Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan amekutana na kufanya mazungumzo na Waziri Mkuu wa Ubelgiji Mhe. Alexander De Croo, Brussels nchini Ubelgiji jana tarehe 17 Februari, 2022.
Katika mazungumzo hayo Mhe. De Croo alikubali ombi la Mhe. Rais Samia la kuisaidia Tanzania kujenga kiwanda cha kutengeneza dawa kwa ajili ya watoto pamoja na kuzalisha dawa ya covid.
Mhe. De Croo alipongeza mtazamo wa Mhe. Rais Samia kuhusu usalama wa ukanda wa nchi za Kusini mwa Jangwa la Sahara na rai yake kwa mataifa mbalimbali kuunga mkono msimamo wa Umoja wa Ulaya (EU) wa kufanya Burundi kuondolewa vikwazo.
1 CDA Street, 40477
Anuani ya posta: 1249, DODOMA, TANZANIA
Simu: +255 26 232 4817
Simu ya kiganjani:
Baruapepe: cd@dodomacc.go.tz
Copyright ©2017 The City Council of Dodoma. All rights reserved.