• Wasiliana nasi |
    • Maswali na majibu |
    • Baruapepe - Watumishi |
    • eVibali |
    • Malalamiko |
Dodoma City Council
Dodoma City Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Jiji la Dodoma

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa taasisi
    • Idara
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Mipango, Takwimu na Ufuatiliaji
      • Afya
      • Fedha na Biashara
      • Elimu ya Msingi
      • Elimu ya Sekondari
      • Maji
      • Kilimo, Umwagiliaji na Ushirika
      • Mifugo na Uvuvi
      • Ardhi na Mipango Miji
      • Maendeleo ya Jamii, Ustawi wa Jamii, Jinsia na Vijana
      • Ujenzi
      • Mazingira na Udhibiti wa Taka ngumu
    • Vitengo
      • Sheria na Usalama
      • Mkaguzi wa Ndani
      • TEHAMA na Uhusiano
      • Manunuzi
      • Uchaguzi
      • Ufugaji Nyuji
    • Ward
  • Fursa za Uwekezaji
    • Maeneo ya Utalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
    • Mji wa Serikali
    • Kwa nini uwekeze Dodoma?
  • Huduma Zetu
    • Maendeleo ya jamii
    • Elimu
    • Miundombinu
    • Mazingira
    • Afya
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Fedha na Utawala
      • Mipango miji na Mazingira
      • Uchumi, Afya na Elimu
      • Kudhitibi UKIMWI
      • Maadili
    • Kamati zingine/Bodi/Uwakilishi
    • Ratiba
      • Vikao vya Madiwani
      • Kuonana na Mstahiki Meya
  • Miradi
    • Miradi itakayotekelezwa
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Ripoti
    • Sheria Ndogo
    • Miongozo
    • Mpango Mkakati
    • Fomu
    • Jifunze Nyumbani
    • Mpango Kabambe
    • Jarida
    • Asemavyo Mahia - Afya na Mazingira
  • Kituo cha habari
    • Taarifa kwa vyombo vya habari
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya picha
    • Habari
    • Matukio
  • City TV

Ufugaji wa samaki katika mabwawa, vizimba kupunguza uvuvi haramu

Imewekwa tarehe: December 9th, 2020

Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Mashimba Ndaki amesema ufugaji wa Samaki katika Mabwawa na Vizimba ukihamasishwa na kupewa msukumo mkubwa utaongeza wingi wa samaki na utasaidia kupunguza uvuvi harama katika maji ya asili.

Ndaki aliyasema hayo alipotembelea Shamba la Waziri Mkuu Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mizengo Pinda lililopo jijini Dodoma Disemba 9, 2020.

Alisema kuwa serikali imefanya kazi kubwa katika kuimarisha sekta ya uvuvi ikiwemo ufugaji wa samaki katika vizimba na mabwawa lakini alisisitiza kuwa kunahitajika kuongeza nguvu na jitihada zaidi kuwahamasisha wananchi kujiingiza katika ufugaji wa samaki ili kujiongezea kipato na kupunguza utegemezi wa mazao ya samaki kutoka katika maji ya asili.

“Ufugaji wa samaki kwa kutumia vizimba na mabwawa utatusaidia kupunguza purukushani kati ya serikali na wavuvi haramu kwa sababu kama samaki wengi watapatikana kupitia ufugaji, watu hawataona haja ya kuhangaika na uvuvi usio na tija,” alisema Ndaki huku akiongeza kuwa;

“Tunahitaji kufanya jitihada zaidi kutangaza na kuhamasisha ufugaji wa samaki hasa kwa kutumia mabwawa ya gharama nafuu kama malambo ili wafugaji na wananchi kwa ujumla waweze kuona ufugaji huo ni nafuu na wanaweza kupata kipato kupitia kazi hiyo,” alisema Ndaki

Aliongeza kwa kusema kuwa hamasa ya ufugaji wa samaki ikiwa kubwa na wanunuzi nao wataongezeka jambo ambalo litapelekea pia kuongezeka kwa wawekezaji katika vyakula na ukuzaji wa vifaranga na hivyo kutatua changamoto iliyopo sasa ya uchache wa vifaranga na vyakula vya samaki.

“Ndani ya Wizara tutaona namna ya kujipanga ili tuendelee kuiwezesha zaidi hii sekta ya uvuvi iweze kukua zaidi na kuongeza kipato cha watu wetu na kutoa mchango mkubwa katika pato la Taifa,” alisisitiza Ndaki

Awali wakati akimkaribisha Waziri huyo Mteule Shambani hapo, Waziri Mkuu Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mizengo Pinda alisema kuwa changamoto kubwa anayoipata shambani hapo ni kutopatikana kwa urahisi kwa vifaranga vya samaki pamoja na chakula cha uhakika.

“Hapa tunapata changamoto ya vifaranga vya samaki havipatikani kwa urahisi lakini pia hakuna mahala ambapo unaweza kusema hapa wanazalisha chakula cha uhakika,” alisema Pinda

Aliongeza kwa kusema kuwa pamoja na jitihada kubwa za serikali katika kuimarisha sekta ya uvuvi lakini angetamani kuona sekta hiyo inaendelea kupewa nafasi kubwa zaidi hasa katika ufugaji wa samaki wa kutumia mabwawa na vizimba kwani utasaidia wananchi kujipatia kipato na kukuza uchumi wao.

Naye, Katibu Mkuu, Wizara ya Mifugo na Uvuvi (Uvuvi), Dkt. Rashid Tamatamah alisema kuwa kwa sasa serikali inaendelea kukarabati vituo vya uzalishaji wa vifaranga ili kuongeza uwezo wa kuzalisha ikiwemo kuimarisha mashamba darasa ili kufundisha watu namna ya kutengeneza chakula cha samaki na ufugaji wa samaki.

Dkt. Tamatamah aliongeza kuwa serikali inaendelea kuhamasisha uwekezaji katika uzalishaji wa vifaranga na uzalishaji wa Chakula na kwa sasa wapo katika mazungumzo na serikali ya Misri ili Kampuni zao ziweze kuwekeza katika uzalishaji mkubwa wa vifaranga na vyakula vya samaki hapa nchini.

Ndaki alifanya ziara hiyo muda mfupi baada ya kuapishwa rasmi kuwa Waziri wa Mifugo na Uvuvi Disemba 9, 2020, na kazi yake ya kwanza ilikuwa kutembelea machinjio ya Dodoma na Shamba la Waziri Mkuu Mstaafu, Mizengo Pinda.

Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Mashimba Ndaki akiwapa chakula Samaki katika moja ya Mabwawa ya samaki yaliyopo katika shamba la Waziri Mkuu (Mst) wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mizengo Pinda (wa kwanza kushoto) alipotembelea shamba hilo lililopo jijini Dodoma Disemba 9, 2020. Kushoto kwake ni Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Pauline Gekul.

Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Mashimba Ndaki(wa pili kutoka kulia aliyeinama) akikagua mbuzi wanaosubiria kuchinjwa alipotembelea Machinjio ya Dodoma yaliyopo jijini Dodoma Disemba 9, 2020. Wa kwanza kulia aliyeshika mbuzi ni Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Pauline Gekul. Wa kwanza kushoto ni Katibu Mkuu, Wizara ya Mifugo na Uvuvi (Mifugo), Prof. Elisante Ole Gabriel na wapili ni Meneja wa Machinjio ya Dodoma, Victor Mwita.


Matangazo

  • MKUTANO WA BARAZA LA WAHESHIMIWA MADIWANI January 30, 2025
  • KITUO CHA AFYA ILAZO KIMEANZA KUTOA HUDUMA January 13, 2025
  • HOSPITALI YA JIJI LA DODOMA IMEANZA KUTOA HUDUMA ZA AFYA January 12, 2025
  • TANGAZO LA UUZWAJI WA VIWANJA KIKOMBO December 03, 2024
  • Angalia zote

Habari za hivi punde

  • Barabara ya Lami ya Kilometa 6 yawanufaisha wakazi wa Kata ya Miyuji

    April 23, 2025
  • Huduma ya Chakula na Lishe yapandisha ufaulu Shule ya Sekondari Nala

    April 22, 2025
  • Mradi wa Maji Nala wa Bil. 1.3, mkombozi kwa wananchi

    April 22, 2025
  • Milioni 500 kukamilisha mradi wa Kituo cha Afya Kizota

    April 22, 2025
  • Angalia zote

Video

Watendaji Kata Wilaya ya Dodoma watakiwa kusimamia maswala ya Lishe
Video zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • Historia ya Manispaa
  • Wasifu wa Manispaa
  • Kata na Madiwani
  • Mji wa Serikali
  • Orodha ya Madiwani
  • Mpango Mkakati wa Halmashauri (SP)
  • Kwanini uwekeze Dodoma?
  • Zabuni za Wakala wa Ukusanyaji Mapato
  • Zabuni ya Usafi wa Mazingira

Viunganishi Linganifu

  • Msalato Sekondari
  • Mkoa wa Dodoma
  • OR-TAMISEMI
  • Utumishi
  • Chuo Kikuu Dodoma (UDOM)
  • Bunge

World visitors tracker

world map hits counter

Idadi ya watembeleaji

free HitCounter

Ramani elekezi

Wasiliana nasi

    1 CDA Street, 40477

    Anuani ya posta: 1249, DODOMA, TANZANIA

    Simu: +255 26 232 4817

    Simu ya kiganjani:

    Baruapepe: cd@dodomacc.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya tovuti

Copyright ©2017 The City Council of Dodoma. All rights reserved.