• Wasiliana nasi |
    • Maswali na majibu |
    • Baruapepe - Watumishi |
    • eVibali |
    • Malalamiko |
Dodoma City Council
Dodoma City Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Jiji la Dodoma

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa taasisi
    • Idara
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Mipango, Takwimu na Ufuatiliaji
      • Afya
      • Fedha na Biashara
      • Elimu ya Msingi
      • Elimu ya Sekondari
      • Maji
      • Kilimo, Umwagiliaji na Ushirika
      • Mifugo na Uvuvi
      • Ardhi na Mipango Miji
      • Maendeleo ya Jamii, Ustawi wa Jamii, Jinsia na Vijana
      • Ujenzi
      • Mazingira na Udhibiti wa Taka ngumu
    • Vitengo
      • Sheria na Usalama
      • Mkaguzi wa Ndani
      • TEHAMA na Uhusiano
      • Manunuzi
      • Uchaguzi
      • Ufugaji Nyuji
    • Ward
  • Fursa za Uwekezaji
    • Maeneo ya Utalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
    • Mji wa Serikali
    • Kwa nini uwekeze Dodoma?
  • Huduma Zetu
    • Maendeleo ya jamii
    • Elimu
    • Miundombinu
    • Mazingira
    • Afya
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Fedha na Utawala
      • Mipango miji na Mazingira
      • Uchumi, Afya na Elimu
      • Kudhitibi UKIMWI
      • Maadili
    • Kamati zingine/Bodi/Uwakilishi
    • Ratiba
      • Vikao vya Madiwani
      • Kuonana na Mstahiki Meya
  • Miradi
    • Miradi itakayotekelezwa
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Ripoti
    • Sheria Ndogo
    • Miongozo
    • Mpango Mkakati
    • Fomu
    • Jifunze Nyumbani
    • Mpango Kabambe
    • Jarida
    • Asemavyo Mahia - Afya na Mazingira
  • Kituo cha habari
    • Taarifa kwa vyombo vya habari
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya picha
    • Habari
    • Matukio
  • City TV

Ujenzi wa miundombinu ya Barabara yarahisisha usafiri kwa wananchi Mtumba

Imewekwa tarehe: May 7th, 2025

Na. Leah Mabalwe, MTUMBA

Kata ya Mtumba yanufaika na ujenzi wa barabara pamoja na kalavati kwa gharama ya shilingi 73,000,000 kwa lengo la kurahisisha upatikanaji wa usafiri na usafirishaji katika eneo hilo.

Hayo yalielezwa na Diwani wa Kata ya Mtumba, Edward Maboje alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari waliotembelea kata hiyo kuona miradi ya maendeleo mbalimbali iliyotekelezwa na serikali kwa kipindi cha miaka minne. 

Diwani Maboje alisema kuwa kata yake imepata miundombinu mizuri ambayo inasaidia usafiri kupatikana kwa urahisi. “Katika kata hii ya Mtumba tulikuwa na changamoto ya ubovu wa barabara kwa kiasi kikubwa, hususan barabara za Mtaa wa Vikonje pamoja na barabara kutoka Mtumba Kibaoni hadi Shule ya Msingi Mtumba na hali hii ilikuwa ikiwapa changamoto wakazi wa mtaa huo kwasababu hapo mwanzo mvua zilipokuwa zikinyesha watu walikuwa wakipata shida kuvuka na kwenda sehemu nyingine” alisema Maboje.

Aliongeza kuwa wananchi wa Kata ya Mtumba wanafuraha kubwa kupata miundombinu hiyo. “Serikali imetuletea jumla ya shilingi 73,000,000 kwaajili ya ujenzi wa barabara hizi. Niseme kwamba toka ujenzi huu wa kalavati pamoja na kutengeneza barabara uanze ingawa sio kwa kiwango cha lami imeweza kuwarahisishia wananchi kuvuka na kwenda sehemu nyingine kwaajili ya kufuata mahitaji na hata wasafirishaji wanaweza kusafirisha watu pamoja na bidhaa kiurahisi” aliongeza Maboje.

Kwa upande wake mwananchi Cosmas Kanjongo alisema kuwa anaishukuru serikali kwa kuwajengea barabara ambayo inawasaidia kusafiri kwa haraka. “Kutokana na ujenzi huu wa kalavati pamoja na barabara hapa kwetu, tumesaidika sana. Kwanza kabisa hili kalavati linatusaidia kwa msimu huu wa mvua hatukupata madhara makubwa kwasababu linaruhusu maji kupita kiurahisi kuelekea sehemu zingine. Na hii barabara ilivyoboreshwa inatusaidia kwasababu inapitika kiurahisi, tunaweza kupitisha mizigo yetu kuelekea barabara kubwa” alisema Kanjongo.

Naye Celina Chibada aliipongeza serikali kwa kutatua changamoto ya barabara ambayo imeleta msaada kwa wanawake na watoto wanaotumia barabara hiyo.  “Kabla ya ujenzi huu wa barabara kulikuwa hapapitiki na mvua zilivyokuwa zinanyesha pikipiki zilikuwa hazipiti, sisi wanawake na watoto tulikua tunateseka sana kupita. Kwa sasa tunaishukuru sana serikali kwa kutujengea hii barabara pamoja na kalavati tunanufaika nayo sana” alipongeza Chibada.



Matangazo

  • MKUTANO WA BARAZA LA WAHESHIMIWA MADIWANI January 30, 2025
  • KITUO CHA AFYA ILAZO KIMEANZA KUTOA HUDUMA January 13, 2025
  • HOSPITALI YA JIJI LA DODOMA IMEANZA KUTOA HUDUMA ZA AFYA January 12, 2025
  • TANGAZO LA UUZWAJI WA VIWANJA KIKOMBO December 03, 2024
  • Angalia zote

Habari za hivi punde

  • Mstahiki Meya wa Jiji la Dodoma atoa pongezi kwa Madiwani

    May 25, 2025
  • Mkopo wa 10% tija kwa maendeleo ya vijana, wanawake na watu wenye ulemavu

    May 23, 2025
  • Mkopo wa 10% tija kwa maendeleo ya vijana, wanawake na watu wenye ulemavu

    May 23, 2025
  • Wananchi Kata ya Madukani washukuru kuboreshwa huduma za Afya, Zahanati ya Chikande

    May 21, 2025
  • Angalia zote

Video

Watendaji Kata Wilaya ya Dodoma watakiwa kusimamia maswala ya Lishe
Video zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • Historia ya Manispaa
  • Wasifu wa Manispaa
  • Kata na Madiwani
  • Mji wa Serikali
  • Orodha ya Madiwani
  • Mpango Mkakati wa Halmashauri (SP)
  • Kwanini uwekeze Dodoma?
  • Zabuni za Wakala wa Ukusanyaji Mapato
  • Zabuni ya Usafi wa Mazingira

Viunganishi Linganifu

  • Msalato Sekondari
  • Mkoa wa Dodoma
  • OR-TAMISEMI
  • Utumishi
  • Chuo Kikuu Dodoma (UDOM)
  • Bunge

World visitors tracker

world map hits counter

Idadi ya watembeleaji

free HitCounter

Ramani elekezi

Wasiliana nasi

    1 CDA Street, 40477

    Anuani ya posta: 1249, DODOMA, TANZANIA

    Simu: +255 26 232 4817

    Simu ya kiganjani:

    Baruapepe: cd@dodomacc.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya tovuti

Copyright ©2017 The City Council of Dodoma. All rights reserved.