• Wasiliana nasi |
    • Maswali na majibu |
    • Baruapepe - Watumishi |
    • eVibali |
    • Malalamiko |
Dodoma City Council
Dodoma City Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Jiji la Dodoma

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa taasisi
    • Idara
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Mipango, Takwimu na Ufuatiliaji
      • Afya
      • Fedha na Biashara
      • Elimu ya Msingi
      • Elimu ya Sekondari
      • Maji
      • Kilimo, Umwagiliaji na Ushirika
      • Mifugo na Uvuvi
      • Ardhi na Mipango Miji
      • Maendeleo ya Jamii, Ustawi wa Jamii, Jinsia na Vijana
      • Ujenzi
      • Mazingira na Udhibiti wa Taka ngumu
    • Vitengo
      • Sheria na Usalama
      • Mkaguzi wa Ndani
      • TEHAMA na Uhusiano
      • Manunuzi
      • Uchaguzi
      • Ufugaji Nyuji
    • Ward
  • Fursa za Uwekezaji
    • Maeneo ya Utalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
    • Mji wa Serikali
    • Kwa nini uwekeze Dodoma?
  • Huduma Zetu
    • Maendeleo ya jamii
    • Elimu
    • Miundombinu
    • Mazingira
    • Afya
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Fedha na Utawala
      • Mipango miji na Mazingira
      • Uchumi, Afya na Elimu
      • Kudhitibi UKIMWI
      • Maadili
    • Kamati zingine/Bodi/Uwakilishi
    • Ratiba
      • Vikao vya Madiwani
      • Kuonana na Mstahiki Meya
  • Miradi
    • Miradi itakayotekelezwa
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Ripoti
    • Sheria Ndogo
    • Miongozo
    • Mpango Mkakati
    • Fomu
    • Jifunze Nyumbani
    • Mpango Kabambe
    • Jarida
    • Asemavyo Mahia - Afya na Mazingira
  • Kituo cha habari
    • Taarifa kwa vyombo vya habari
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya picha
    • Habari
    • Matukio
  • City TV

Ujenzi Uwanja wa Ndege Msalato unakuja

Imewekwa tarehe: September 13th, 2021

Na Rhoda Simba, Dodoma

WAZIRI wa Ujenzi na Uchukuzi, Prof. Makame Mbarawa, ameuagiza Wakala wa Barabara nchini (TANROADS) kuhakikisha kuwa wanasimamia ujenzi wa kiwanja cha Ndege cha kimataifa cha Msalato ili ukamilike kwa wakati na kwa viwango vilivyowekwa.

Waziri Prof. Mbarawa ameyasema hayo leo jijini hapa mara baada ya kutiliana saini na Mkandarasi mkataba wa mradi wa ujenzi wa kiwanja hicho unaofadhiliwa na Benki ya Maendeleo ya Afrika (AFDB).

Amesema kukamilika kwa ujenzi wa uwanja huo kutawezesha kutua kwa Ndege kubwa kama vile Airbus pamoja na Dreamliner katika Mkoa wa Dodoma. “Pia kiwanja hiki kitafungua fursa mbalimbali za kiuchumi kwa Mkoa wa Dodoma hivyo, TANROADS muhakikishe kuwa mkandarasi mnamsimamia ipasavyo ili kumaliza kazi hii kwa haraka na kwa ufanisi mkubwa”  ameagiza Prof. Mbarawa.

Nae Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Barabara nchini (TANROADS) Mhandisi Rogatus Mativila, akitoa taarifa fupi ya mradi wa ujenzi wa kiwanja hicho, amesema kitajengwa kwa awamu mbili.

“Awamu ya kwanza inahusisha kazi kuu mbili ambazo ni ujenzi wa barabara ya kuruka ndege na ujenzi wa majengo ikiwemo jengo la abiria” amesema Mtivila.

“Mkandarasi aliyepatikana kwa ajili ya kazi ya ujenzi wa barabara ya kuruka na kutua Ndege ni Sinohydro Corporation Limited in JV with M/S Beijing Sino-Aero Construction Engineering Co., Ltd and M/s China Jiangxi International Economic and Technical Cooperation CO. Ltd kutoka China” amesema Mtivila.

Pia, amesema awamu ya kwanza ya ujenzi huo itakapo kamilika kiwanja hicho kitakuwa na uwezo wa kuhudumia abiria milioni 1.5 kwa mwaka. “Mheshimiwa Waziri awamu ya pili ya mradi itatekelezwa kwa kutegemea mahitaji yatakayojitokeza ndani ya kipindi cha miaka 20, baada ya ujenzi wa awamu ya kwanza kukamilika” amesema Mtivila.

Aidha, amesema mradi wa ujenzi wa kiwanja hicho cha kimataifa Msalato, unatekelezwa kwa ufadhiri wa benki ya Maendeleo ya Afrika (AFDB) kwa fedha za mkopo nafuu.

Amesema AFDB, watatoa jumla ya Dola milioni 329.47 na serikali ya Tanzania itagharamia Sh. bilioni 127 ambapo fedha zitakazo changiwa na serikali ni pamoja na malipo ya fidia kwa wananchi watakao pisha ujenzi wa mradi.

Kadhalika amesema ujenzi wa kiwanja hicho utakapokamilika utarahisisha usafirishaji wa watu na bidhaa kutoka na kuingia katika jiji la Dodoma na kati ya Tanzania na nchi mbalimbali, kukuza utalii, uchumi na kuongeza ajira.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Miundombinu, Selemani Kakoso, amesema kitendo cha wizara hiyo kutiana saini mkataba wa ujenzi kimejibu maswali mengi yalikuwa yakihojiwa na wananchi juu ya hatima ya uwanaja huo. “Watu baada ya hayati Rais Magufuli kufariki waliona kama miradi hii ambayo alikua ameiasisi haitatekelezwa tena lakini leo hii tunashukuru Rais Samia Suluhu Hassan, ameweza kujibu maswali ya watu wengi” alisema Kakoso.

Vilevile, amesema kamati hiyo ipo tayari kutoa ushirikiano katika utekelezaji wa mradi huo ili ukamilike kwa wakati na kwa viwango vilivyowekwa.

 

Matangazo

  • MKUTANO WA BARAZA LA WAHESHIMIWA MADIWANI January 30, 2025
  • KITUO CHA AFYA ILAZO KIMEANZA KUTOA HUDUMA January 13, 2025
  • HOSPITALI YA JIJI LA DODOMA IMEANZA KUTOA HUDUMA ZA AFYA January 12, 2025
  • TANGAZO LA UUZWAJI WA VIWANJA KIKOMBO December 03, 2024
  • Angalia zote

Habari za hivi punde

  • Barabara ya Lami ya Kilometa 6 yawanufaisha wakazi wa Kata ya Miyuji

    April 23, 2025
  • Huduma ya Chakula na Lishe yapandisha ufaulu Shule ya Sekondari Nala

    April 22, 2025
  • Mradi wa Maji Nala wa Bil. 1.3, mkombozi kwa wananchi

    April 22, 2025
  • Milioni 500 kukamilisha mradi wa Kituo cha Afya Kizota

    April 22, 2025
  • Angalia zote

Video

Watendaji Kata Wilaya ya Dodoma watakiwa kusimamia maswala ya Lishe
Video zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • Historia ya Manispaa
  • Wasifu wa Manispaa
  • Kata na Madiwani
  • Mji wa Serikali
  • Orodha ya Madiwani
  • Mpango Mkakati wa Halmashauri (SP)
  • Kwanini uwekeze Dodoma?
  • Zabuni za Wakala wa Ukusanyaji Mapato
  • Zabuni ya Usafi wa Mazingira

Viunganishi Linganifu

  • Msalato Sekondari
  • Mkoa wa Dodoma
  • OR-TAMISEMI
  • Utumishi
  • Chuo Kikuu Dodoma (UDOM)
  • Bunge

World visitors tracker

world map hits counter

Idadi ya watembeleaji

free HitCounter

Ramani elekezi

Wasiliana nasi

    1 CDA Street, 40477

    Anuani ya posta: 1249, DODOMA, TANZANIA

    Simu: +255 26 232 4817

    Simu ya kiganjani:

    Baruapepe: cd@dodomacc.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya tovuti

Copyright ©2017 The City Council of Dodoma. All rights reserved.