WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amesema maamuzi yaliyofanywa na Serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Mheshimiwa Rais Samia Suluhu Hassan kumkaribisha muwekezaji wa ujenzi wa kiwanda cha mboloea cha Itracom ni sahihi kwa maendeleo ya sekta ya kilimo nchini.
Amesemi Serikali itasimamia ujenzi wa mradi huo ili kuhakikisha azma ya Mhe. Rais Samia ya kuendeleza sekta ya kilimo inafikiwa kwa sababu changamoto kubwa iliyokuwa inawahakabili wakulima wengi ni upatikanaji wa mbaolea ambayo inakwenda kuwa histori.
Waziri Mkuu ameyasema hay oleo Jumamosi, Januari 15, 2022 wakati akizungumza na uongozi wa wafanyakazi wanaojenga kiwanda hicho katika eneo Nala jijini Dodoma. “Serikali imedhamiria kuimarisha sekta ya kilimo ili Watanzania watakaoitegemea wapate mafanikao.
Mheshimiwa Majaliwa ambaye leo amefanya ziara ya kukagua maendeleo ya ujenzi huo amesema ameridhishwa na kasi ya ujenzi wake na kwamba Serikali inataka kuona Watanzani wengi wananufaika na uwekezaji huo. Ujenzi wa kiwanda hicho umefikia asilimia 52.
Ujenzi wa kiwanda hiki ni matokeo ya ziara ya Mheshimiwa Rais Samia nchini Burundi, lengo ni kuhakikisha tuzalisha mbolea hapa hapa nchini baada ya kutegemea kuagiza nje kwa kiasi kikubwa. Kiwanda hiki kinatarajiwa kuzalisha mbolea hapa nchini badala ya kutegemea kuagiza nje kwa kasi kikubwa. Kiwanda hiki inatarajiwa kuzalisha tani laki sita kwa mwaka.” amesema Majaliwa.
1 CDA Street, 40477
Anuani ya posta: 1249, DODOMA, TANZANIA
Simu: +255 26 232 4817
Simu ya kiganjani:
Baruapepe: cd@dodomacc.go.tz
Copyright ©2017 The City Council of Dodoma. All rights reserved.