OR-TAMISEMI
Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais - TAMISEMI (Elimu) Dkt. Charles Msonde amewataka watendaji wa Hamshauri nchini kushughulikia uhamisho wa walimu na watumishi wengine kwa kutumia mfumo uliowekwa ili kuondoa sitofahamu zinazojitokeza.
Dkt. Msonde ametoa maelekezo hayo kwenye kikao kazi cha majumuisho ya ziara ya katika mkoa wa Tabora kilichowakutanisha walimu,walimu wakuu,wakuu wa shule,Maofisa Elimu na wakurugenzi wa Halmashauri za mkoa wa huo kilichofanyika katika ukumbi wa shule ya Sekondari Mihayo Manispaa ya Tabora.
“Siku zote kuwa makini kuona kwenye mfumo tunapitisha nini kwasababu watu wameomba uhamisho ni lazima tuwapitishie ili mwenye mamlaka ya kuidhinisha uhamisho akiona haitahili yeye atakataa lakini sisi tuwapitishie kulingana na maombi yao, ” amesema
Dkt. Msonde amesisitiza kuwa endapo mkurugenzi atakuwa amebanwa na shughuli zingine na kushindwa kuingia kwenye mfumo anapaswa kukasimu mamlaka kwa mtu mwingine ili kuhakikisha maombi hayakai kwa muda mrefu na kuwaacha watumishi wakilalamika.
Akizungumza kwa niaba ya Wakurugenzi wa Halmashauri za Mkoa wa Tabora, Grace Quintine ambaye ni Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Urambo ameahidi kufanyia kazi maelekezo hayo na kuyasimamia ili kuwe na ufanisi katika sekta ya Elimu katika mkoani humo.
1 CDA Street, 40477
Anuani ya posta: 1249, DODOMA, TANZANIA
Simu: +255 26 232 4817
Simu ya kiganjani:
Baruapepe: cd@dodomacc.go.tz
Copyright ©2017 The City Council of Dodoma. All rights reserved.