• Wasiliana nasi |
    • Maswali na majibu |
    • Baruapepe - Watumishi |
    • eVibali |
    • Malalamiko |
Dodoma City Council
Dodoma City Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Jiji la Dodoma

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa taasisi
    • Idara
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Mipango, Takwimu na Ufuatiliaji
      • Afya
      • Fedha na Biashara
      • Elimu ya Msingi
      • Elimu ya Sekondari
      • Maji
      • Kilimo, Umwagiliaji na Ushirika
      • Mifugo na Uvuvi
      • Ardhi na Mipango Miji
      • Maendeleo ya Jamii, Ustawi wa Jamii, Jinsia na Vijana
      • Ujenzi
      • Mazingira na Udhibiti wa Taka ngumu
    • Vitengo
      • Sheria na Usalama
      • Mkaguzi wa Ndani
      • TEHAMA na Uhusiano
      • Manunuzi
      • Uchaguzi
      • Ufugaji Nyuji
    • Ward
  • Fursa za Uwekezaji
    • Maeneo ya Utalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
    • Mji wa Serikali
    • Kwa nini uwekeze Dodoma?
  • Huduma Zetu
    • Maendeleo ya jamii
    • Elimu
    • Miundombinu
    • Mazingira
    • Afya
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Fedha na Utawala
      • Mipango miji na Mazingira
      • Uchumi, Afya na Elimu
      • Kudhitibi UKIMWI
      • Maadili
    • Kamati zingine/Bodi/Uwakilishi
    • Ratiba
      • Vikao vya Madiwani
      • Kuonana na Mstahiki Meya
  • Miradi
    • Miradi itakayotekelezwa
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Ripoti
    • Sheria Ndogo
    • Miongozo
    • Mpango Mkakati
    • Fomu
    • Jifunze Nyumbani
    • Mpango Kabambe
    • Jarida
    • Asemavyo Mahia - Afya na Mazingira
  • Kituo cha habari
    • Taarifa kwa vyombo vya habari
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya picha
    • Habari
    • Matukio
  • City TV

Tumbaku yaendelea kuua mamilioni

Imewekwa tarehe: June 1st, 2021

TAKRIBANI watu milioni sita hufariki dunia kila mwaka kutokana na matumizi ya tumbaku na bidhaa zake zikiwemo sigara na shisha au kuvuta moshi kutoka kwa mvutaji huku kati ya hao ni watoto ambao hupoteza maisha kwa asilimia 28, wanawake asilimia 6 na wanaume asilimia 12, huku ikikadiriwa kuwa hadi kufikia mwaka 2030 vifo vitokanavyo na matumizi ya tumbaku vitaongezeka na kufikia zaidi ya milioni nane kwa mwaka.

Hayo yameelezwa leo na Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt. Dorothy Gwajima katika maadhimisho ya siku ya kutotumia tumbaku duniani yaliyofanyika Jijini Dar es Salaam ambapo amesema katika maadhimisho hayo ya Mei 31 dunia huadhimisha siku hiyo kwa kuelimisha dunia madhara ya kiafya yatokanayo na matumizi ya bidhaa za tumbaku kwa njia mbalimbali ikiwemo kunusa, kuvuta au kutafuna.

“Kauli mbiu ya mwaka huu ni "Dhamiria Kuacha Kutumia Tumbaku na Bidhaa zake.” Kauli mbiu hii imelenga kuhamasisha kuacha matumizi ya tumbaku kwa kuelimisha jamii kuhusu madhara ya kiafya yatokanayo na matumizi ya tumbaku na bidhaa zake na uhusiano uliopo baina ya matumizi ya tumbaku na bidhaa zake na magonjwa yasiyo ya kuambukiza, Kauli mbiu hii inahimiza kuwepo kwa mpango na hatua za Serikali na jamii ili kupunguza visababishi vya magonjwa yasiyoambukiza kutokana na tumbaku.” Amesema.

Gwajima amesema, licha ya watu laki sita kupoteza maisha kila mwaka kwa kutumia tumbaku na kuvuta moshi kutoka kwa mtumiaji, madhara yanayowapata waathirika ni pamoja na kupata magonjwa yasiyoambukiza ikiwemo saratani, magonjwa ya njia ya hewa, mapafu na kisukari na mengineyo ambayo huathiri moyo, mishipa ya damu na kuongeza uhatarishi wa kupata shinikizo la juu la damu.

”Pia tumbaku hupunguza kiwango cha oksijeni inayoweza kusafirishwa na damu na hivyo kuwa na uwezekano mkubwa wa kuifanya damu kuganda na kusababisha magonjwa mengine ya moyo ambayo huweza kupelekea kiharusi au kifo cha ghafla….Tuwalinde watoto tumeona asilimia 28 ya watoto hupoteza maisha kwa kuathirika na moshi kutoka kwa wavutaji, tunajenga taifa la watoto imara ni wajibu wetu kuwalinda, Wizara kwa kushirikiana na Serikali na jamii tunapaswa kuhamasika na bila kushurutisha katika kuacha matumizi ya tumbaku na bidhaa zake.” Amesema.

Amesema malengo katika maadhimisho ya mwaka huu ni kuhamasisha kuamua kwa dhati kuachana na matumizi ya tumbaku na bidhaa zake ili kuilinda jamii kutokana na madhara ya kiafya yatokanayo na tumbaku, kuongeza uelewa kwenye kundi kubwa la jamii juu ya madhara yanayoweza kupatikana kutokana na kutumia tumbaku au kuwa karibu na mtu anayetumia tumbaku pamoja na kuipa moyo nchi katika kuongeza nguvu kwenye utekelezaji wa mkataba wa kimataifa na kudhibiti matumizi ya bidhaa za tumbaku ili kuilinda jamii dhidi ya athari za matumizi ya tumbaku na bidhaa zake pamoja na kuepuka gharama kubwa za kutibu magonjwa yasiyoambukiza.

Kuhusu mkakati wa Serikali ya Tanzania katika suala hilo Dkt. Gwajima amesema Serikali inaendelea na utekelezaji wa sera ya Afya ya 2007 inayolenga kutoa huduma kwa magonjwa yasiyoambukizwa kwa umahiri zaidi kwa kushirikiana na Shirika la Afya Duniani (WHO) ambalo limekuwa likifanya jitihada mbalimbali za kudhibiti matumizi ya bidhaa za tumbaku na hadi sasa Serikali ya Tanzania inaendelea kusisitiza kuacha utumiaji wa bidhaa za tumbaku iitwayo ‘Shisha.’

Madhara yatokanayo na tumbaku na bidhaa zake hayawezi kudhibitiwa na Serikali pekee, bali kwa jamii hasa vijana na taasisi zisizo za kiserikali kutoa ushirikiano na kuhakikisha harakati zimepewa wito kwa kushiriki kikamilifu kwa kupokea elimu inayotolewa.

Matangazo

  • MKUTANO WA BARAZA LA WAHESHIMIWA MADIWANI January 30, 2025
  • KITUO CHA AFYA ILAZO KIMEANZA KUTOA HUDUMA January 13, 2025
  • HOSPITALI YA JIJI LA DODOMA IMEANZA KUTOA HUDUMA ZA AFYA January 12, 2025
  • TANGAZO LA UUZWAJI WA VIWANJA KIKOMBO December 03, 2024
  • Angalia zote

Habari za hivi punde

  • Barabara ya Lami ya Kilometa 6 yawanufaisha wakazi wa Kata ya Miyuji

    April 23, 2025
  • Huduma ya Chakula na Lishe yapandisha ufaulu Shule ya Sekondari Nala

    April 22, 2025
  • Mradi wa Maji Nala wa Bil. 1.3, mkombozi kwa wananchi

    April 22, 2025
  • Milioni 500 kukamilisha mradi wa Kituo cha Afya Kizota

    April 22, 2025
  • Angalia zote

Video

Watendaji Kata Wilaya ya Dodoma watakiwa kusimamia maswala ya Lishe
Video zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • Historia ya Manispaa
  • Wasifu wa Manispaa
  • Kata na Madiwani
  • Mji wa Serikali
  • Orodha ya Madiwani
  • Mpango Mkakati wa Halmashauri (SP)
  • Kwanini uwekeze Dodoma?
  • Zabuni za Wakala wa Ukusanyaji Mapato
  • Zabuni ya Usafi wa Mazingira

Viunganishi Linganifu

  • Msalato Sekondari
  • Mkoa wa Dodoma
  • OR-TAMISEMI
  • Utumishi
  • Chuo Kikuu Dodoma (UDOM)
  • Bunge

World visitors tracker

world map hits counter

Idadi ya watembeleaji

free HitCounter

Ramani elekezi

Wasiliana nasi

    1 CDA Street, 40477

    Anuani ya posta: 1249, DODOMA, TANZANIA

    Simu: +255 26 232 4817

    Simu ya kiganjani:

    Baruapepe: cd@dodomacc.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya tovuti

Copyright ©2017 The City Council of Dodoma. All rights reserved.