• Wasiliana nasi |
    • Maswali na majibu |
    • Baruapepe - Watumishi |
    • eVibali |
    • Malalamiko |
Dodoma City Council
Dodoma City Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Jiji la Dodoma

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa taasisi
    • Idara
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Mipango, Takwimu na Ufuatiliaji
      • Afya
      • Fedha na Biashara
      • Elimu ya Msingi
      • Elimu ya Sekondari
      • Maji
      • Kilimo, Umwagiliaji na Ushirika
      • Mifugo na Uvuvi
      • Ardhi na Mipango Miji
      • Maendeleo ya Jamii, Ustawi wa Jamii, Jinsia na Vijana
      • Ujenzi
      • Mazingira na Udhibiti wa Taka ngumu
    • Vitengo
      • Sheria na Usalama
      • Mkaguzi wa Ndani
      • TEHAMA na Uhusiano
      • Manunuzi
      • Uchaguzi
      • Ufugaji Nyuji
    • Ward
  • Fursa za Uwekezaji
    • Maeneo ya Utalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
    • Mji wa Serikali
    • Kwa nini uwekeze Dodoma?
  • Huduma Zetu
    • Maendeleo ya jamii
    • Elimu
    • Miundombinu
    • Mazingira
    • Afya
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Fedha na Utawala
      • Mipango miji na Mazingira
      • Uchumi, Afya na Elimu
      • Kudhitibi UKIMWI
      • Maadili
    • Kamati zingine/Bodi/Uwakilishi
    • Ratiba
      • Vikao vya Madiwani
      • Kuonana na Mstahiki Meya
  • Miradi
    • Miradi itakayotekelezwa
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Ripoti
    • Sheria Ndogo
    • Miongozo
    • Mpango Mkakati
    • Fomu
    • Jifunze Nyumbani
    • Mpango Kabambe
    • Jarida
    • Asemavyo Mahia - Afya na Mazingira
  • Kituo cha habari
    • Taarifa kwa vyombo vya habari
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya picha
    • Habari
    • Matukio
  • City TV

Tumieni haki yenu kupiga kura, Dodoma ni shwari - Wakili Mkufya

Imewekwa tarehe: October 25th, 2020

WAPIGA kura wa Jimbo la Dodoma mjini wametakiwa kutumia haki yao ya kikatiba kwenda kupiga kura na kumchagua Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mbunge na Madiwani bila wasiwasi.

Kauli hiyo ilitolewa na Msimamizi wa Uchaguzi Jimbo la Dodoma mjini, Wakili Msekeni Mkufya alipokuwa akiongea na waandishi wa habari ofisini kwake.

Wakili Mkufya alisema “wananchi ambao ni wapiga kura wa Jimbo la Dodoma mjini msiwe na wasiwasi wowote kwenda kupiga kura siku ya tarehe 28 Oktoba, 2020. Tumieni haki yenu ya kisheria kujitokeza kupiga kura kumchagua Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mbunge na Madiwani. Kama Msimamizi niliyepewa dhamana ya kusimamia uchaguzi huu mwaka 2020, nawahakikishia Dodoma ni shwari na mazingira yanaruhusu kufanya hivyo. Vituo vitakuwa wazi kwa muda uliopangwa kuwaruhusu kupiga kura kwa mujibu wa sheria.

Aidha, mtu atapiga kura mahali alipojiandikisha na anatakiwa kwenda na kadi yake ya kupigia kura. Daftari limehakikiwa, ikitokea akapata shida ya kuona jina lake yupo karani na msimamizi wa kituo kutoa msaada huo, aliongeza.

Alisema kuwa Tume ya Taifa ya Uchaguzi imejipanga vizuri kuhakikisha wananchi wote wenye sifa wanapiga kura. Hata kwa wale ambao hawaoni, zipo karatasi za nukta nundu kwa ajili yao, aliongeza. “Kwa wale wenye mahitaji maalum, Tume imetoa mwongozo mtu huyo anaweza kuja na mtu anayemwamini kumsaidia. Tume imetengeneza mazingira mazuri hata katika vituo vya kupigia kura ile sehemu ya kupigia kura ya faragha imetengenezwa kwa muundo unaomruhusu mtu mwenye ulemavu na mtu asiye na ulemavu kupiga kura kwa usawa” alisema Wakili Mkufya.

Jimbo la Dodoma mjini ni miongoni mwa majimbo makubwa likiwa na vituo vya kupigia kura 911, katika kata 41, likiwa na jumla ya wapiga kura 335,324.



Matangazo

  • MKUTANO WA BARAZA LA WAHESHIMIWA MADIWANI January 30, 2025
  • KITUO CHA AFYA ILAZO KIMEANZA KUTOA HUDUMA January 13, 2025
  • HOSPITALI YA JIJI LA DODOMA IMEANZA KUTOA HUDUMA ZA AFYA January 12, 2025
  • TANGAZO LA UUZWAJI WA VIWANJA KIKOMBO December 03, 2024
  • Angalia zote

Habari za hivi punde

  • Barabara ya Lami ya Kilometa 6 yawanufaisha wakazi wa Kata ya Miyuji

    April 23, 2025
  • Huduma ya Chakula na Lishe yapandisha ufaulu Shule ya Sekondari Nala

    April 22, 2025
  • Mradi wa Maji Nala wa Bil. 1.3, mkombozi kwa wananchi

    April 22, 2025
  • Milioni 500 kukamilisha mradi wa Kituo cha Afya Kizota

    April 22, 2025
  • Angalia zote

Video

Watendaji Kata Wilaya ya Dodoma watakiwa kusimamia maswala ya Lishe
Video zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • Historia ya Manispaa
  • Wasifu wa Manispaa
  • Kata na Madiwani
  • Mji wa Serikali
  • Orodha ya Madiwani
  • Mpango Mkakati wa Halmashauri (SP)
  • Kwanini uwekeze Dodoma?
  • Zabuni za Wakala wa Ukusanyaji Mapato
  • Zabuni ya Usafi wa Mazingira

Viunganishi Linganifu

  • Msalato Sekondari
  • Mkoa wa Dodoma
  • OR-TAMISEMI
  • Utumishi
  • Chuo Kikuu Dodoma (UDOM)
  • Bunge

World visitors tracker

world map hits counter

Idadi ya watembeleaji

free HitCounter

Ramani elekezi

Wasiliana nasi

    1 CDA Street, 40477

    Anuani ya posta: 1249, DODOMA, TANZANIA

    Simu: +255 26 232 4817

    Simu ya kiganjani:

    Baruapepe: cd@dodomacc.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya tovuti

Copyright ©2017 The City Council of Dodoma. All rights reserved.