NAIBU WAZIRI wa Afya, Mheshimiwa Dkt. Godwin Mollel amewataka wananchi kuchukua tahadhari juu ya mlipuko wa ugonjwa wa Ebola ambao umeripotiwa hivi karibuni katika Nchi jirani ya Uganda.
Dkt. Mollel amesema hayo alipokuwa Halmashauri ya Wilaya ya Msalala, Mkoani Geita katika ziara ya kutembelea na kukagua miradi ya Afya inayotekelezwa katika ngazi ya Kata
“Ni rahisi kuukwepa ugonjwa wa Ebola. Jufunzeni, fuateni taratibu mlizopewa kadri ya miongozo ya Afya iliyotolewa na Wizara ya Afya” amesema Dkt. Mollel.
Pamoja na hayo, Dkt. Mollel aliwahikikishia Wananchi wa Msalala kuwa Tanzania bado ipo salama lakini akasisitiza kuwa Tanzania itakuwa salama zaidi endapo kila mwananchi atafuata kanuni na miongozo ya Afya kadri ilivyotolewa na Wizara ya Afya.
1 CDA Street, 40477
Anuani ya posta: 1249, DODOMA, TANZANIA
Simu: +255 26 232 4817
Simu ya kiganjani:
Baruapepe: cd@dodomacc.go.tz
Copyright ©2017 The City Council of Dodoma. All rights reserved.