WAZIRI Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Kassim Majaliwa amesema Serikaliya awamu ya sita inayoongozwa na Rais Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan itaendeleakuuboresha Mji wa Dodoma kwa kujenga miundombinu ya barabara, maji pamoja nanyumba za watumishi.
Waziri Mkuu Majaliwa ameyasema hayo Jumapili, Oktoba 31, 2021 baada ya kuweka jiwela msingi la ujenzi wa nyumba 1,000 za makazi zinazojengwa na Shirika la Nyumbala Taifa (NHC) katika eneo la Chamwino na Iyumbu Mkoani Dodoma.
Akifafanua zaidi amesema kuwa hivi karibuni Rais Samiaametoa shilingi Bilioni 20 ambazo ni mkopo nafuu kwa Shirika la Nyumba la Taifaili ziwe mtaji wa kujenga nyumba 1,000 katika maeneo ya Chamwino na Iyumbujijini Dodoma ambao hadi kukamilika kwake mradi huo utagharimu Shilingi Bilioni71 huku awamu ya kwanza ikitumia Bilioni 21.4 kukamilisha nyumba 404.
Majaliwa amesema kuwa Serikali itaendelea kuwekeza kwenyemiradi mikubwa ya ujenzi wa majengo ya Ofisi na Makazi kwa Watumishi wa Ummaili kupunguza gharama kubwa ya kodi ya pango pamoja na kuimarisha utendaji nauwajibikaji wa watumishi hao katika kuwahudumia Watanzania.
Aidha, Waziri Mkuu ameliagiza Shirika la Nyumba la Taifakukaa pamoja na DUWASA, TARURA na TANESCO ili kuona namna bora ya kushirikianana kufanikisha upatikanaji wa miundombinu hiyo muhimu na kupunguza mzigo wagharama kwa Shirika hilo ili miradi hiyo iweze kukamilika kwa wakati na kwagharama nafuu.
Waziri Mkuu Majaliwa amesema “Wakurugenzi wa Halmashaurihususan halmashauri mpya tumieni Shirika la Nyumba la Taifa pamoja na WatumishiHousing ili muweze kuharakisha ujenzi wa nyumba bora za watumishi waHalmashauri kwa gharama nafuu.”
Vilevile, Mheshimiwa Majaliwa ameliagiza Shirika hilokupunguza gharama za manunuzi kwa kununua vifaa kama mabati, mabomba, vigaekutoka kwa wazarishaji wa ndani ya nchi kwa kuweka oda maalum ili miradiikamilike kwa muda uliopangwa na kuhakikisha sheria na taratibu za manunuzizinafuatwa ipasavyo.
Awali, akizungumza baada ya kukagua ujenzi wa nyumba 100katika eneo la Chamwino, Waziri Mkuu aliipongeza Wizara ya Ardhi pamojana Shirika la Nyumba la Taifa kwa hatua ya ujenzi nyumba hizo pamoja nampango wa ujenzi wa nyumba za makazi.
Aidha, Mheshimiwa Majaliwa amewapongeza wafanyakaziwakitanzania walioshiriki katika ujenzi wa nyumba hizo ikiwa ni utekelezaji wamsisitizo wa Rais Samia Suluhu Hassan kuhusu ushirikishwaji wa watanzaniakatika ujenzi wa miradi mikubwa ya ujenzi.
Naye Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe.William Lukuvi, amesema Serikali kupitia Shirika la Nyumba la Taifa haitaruhusuutaratibu wa mtu mmoja kununua nyumba nyingi katika eneo hilo na kisha kuanzautaratibu wa kupangisha, ila watatoa fursa sawa kwa Watanzania wa kada zote iliwaweze kunufaika na mradi huo.
Mkurugenzi wa Shirika la Nyumba la Taifa Dkt. MaulidBanyani pamoja na kuishukuru Serikali kwa kutoa mkopo nafuu kwa Shirika hiloamesema awamu ya kwanza ya mradi wa nyumba 1,000 unaotekelezwa na Shirika hiloMkoani Dodoma ulianza Januari 6, 2021 kwa eneo la Iyumbu na Chamwino ulianzaFebruari 1, 2021.
“Mradi huu mkubwa unaohusisha ujenzi wa nyumba za makazi 1,000katika Jiji la Dodoma utagharimu Shilingi bilioni 71 hadi kukamilika ambapoawamu hii ya kwanza yenye nyumba 404 itagharimu shilingi bilioni 21.4 na kazikubwa ya ujenzi itakuwa imekamilika ifikapo Desemba 2021 na kubakiwa naukamilishaji wa kazi chache za nje ambazo nazo zitaisha mwezi Januari 2022.”
1 CDA Street, 40477
Anuani ya posta: 1249, DODOMA, TANZANIA
Simu: +255 26 232 4817
Simu ya kiganjani:
Baruapepe: cd@dodomacc.go.tz
Copyright ©2017 The City Council of Dodoma. All rights reserved.