WAZIRI Mkuu Kassim Majaliwa amesema Serikali ya awamu ya sita inayooongozwa na Mheshimiwa Rais Samia Suluhu Hassan imedhamiria kumaliza tatizo la upatikanaji wa huduma ya maji safi na salama katika vijiji vyote nchini vikiwemo vya Wilaya ya Ruangwa Mkoani Lindi.
Amesema suala la upatikanaji wa huduma ya maji safi na salama ni miongoni mwa vipaumbelel vya Serikali katika awamu hii, hivyo suala la upatikanaji wa huduma ya maji ni endelevu. “Tutaendelea kuboresha miradi ya maji ili maeneo yote nchini yapate maji ya uhakika.”
Mheshimiwa Majaliwa ametoa kauli hiyo leo tarehe 23 Julai, 2021 wakati akizungumza kwa nyakati tofauti na wananchi wa Wilaya ya Ruangwa kwenye mikunato ya hadhara iliyofanyika katika vijiji vya Mpara, Mtimbo, Mmawa, Chikoko, Chinokole na Kilimahewa walayani Ruangwa.
Waziri Mkuu amesema Serikali inatekeleza kampeni ya kumtua mama ndoo kichwani ili kuhakikisha wananchi wote nchini wanapata huduma hiyo karibu na maeneno yako ya makazi. Amewataka waendelee kuiamini Serikali yao kwa sababu imedhamiria kuwatumikia.
Akizungumza kuhusu tatizo la maji wilayani Ruangwa amesema Serikali inatekeleza ujenzi wa mradi wa maji wa Mbwinji ambao unatoa maji Ndanda hadi Ruangwa. “Mradi huu mkubwa unatarajiwa kupunguza kwa kiasi kikubwa tatizo la upatikanaji wa maji wilayani Ruangwa.”
Waziri Mkuu amesema mbali na huduma ya maji safi na salama, pia Serikali imedhamiria kusambaza umeme katika vijiji vyote ambavyo bado havijaunganishiwa nishati hiyo nchini, hivyo amewataka wananchi wafanye maandalizi ya kufikisha nishati hiyo katika makazi yao.
Amesema Mheshimiwa Rais Samia anataka kuona kila nyumba ya Mtanzania inapata umeme tena kwa gharama nafuu na ametenga fedha nyingi zitakazotosheleza kusambaza umeme nchi nzima vikiwemo na vijiji vya Ruangwa. Gharama za kuunganishiwa umeme huo ni shilingi 27,000 tu.
1 CDA Street, 40477
Anuani ya posta: 1249, DODOMA, TANZANIA
Simu: +255 26 232 4817
Simu ya kiganjani:
Baruapepe: cd@dodomacc.go.tz
Copyright ©2017 The City Council of Dodoma. All rights reserved.