Na. Asteria Frank
WATU wasiopungua 90 washiriki kwenye msafara wa kuendesha baiskeili kutoka Dar-es-salaam na kwenda Butihama kwa lengo la kumuenzi Baba wa Taifa Mwl. Julius Kambarage Nyerere wawasili Jijini Dodoma katika shule ya Msingi Dodoma Makulu.
Msafara huo wa Twende Butihama ulianza safari tarehe 30 Septemba kutoka Dar-es-salam na unatarajiwa kufika Butihama tarehe 13 Oktoba 2024, ukidhaminiwa na Vodacom Pamoja na Stanbic Bank walipokelewa na kukabidhi madawati 100 na kupanda miti katika shule ya Msingi Dodoma makulu.
Katibu Tawala Mkoa wa Dodoma, Kaspar Mmuya aliupokea vyema msafara huo wa Twende Butihama na alisema kuwa, upandaji miti unaunga Falsafa ya kutunza mazingira na utoaji wa madawati mashuleni unaugana na Falsafa ya Mwl Julius Kambarage Nyerere ya kuangamiza uadui wa Maendeleo ikiwemo Ujinga,Umaskini na Maradhi.
Alisema kuwa, kitendo wanachofanya ni kizuri kwa Tanzania cha kumuenzi Baba Taifa kwa kuendesha Baiskeli kutoka Dar-es-salaam mpaka Butihama kinaonesha uzalendo “nimeambiwa safari hizi zimefanyika zaidi ya miaka sita huku mkisema tunamuenzi Baba wa Taifa kwa vitendo ni ukweli nimeona wakati ulivyokuwa unatambalisha hapa sio Tanzania tu ni zaidi ya Tanzania na hayo ndio Maisha alikuwa akiishi Mwl Julias Kambarage Nyerere hakuwa mbinafsi alikuwa anapenda Umoja” alisema Mmuya.
Aidha, Naibu Meya wa Halmashauri ya Jiji la Dodoma Fadhili Chibago alisema kuwa Jiji la Dodoma tumefarijika sana kwa kuwapokea Twende Butihama kwa baiskeli kwakuwa wamefanya kitu kizuri na kwa zoezi la kupanda miti kwa maana Mhe.Rais Dkt Samia Suluh Hassan na Makamu wa Rais wetu watamani Dodoma iendelee kuwa Kijani.
Alisema kuwa upandaji wa miti unaunganisha Falsafa ya viongozi wetu wa Nchi lakini pia kitendo cha hawa ndugu kuleta madawati yatawafanya watoto wakae na wanaposoma waelewe vizuri “ tunawashukuru na tuwakaribishe sana Dodoma kwakuwa Dodoma ni fahari ya watanzania na ni mahali pa kuishi pia zabibu nzuri inapatika huku karibuni sana” alisema Chibago.
Naye Mwenyekiti wa Msafara wa Twende Butihama Gabriel Landa alisema kuwa wanatarajia kufika Butihama Oktoba 13 kwa lengo la kumuenzi Baba wa Taifa kwa vitendo na kwaajili ya kuadhimisha miaka 25 ya kumbukizi ya kifo cha Mwl. Julias Kambarage Nyerere tarehe 14 Oktoba.
Alisema kuwa Msafara huu umezingatia jinsi zote mbili ya wanawake na wanaume bila kusahau Watoto chini ya miaka 20. Pia umejumuisha waendesha baiskeli kati yao ni Tanzania Bara kama vile Arusha, Kilimanjaro, Tanga, Tabora, Mbeya, Iringa, Geita, Mwanza na Katavi Pamoja na Tanzania Visiwani ambayo ni Uguja na Pemba sio hivyo tu tupo na Nchi Jirani kama Kenya, Burundi, Malawi na Congo.
“Kuna falsafa nyingi sana alituachia baba wa taifa na moja wapo ya kupambana na maadui watutu wa maendeleo kama Ujinga, Umaskini na Maradhi, tumekuwa tukifanya hayo kwa kipindi chote tangia tumeanza mwaka 2019 na kupitia wadau mbalimbali tumeweza kukabidhi madawati zaidi ya 1000 katika shule zaidi ya 13 hadi kufikia mwaka jana lakini pia tumeweza kupanda miti zaidi ya 50,000 na kuhamasisha watanzania kujali afya” alisema Landa.
Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi Dodoma Makulu Amon Chalo Sebyiga alisema kuwa tunashukuru Twende Butihama kwa kutukabidhi madawati 100 kati ya madawati 212 yaliyo kuwa pungufu katika shule yangu.
Alisema kuwa makabidhio hayo yataenda kupunguza msongomano wa wanafunzi kukaa watu wa tano kwenye dawati moja “ jamii ya Dodoma Makulu na watu wanaozunguka eneo hili nawatakia safari njema ndugu zetu waTwende Butihama” alisema Sebyiga.
1 CDA Street, 40477
Anuani ya posta: 1249, DODOMA, TANZANIA
Simu: +255 26 232 4817
Simu ya kiganjani:
Baruapepe: cd@dodomacc.go.tz
Copyright ©2017 The City Council of Dodoma. All rights reserved.