OR-TAMISEMI
KAMATI ya kudumu ya Bunge ya Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa imetoa rai kwa Serikali kuhakikisha wanaweka mageti janja kwenye vituo vya kukatia tiketi ili kuongeza mapato na kuboresha huduma kwa watanzania
Rai hiyo imetolewa leo Mei 4, 2024 na Makamu Mwenyekiti wa Kamati hiyo Mhe. Justine Lazaro Nyamoga alipokuwa akifanya majumuisho ya ziara ya kikazi kwenye miradi ya ujenzi wa miundombinu ya mabasi yaendayo haraka na ujenzi wa soko la Kariakoo jijini Dar es salaam
Amesema haiwezekani kuona wananchi mpaka sasa bado wanapanga foleni kukata tiketi wakati mageti janja yameletwa na serikali ,lakini hajafungwa jambo hili linawakera wananchi na9 kurudisha nyuma maendeleo ya nchi
Ameendelea kufafanua kuwa lengo la serikali ni kuhakikisha inakusanya mapato kwa kutumia mifumo ya TEHAMA na kuwapunguzia adha wananchi ya kupanga foleni kusubiri huduma
Inshangaza kuona mpaka sasa wananchi wanapanga foleni kukata tiketi wakati katika kipindi hiki cha mabadiliko ya teknolojia ilikuwa inatakiwa wananchi kuwa na kadi maalum za huduma ya usafirishaji'amesisitiza Mhe Nyamoga
Amesema si vizuri kuwaacha wananchi wanapanga foleni kukata tiketi ambapo wanatumia muda mrefu ambapo kama serikali ni jukubu let kuhakikisha tunwarahisishia huduma wananchi
Aidha, wameipongeza serikali kwa kuhakikisha wanatumia wataalam wa ndani katika kuujenga mfumo wa matumizi ya mageti janja ambao utasaidia kupunguza mianya ya rushwa na kuongeza mapato
1 CDA Street, 40477
Anuani ya posta: 1249, DODOMA, TANZANIA
Simu: +255 26 232 4817
Simu ya kiganjani:
Baruapepe: cd@dodomacc.go.tz
Copyright ©2017 The City Council of Dodoma. All rights reserved.