msingi
      • Elimu ya Sekondari
      • Maji
      • Kilimo, Umwagiliaji na Ushirika
      • Mifugo na Uvuvi
      • Ardhi na Mipango Miji
      • Maendeleo ya Jamii, Ustawi wa Jamii, Jinsia na Vijana
      • Ujenzi
      • Mazingira na Udhibiti wa Taka ngumu
    • Vitengo
      • Sheria na Usalama
      • Mkaguzi wa Ndani
      • TEHAMA na Uhusiano
      • Manunuzi
      • Uchaguzi
      • Ufugaji Nyuji
    • Ward
  • Fursa za Uwekezaji
    • Maeneo ya Utalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
    • Mji wa Serikali
    • Kwa nini uwekeze Dodoma?
  • Huduma Zetu
    • Maendeleo ya jamii
    • Elimu
    • Miundombinu
    • Mazingira
    • Afya
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Fedha na Utawala
      • Mipango miji na Mazingira
      • Uchumi, Afya na Elimu
      • Kudhitibi UKIMWI
      • Maadili
    • Kamati zingine/Bodi/Uwakilishi
    • Ratiba
      • Vikao vya Madiwani
      • Kuonana na Mstahiki Meya
  • Miradi
    • Miradi itakayotekelezwa
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Ripoti
    • Sheria Ndogo
    • Miongozo
    • Mpango Mkakati
    • Fomu
    • Jifunze Nyumbani
    • Mpango Kabambe
    • Jarida
    • Asemavyo Mahia - Afya na Mazingira
  • Kituo cha habari
    • Taarifa kwa vyombo vya habari
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya picha
    • Habari
    • Matukio
  • City TV

Treni yarejea Arusha baada ya miaka 30

Imewekwa tarehe: August 15th, 2020

TRENI ya kwanza ya mizigo ya majaribio imewasili katika Stesheni ya Arusha baada ya zaidi ya miaka 30 ikitokea Tanga na kupokelewa na maelfu ya wananchi waliojitokeza katika Stesheni hiyo Agosti 13, 2020.

Treni hiyo iliwasili jijini Arusha ikiwa na shehena ya tani 400 za Saruji, ambapo Mkuu wa Wilaya ya Arusha mjini Mhe. Kenani Kihongsi kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe. Idd Kimanta aliungana na wananchi wa Arusha kuipokea treni hiyo. Katika tukio hilo la kihistoria Mkuu wa wilaya ya Arumeru Mhe. Jerry Muro aliungana na watumishi kutoka Shirika la Reli Tanzania – TRC kwa kupanda treni hiyo kutoka Stesheni ya Usa River hadi stesheni ya Arusha.

Kurejeshwa kwa safari za treni kwa reli ya Kaskazini ni moja kati ya utekelezaji mkubwa wa ahadi za Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya kurejesha huduma hiyo ambapo Julai 2019 Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa alizindua rasmi usafiri wa treni kati ya Dar es Salaam na Moshi ambapo huduma zinaendelea na hivi karibuni huduma za usafiri wa treni Dar es Salaam, Tanga na Arusha zitazinduliwa rasmi baada ya majaribio ya njia kufanikiwa kwa kiwango kikubwa.

“Tumekuja kuwaambia kwamba kazi ya miaka mitano ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli katika kutekeleza ilani ya Chama Cha Mapinduzi leo inakamilika katika mkoa wetu wa Arusha” alisema Mkuu wa Wilaya ya Arumeru Mhe. Jerry Muro

Aidha, Mkuu wa Wilaya ya Arusha mjini aliongeza kuwa ni zaidi ya miaka 30 reli hiyo imeacha kufanya kazi na baadhi ya wananchi wamezaliwa hawajawahi kuiona treni lakini kwa kipindi cha miaka mitano ya Amiri Jeshi Mkuu na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli treni imeweza kufika Arusha na wananchi wanaanza kunufaika na fursa zilizoletwa na treni hiyo.

Baadhi ya wananchi waliojitokeza kuipokea treni hiyo wameeleza maoni yao juu ya kurejea kwa huduma hizo ambapo wameonesha kufurahishwa na maamuzi hayo na kuonesha utayari wa kuchangamkia fursa zitokazokuwepo ikiwemo biashara na ajira ambazo zimeanza kuonekana mara baada ya treni ya shehena ya saruji kuwasili jijini hapo ambapo vijana wamejipatia kibarua cha kupakua mizigo kutoka kwenye treni.

“Treni hii tumeipokea kwa mikono miwili, tumefurahi na tunaendelea kumuunga mkono Rais Magufuli aweze kufanya yale yanayomgusa kila mtu ili maendeleo ya leo na kesho, kwa sababu Saruji tunayonunua leo 15,000 itapungua bei kutokana na usafiri huu nafuu” alisema James Peter mkazi wa jiji la Arusha.

Sambamba na kuwasili kwa treni ya majaribio iliyobeba Tani 800 za Saruji, Shirika la Reli linaendelea na kutoa elimu ya uelewa katika Shule, maeneo ya mikusanyiko ikiwemo vituo vya Mabasi, Pikipiki na mikutano ya wananchi kuhamasisha wananchi kutunza miundombinu ya reli na kuzingatia usalama katika maeneo ya reli ili kuepusha ajali.


Matangazo

  • MKUTANO WA BARAZA LA WAHESHIMIWA MADIWANI January 30, 2025
  • KITUO CHA AFYA ILAZO KIMEANZA KUTOA HUDUMA January 13, 2025
  • HOSPITALI YA JIJI LA DODOMA IMEANZA KUTOA HUDUMA ZA AFYA January 12, 2025
  • TANGAZO LA UUZWAJI WA VIWANJA KIKOMBO December 03, 2024
  • Angalia zote

Habari za hivi punde

  • Barabara ya Lami ya Kilometa 6 yawanufaisha wakazi wa Kata ya Miyuji

    April 23, 2025
  • Huduma ya Chakula na Lishe yapandisha ufaulu Shule ya Sekondari Nala

    April 22, 2025
  • Mradi wa Maji Nala wa Bil. 1.3, mkombozi kwa wananchi

    April 22, 2025
  • Milioni 500 kukamilisha mradi wa Kituo cha Afya Kizota

    April 22, 2025
  • Angalia zote

Video

Watendaji Kata Wilaya ya Dodoma watakiwa kusimamia maswala ya Lishe
Video zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • Historia ya Manispaa
  • Wasifu wa Manispaa
  • Kata na Madiwani
  • Mji wa Serikali
  • Orodha ya Madiwani
  • Mpango Mkakati wa Halmashauri (SP)
  • Kwanini uwekeze Dodoma?
  • Zabuni za Wakala wa Ukusanyaji Mapato
  • Zabuni ya Usafi wa Mazingira

Viunganishi Linganifu

  • Msalato Sekondari
  • Mkoa wa Dodoma
  • OR-TAMISEMI
  • Utumishi
  • Chuo Kikuu Dodoma (UDOM)
  • Bunge

World visitors tracker

world map hits counter

Idadi ya watembeleaji

free HitCounter

Ramani elekezi

Wasiliana nasi

    1 CDA Street, 40477

    Anuani ya posta: 1249, DODOMA, TANZANIA

    Simu: +255 26 232 4817

    Simu ya kiganjani:

    Baruapepe: cd@dodomacc.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya tovuti

Copyright ©2017 The City Council of Dodoma. All rights reserved.