Ujumbe wa watu watano kutoka Halmashauri ya Jiji la Dodoma ukiongozwa na Mstahiki Meya Profesa Davis Mwamfupe umewasili Jijini Linz nchini Austria leo Septemba 5, 2018 kwa ziara ya kikazi.
Awali, mwezi Machi 2017, ujumbe kutoka Halmashauri ya Jiji la Linz ukiongozwa na Naibu Meya bwana Detlef Wimmer ulitembelea Jiji la Dodoma katika ziara ya kikazi iliyolenga kujenga mahusiano ya karibu ya kiushirikiano baina ya Majiji hayo, ambapo mwishoni mwa ziara hiyo, aliyekuwa Mstahiki Meya wa Manispaa ya Dodoma Jaffari Mwanyemba na Naibu Meya wa Linz Detlef Wimmer walisaini Hati ya Makubaliano (Memorandum of Understanding) ya ushirikiano katika maeneo mbalimbali yanayohusu majukumu ya Halmashauri hizo katika kuwatumikia wananchi wao.
Ziara hii ni muendelezo wa utekelezaji wa makubaliano hayo na uhusiano mzuri ulioanzishwa kati ya Majiji haya, ambapo Mstahiki Meya wa Jiji la Dodoma ameambatana na Naibu Meya Mhe. Jumanne Ngede, Mkurugenzi wa Jiji Godwin Kunambi, Diwani wa viti maalum mhe. Joan Mazanda na Mkuu wa Idara ya Mipango, Takwimu na Ufuatiliaji Shabani Juma.
1 CDA Street, 40477
Anuani ya posta: 1249, DODOMA, TANZANIA
Simu: +255 26 232 4817
Simu ya kiganjani:
Baruapepe: cd@dodomacc.go.tz
Copyright ©2017 The City Council of Dodoma. All rights reserved.